Sekretarieti ya Bunge: Kuna mapungufu katika Mkataba wa Bandari na DP World; ukomo wake uwekwe wazi

Sekretarieti ya Bunge: Kuna mapungufu katika Mkataba wa Bandari na DP World; ukomo wake uwekwe wazi

Sawa tu, lakini hivi hili bunge ndilo lilipitisha huu mkataba, leo wanatoa haya maoni, je mwanzoni walikuwa hawajausoma hou mkataba wakagundua madhaifu yake na wayarekebishe?
Wanasema walitaka kula PESA ya mwarabu kwanza
 
Tumelumbana weee, tumeelezana weee, Kuna wale vichwa maji wakajifanya wajuaji kuliko hata wajuaji wenyewe. Haya Sasa huu hapa Waraka wa bunge na kwa kifupi wamekubali kuwa...
Sasa mbona wako busy kuwapotosha Watanzania. Hawa maccm ni ya ajabu sana.
 
Naomba mpendekeze wajumbe 9 nitakao ongozana nao kuelekea hifadhi ya wanyama Buligi ili wakashuhudie makabhiano ya hati ya umiliki wa hifadhi hiyo kwa spy aliyevujisha mkataba huu hatari zaidi duniani aitumie awezavyo kwa kipindi kischo zidi miezi 12.
 
Sawa tu, lakini hivi hili bunge ndilo lilipitisha huu mkataba, leo wanatoa haya maoni, je mwanzoni walikuwa hawajausoma hou mkataba wakagundua madhaifu yake na wayarekebishe?
Hongo Ilikuwa imewafumba macho mkuu.Ni hivii,hatuna Rais,hatuna Bunge,hatuna Speaker,hatuna Waziri Mkuu,na hatuna Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Judge Mkuu.Ni wazi kwa sasa we need a caretaker government itupeleke mpaka 2025 tutakapo chagua viongozi wapya.I suggest the necessary steps zianze kuchukuliwa ili tufanikishe hilo.Sauti ya Watanzania please lead the way,tuongozeni ku-demand Serikali ya CCM ijiuzulu.Future steps serikali ya CCM ikishaondoka madarakani ni straight forward.
 
Hongo Ilikuwa imewafumba macho mkuu.Ni hivii,hatuna Rais,hatuna Bunge,hatuna Speaker,hatuna Waziri Mkuu,na hatuna Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Judge Mkuu.Ni wazi kwa sasa we need a caretaker government itupeleke mpaka 2025 tutakapo chagua viongozi wapya.I suggest the necessary steps zianze kuchukuliwa ili tufanikishe hilo.Sauti ya Watanzania please lead the way.

Kama ulivyosema, hongo ni mbaya sana.

Yawezekana hao wote uliowataja wameshiriki kwa namna moja au nyingine.
 
Nimejaribu kulifanyia kazi swali lako ila sijapata majibu! Labda wewe ukipitia au kuuliza vizur unipe utofauti kati ya hiyo kamati yenye mamlaka hayo na Sekretarieti

Japo sio mwanasheria Nitajaribu kujibu kwa kuchangia Hoja ili tuelewane

Firstly Respond yangu ya swali ilitokana na kile ulichojibu wewe kwenye uzi huu kwa picha comments #256 kwa kusema bunge au kamati ya bunge halina Uwezo wa kurekebisha mkataba...

Naomba kukurekebisha kwa hapo kwa kusema Hiyo dhana sio kweli Kwa mujibu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 Sura ya 3 ibara ya 63 (3) kifungu kidogo (e) ambayo huweza kusomwa pamoja na sheria Ya madaraka ya Bunge ya mwaka 1984 na 15 ibara ya 12. pamoja na Sheria ya namba 4 ya 1992 ib.17 na Sheria ya 1992 Na.20 ib.11

"Kwa madhumuni ya utekelezaji wa madaraka yake Bunge laweza kujadili na kuridhia mikataba yote inayohusu Jamhuri ya Muungano na ambayo kwa masharti yake inahitaji kuridhiwa".
katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Sura 3 ib 63 (3e))


so ulichokisema hapo haukuwa sahihi.....

Labda niende kwenye Kanuni au Mwongozo na utaratibu wa kuridhia Mikataba ya Kimataifa ya mwaka 2017 Ambayo ndo ilikuwa hoja yako kuu...

jaribu kupitia Paragraph Ya Tatu ya utangulizi wa Mwongozo huo umeweka wazi kabisa kwamba maridhiano hayo hufanywa na kamati mbalimbali za Bunge...


Huenda kuna Tatizo linaweza kuja kuwa ni La Uelewa Wa hasa Majukumu ya lini hasa Bunge linakuwa Kamati ya Bunge na lini hasa Bunge linaweza kuwa kama Sekretarieti na lini hasa Bunge Huwa kaM bunge, Tujitahidi kizisoma sana sheria haziuzwi ziko Mtandaoni na nyingi ni free.

Ok Nitajaribu kuelezea hivi vitu vitatu,Bunge,Kamati ya Bunge na Sekretarieti Ya bunge...

Majibu yangu yanaweza yakawa marefu lakini Lengo ni kutoa Elimu

Ntaanza na Bunge

Ambapo bunge ni Mhimili au chombo kilichoanzishwa kwa Mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Tanzania Ya mwaka 1977 Ibara ya 62 ndiyo inayoweka uwepo wa Bunge la Tanzania. Ibara ya 63 na 64 za Katiba hiyo zinalipa Bunge mamlaka na madaraka lililonalo. Hivyo basi, Muundo wa Bunge pamoja na majukumu yake vimewekwa bayana katika Katiba ya nchi.Ikiwemo hiyo ya kuchambua na Kuridhia mikataba na sheria...

Majukumu ya Bunge yametamkwa katika Ibara ya 63 (2) ya Katiba ya Nchi, Nitaquote

“Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano, ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya Wananchi, ya kusimamia na kuishauri Serikali ya Muungano pamoja na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake “

Kamati Za Bunge..

Ibara ya 96 ya katiba ikisomwa pamoja na Sheria ya 1995 Na.12 Ibara 16 inalipa Bunge uwezo wa kuunda kamati za Bunge za namna mbali mbali kadri litakavyoona inafaa kwa ajili ya utekelezaji bora wa madaraka yake.
Ibara ya 89 inalipa Bunge mamlaka ya kutunga Kanuni za Kudumu kwa ajili ya kuweka utaratibu wa kutekeleza shughuli zake.

Sasa kwa mujibu wa kanuni za Bunge toleo la mwaka 2020 kuna Kamati Aina Tatu za Bunge kuna Kama ya bunge zima ,Kuna Kamati Teule na kuna Kamati za Kudumu...

Kuna kitu nataka ueleee hapa kabla kamati ya bunge zima haijakaa lazma kamati ndogondogo hizi zikae kujadili kwa kina hoja zake kwa mfano kabla halijajadiliwa swala la afya katika kamati ya Bunge zima lazma Kamati ya afya ya Bunge imekaa na imelijadili hilo Swala kabla ya kulipeleka Kamati ya Bunge zima kujadiliwa......

SASA TWENDE KWENYE SEKRETARIETI...

Sektretarieti Maana yake ni kwamba ni Mtu yoyote Au kikundi chchote kilichopewa mamlaka kisheria kuratibu utekelezaji wa shughuli fulani

kwa mujibu wa KANUNI ZA KUDUMU ZA BUNGE, TOLEO LA JUNI, 2020 sehemu ya 6 ibara ya 25

25.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ya 88 ya Katiba, Sheria ya Uendeshaji Bunge na Kanuni hizi kuhusu uwekaji wa nafasi na ngazi za utumishi, Ofisi ya Bunge itakuwa na Sekretarieti itakayoundwa na Idara, Sehemu na Vitengo mbalimbali kwa namna na idadi ambayo itaiwezesha kutoa huduma bora na kamilifu kwa Bunge, Wabunge na Kamati za Bunge.

(2) Katibu wa Bunge atakuwa Kiongozi wa Sekretarieti ya Bunge kwa mujibu wa Ibara ya 88(3) ya Katiba.
(3) Bila ya kuathiri masharti yaliyotangulia ya Kanuni hii, kutakuwa na Makatibu Wasaidizi wa Bunge, kwa idadi na ngazi mbalimbali kadri itakavyoamuliwa na Tume.

Tafsiri Katibu wa Bunge Akiwa kama Kiongozi wa sekretarieti ya Bunge nadhani tunaweza tukajua kwamba maamuzi ya Katibu wa Bunge hutoka Kw Spika wa Bunge kwani ndye Surbonate wake.....Yaani ndo Taswira yake kwa lugha nyepesi..

Kwahyo kwa kifupi ni kwamba Sekretariet,Bunge na Kamati za bunge ni KITU KIMOJA CHENYE MAJUKUMU TOFAUTI NA YENYE TASWIRA TOFAUTI ILA YENYE LENGO MOJA NA YALIYO NA BODI MOJA YA KIMAAMUZI...

 
11B4676C-46A9-4C83-9A9A-9D809D6B1E3A.jpeg



Kama kanuni zetu za kuingia mikataba zinasema mtu yeyote mwenye mamlaka ya sehemu husika anaweza sign mkataba kwa niaba ya Tanzania; kwanini tudhani ni tofauti upande wa Dubai.

Isitoshe hizo sign hazina nguvu yoyote za kimkataba isipokuwa ridhaa ya bunge tu. Sasa kwanini mtu akadhane na petty issues.

Mengine yote serikali imeshayatolea ufafanuzi wa kutosha; ambae ajaelewa mpaka sasa hataki kuelewa tu including hawa wanaojiita ‘sekretariat ya bunge’.

Hii ni salamu tosha kwa ‘Bi Tozo’ resistance iliyopo huko ndani katika vyombo vya serikali juu ya uongozi wake.

IGA aina shida yoyote, sasa labda inawezekana kuna mambo mengine ya ndani ambayo hatuyajui kuhusu huu mkataba ambao watu wanatumia nguvu sana kupotosha.

Pengine wamechoshwa na ufisadi mkubwa unaoendelea sehemu zingine hii IGA wanaitumia kama fimbo ya kumchapia tu.
 
Duh!...mbona uliridhiwa kwa mbwembwe mno, kweli hatuna bunge.

Kalamu Nguruvi3 JokaKuu
Walitishiwa na spika wao, kwamba "rais anaweza kuvunja bunge"!

Hawa ni watu wazima, wengi wakijidai ni wasomi kwa kiwango cha kuridhisha, na wanajua dhahiri kabisa kuwa wapo hapo Bungeni siyo kujiwakilisha wao wenyewe, bali wananchi.

Sasa mtu unajiuliza, hii CCM hasa imefikafikaje ngazi ya chini kiasi hiki?

Kumbuka, chimbuko la chama hiki ni chama cha wafanyakazi na wakulima, wananchi walio wengi ndani ya nchi hii.
Imekuwakuwaje, hadi chama kikageuka na kuwa Chama cha Mafisadi?

Ni nani atakayekiokoa chama hiki kisididimie moja kwa moja na kupotea kabisa?
 
Kama kanuni zetu za kuingia mikataba zinasema mtu yeyote mwenye mamlaka ya sehemu husika anaweza sign mkataba kwa niaba ya Tanzania; kwanini tudhani ni tofauti upande wa Dubai
Wakati mwingine sijui akili yako huwa unaipeleka wapi. Hili nalo ni jambo la kuandika humu watu walisome na wakubaliane na hoja yako?
 
Back
Top Bottom