Tetesi: Seneti ya Marekani itajadili hali ya Kisiasa Tanzania wakati wowote mwezi huu, hapa CCM lazima wapoteane

Labda Siku nikiona vijana wamekaa makundi makundi nchi nzima wakiwa na hasira na serikali huku Polisi wakiwa hawatoshi na hawaelewi wapeleke nguvu eneo lipi kukabiliana na hasira za vijana ndo ntajua serikali ipo matatani.
 
oh hoo D.Trump asije tandika missile kama kule irani au yemeni, huyu jamaa hatabiriki tuizidi kuiombea nchi yetu …
Alafu huyu jamaa anatandika missile sehemu nyeti ambako nyani wamekusanyika.... Bahati nzuri wale jamaa wa Yemen wanaishi chini ya miamba migumu... Hawa wakwetu wanajikusanya pale bungeni wakisifiana ujinga sijui itakuaje 😄
 
chadema wanabeba na kutaka kutawanya hoja zisizo na maadili ya kiafrika wao ni mawakala wa holo hivyo kuwadhibiti ni jambo la muhimu kama watanzania
 
Sijui kama wataendelea kushupaza shingo😆😁🇪🇺🇪🇺🇪🇺🇺🇲🇺🇲🇺🇲🇺🇲🇺🇲🇺🇲🇺🇲 bado UK.
 
Lazima wajadili, huwezi fanya Jaribio la kumuua KITIMA, na Papa wa Sasa katokea Marekan, alafu Trump akae kimya??.


Na walivyo wapuuzi, mtuhumiwa wao walomkamata ukifika usiku ,wanamrudisha kwake kulala
shida inakuja pale kitima ameumizwa, maaskofu wote wamelalamika, watu wanatekwa na kesi ya Lisu, afu mkuu wa nchi anampongeza papa Leo kwa kuteuliwa. hivi unafikiri papa atamsikiliza nani kati yako na hao maaskofu?
 
Huwa mnazima sana nyie ccm mnawadanganya wanannchi hampangiwi wakati huwohuwo deni unalodaiwa ni tilioni tisini na saba na ni hela za haohao unaosema wasikuamulie
 
uropokaji ni kazi rahisi sana gentleman,

yaani pamoja na matatizo yake yote iliyonayo marekani, iache kushughulikia wananchi wake ibabaike na Tz,
hiyo si nonsense kabisa aise 🐒
Unadhani inapotoa $450M kwa mwaka kukusaidieni masikini nyie haina shida zake za ndani?
Mnajua kuropoka tuu, lakini uhalisia hamtaki kuujua wala kuutafuta!
Ila ufumbuzi wa hili ni kwa wao US kuminya kidogo tu huko kwenye misaada na kudili zaidi kwa kuweka vikwazo kwa viongozi. Wasikanyage US na wale wa EU wawazuie na accts zao pia wafunge ndio mtakapojua!
 
Halafu wanakuja na azimio la kushinikiza hoja ya Braza K kuwa turuhusu ushoga.
 
Moja ya vikwazo ambavyo Marekani yaweza kuweka ni kusitisha uanachama wa AGOA kwa muda usojulikana au kuongeza kiwango cha ushuru na tozo kwa bidhaa kama adhabu.

Ngojea tuangalie kwanza orodha ya vikwazo ambavyo Marekani yaweza kuiwekea Tanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…