Nimejaribu kulifanyia kazi swali lako ila sijapata majibu! Labda wewe ukipitia au kuuliza vizur unipe utofauti kati ya hiyo kamati yenye mamlaka hayo na Sekretarieti
Japo sio mwanasheria Nitajaribu kujibu kwa kuchangia Hoja ili tuelewane
Firstly Respond yangu ya swali ilitokana na kile ulichojibu wewe kwenye uzi huu kwa picha
comments #256 kwa kusema
bunge au kamati ya bunge halina Uwezo wa kurekebisha mkataba...
Naomba kukurekebisha kwa hapo kwa kusema Hiyo dhana
sio kweli Kwa mujibu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977
Sura ya 3 ibara ya 63 (3) kifungu kidogo (e) ambayo huweza kusomwa pamoja na
sheria Ya madaraka ya Bunge ya mwaka 1984 na 15 ibara ya 12. pamoja na
Sheria ya namba 4 ya 1992 ib.17 na Sheria ya 1992 Na.20 ib.11
"
Kwa madhumuni ya utekelezaji wa madaraka yake Bunge laweza kujadili na kuridhia mikataba yote inayohusu Jamhuri ya Muungano na ambayo kwa masharti yake inahitaji kuridhiwa".
katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Sura 3 ib 63 (3e))
so ulichokisema hapo haukuwa sahihi.....
Labda niende kwenye
Kanuni au Mwongozo na utaratibu wa kuridhia Mikataba ya Kimataifa ya mwaka 2017 Ambayo ndo ilikuwa hoja yako kuu...
jaribu kupitia Paragraph Ya Tatu ya utangulizi wa Mwongozo huo umeweka wazi kabisa kwamba maridhiano hayo hufanywa na kamati mbalimbali za Bunge...
Huenda kuna Tatizo linaweza kuja kuwa ni La
Uelewa Wa hasa Majukumu ya lini hasa Bunge linakuwa Kamati ya Bunge na lini hasa Bunge linaweza kuwa kama Sekretarieti na lini hasa Bunge Huwa kaM bunge, Tujitahidi kizisoma sana sheria haziuzwi ziko Mtandaoni na nyingi ni free.
Ok Nitajaribu kuelezea hivi vitu vitat
u,Bunge,Kamati ya Bunge na Sekretarieti Ya bunge...
Majibu yangu yanaweza yakawa marefu lakini Lengo ni kutoa Elimu
Ntaanza na Bunge
Ambapo bunge ni Mhimili au chombo kilichoanzishwa kwa Mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Tanzania Ya mwaka 1977 Ibara ya 62 ndiyo inayoweka uwepo wa Bunge la Tanzania. Ibara ya 63 na 64 za Katiba hiyo zinalipa Bunge mamlaka na madaraka lililonalo. Hivyo basi, Muundo wa Bunge pamoja na majukumu yake vimewekwa bayana katika Katiba ya nchi.Ikiwemo hiyo ya kuchambua na Kuridhia mikataba na sheria...
Majukumu ya Bunge yametamkwa katika Ibara ya 63 (2) ya Katiba ya Nchi, Nitaquote
“Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano, ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya Wananchi, ya kusimamia na kuishauri Serikali ya Muungano pamoja na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake “
Kamati Za Bunge..
Ibara ya 96 ya katiba ikisomwa pamoja na Sheria ya 1995 Na.12 Ibara 16 inalipa Bunge uwezo wa kuunda kamati za Bunge za namna mbali mbali kadri litakavyoona inafaa kwa ajili ya utekelezaji bora wa madaraka yake.
Ibara ya 89 inalipa Bunge mamlaka ya kutunga Kanuni za Kudumu kwa ajili ya kuweka utaratibu wa kutekeleza shughuli zake.
Sasa kwa mujibu wa kanuni za Bunge toleo la mwaka 2020 kuna Kamati Aina Tatu za Bunge kuna Kama ya bunge zima ,Kuna Kamati Teule na kuna Kamati za Kudumu...
Kuna kitu nataka ueleee hapa kabla kamati ya bunge zima haijakaa lazma kamati ndogondogo hizi zikae kujadili kwa kina hoja zake kwa mfano kabla halijajadiliwa swala la afya katika kamati ya Bunge zima lazma Kamati ya afya ya Bunge imekaa na imelijadili hilo Swala kabla ya kulipeleka Kamati ya Bunge zima kujadiliwa......
SASA TWENDE KWENYE SEKRETARIETI...
Sektretarieti Maana yake ni kwamba ni Mtu yoyote Au kikundi chchote kilichopewa mamlaka kisheria kuratibu utekelezaji wa shughuli fulani
kwa mujibu wa KANUNI ZA KUDUMU ZA BUNGE, TOLEO LA JUNI, 2020 sehemu ya 6 ibara ya 25
25.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ya 88 ya Katiba, Sheria ya Uendeshaji Bunge na Kanuni hizi kuhusu uwekaji wa nafasi na ngazi za utumishi, Ofisi ya Bunge itakuwa na Sekretarieti itakayoundwa na Idara, Sehemu na Vitengo mbalimbali kwa namna na idadi ambayo itaiwezesha kutoa huduma bora na kamilifu kwa Bunge, Wabunge na Kamati za Bunge.
(2) Katibu wa Bunge atakuwa Kiongozi wa Sekretarieti ya Bunge kwa mujibu wa Ibara ya 88(3) ya Katiba.
(3) Bila ya kuathiri masharti yaliyotangulia ya Kanuni hii, kutakuwa na Makatibu Wasaidizi wa Bunge, kwa idadi na ngazi mbalimbali kadri itakavyoamuliwa na Tume.
Tafsiri Katibu wa Bunge Akiwa kama Kiongozi wa sekretarieti ya Bunge nadhani tunaweza tukajua kwamba maamuzi ya Katibu wa Bunge hutoka Kw Spika wa Bunge kwani ndye Surbonate wake.....Yaani ndo Taswira yake kwa lugha nyepesi..
Kwahyo kwa kifupi ni kwamba Sekretariet,Bunge na Kamati za bunge ni KITU KIMOJA CHENYE MAJUKUMU TOFAUTI NA YENYE TASWIRA TOFAUTI ILA YENYE LENGO MOJA NA YALIYO NA BODI MOJA YA KIMAAMUZI...