Sensa 2022: Tanzania ina idadi ya watu 61,741,120

Sensa 2022: Tanzania ina idadi ya watu 61,741,120

Kwa mamlaka niliyopewa na katiba ya JMT ya mwaka 1977, nawatangazia kuwa Tanzania ina idadi ya watu 61,741,120.

What was the population of Tanzania 2012 census?


44,928,923

The 2012 Population and Housing Census results show that, Tanzania has a population of 44,928,923 of which 43,625,354 is on Tanzania Mainland and 1,303,569 is in Tanzania Zanzibar.
1667212970433.jpeg

National Bureau of Statistics - Home › references

Tanzania in Figures 2012 - National Bureau of Statistics

 
Nani alikudanganya huo ni uhalisia wa sayansi??
Mbona kama hesabu hii iinapingana na uhalisia na sayansi pia? iweje wanawake na wanaume tupishane kwa gap ndogo hivyo? wanawake walipaswa kuwa 55% wanaume 48% atleast.
 
Hivi angeitisha tu Press conference pale Ikulu kwa ajili ya kuutangazia umma kilichomo kwenye taarifa ya sensa akiambatana na maafisa wawili watatu wa takwimu na Msemaji wa ikulu KUNGEKUWA NA SHIDA GANI?

kulundika watu wote hao na kuwalipa per diem huku V8 zikiunguruma na tayari Taifa lina mahitaji meeengi sana ni kushindwa kufikiri vizuri.
Acha roho ya kimaskini tafuta fursa uwe miongoni mwao maisha ya hivi yatafanya upate magonjwa ya sonona
 
Tanzania bara, mkoa wa DSM unaongoza kwa watu nchini, wapo 5,383,728 sawa na asilimia 8.7 ya watu wote nchini, na mkoa wa pili ni mwanza wenye wakazi 3,696,872 sawa na asilimia 6.
Dar es Salaam, DSM, Bongo sidhani kama itakuja kuacha kuongoza kwani waliopo wanazaliana na wengine wanaamia kwa kasi!
 
Watu wote wa Tanzania 61m ni sawa na idadi ya watu waishio mjini Lagos-Nigeria [emoji23]
We jamaa muongo na mpotoshaji

Lagos ni ya 2 Nigeria kwa watu
Ya kwanza ni Kano

Duniania ya Kwanza ni Tokyo na watu 37mil
 
Nawasalimu kwà jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!

Asee huku sio poa kabisa. Nipo uwanjani hapa, jua kali kinoma, sauti ndogo, bora nitoke nikatizame kwenye Tv

Naamini kwenye tv mtakua mnaenjoy sana.
Wewe TISS kwanini unawahi kutoka kabla ya kumaliza kazi?

Wasalimie Chamwino-Ikulu.
 
Acha roho ya kimaskini tafuta fursa uwe miongoni mwao maisha ya hivi yatafanya upate magonjwa ya sonona

Siko tayari kuishi kwa kudhulumu wengine, maana ya kuwa mtumishi wa umma ni kuhakikisha unatatua matatizo ya umma na sio kufuja mali za umma.

Kuna watu wengi wanavuja jasho usiku na mchana na kulipa makodi kila mahala ili wananchi wengi wapate huduma bora na kwa wakati.

Ni dhambi kubwa sana ukiwa umepewa dhamana na wewe kuitumia hiyo dhamana kujinufaisha na sio kutumika kwa manufaa ya waliokupa dhamana.

Kuwa mwajiriwa kwenye ofisi za umma maana yake umepewa dhamana kutumikia umma na sio kuukandamiza umma kwa kutumia hizo nafasi.
 
Salam

Binafsi zijaona mantiki yoyote Ile kufanyika sherehe kubwa et kutangaza tu idadi ya watu
Zoezi Hilo lingeweza kufanyika ikulu tu na kuhudhuriwa na waratibu wa zoezi la sensa na waandishi wa habari

Kwa haraka haraka sherehe zile zimegharimu sio chini ya 800m

Pesa hizi zingeweza kuchimba visima vingi sana

Nawasilisha...
 
Back
Top Bottom