Sensa 2022: Tanzania ina idadi ya watu 61,741,120

Sensa 2022: Tanzania ina idadi ya watu 61,741,120

Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan akitangaza matokeo ya Sensa Mwaka 2022

Ameainisha kuwa, kwa sasa nchi ina watu 61,741,120.

Dar es Salaam ikiwa na watu 5,383,728 ambayo ni 8.7% ya idadi ya watu kwa nchi nzima.

⁃ Mwanza ikiwa na watu 3,699,872 ambayo ni 6% ya idadi ya watu kwa nchi nzima
 
Tuko vizuri
 
Hivi angeitisha tu Press conference pale Ikulu kwa ajili ya kuutangazia umma kilichomo kwenye taarifa ya sensa akiambatana na maafisa wawili watatu wa takwimu na Msemaji wa ikulu KUNGEKUWA NA SHIDA GANI?

kulundika watu wote hao na kuwalipa per diem huku V8 zikiunguruma na tayari Taifa lina mahitaji meeengi sana ni kushindwa kufikiri vizuri.
Nikweli, kamanchi tuko kwenye hatari ya njaa kali huku viongozi wanaitana eti kusoma taarifa... shame!!
 
Naamini kutakuwa na takwimu sahihi kwa maendeleo na mgawanyo sahihi wa keki ya taifa. Kipindi cha mwendazake si ajabu takwimu zingepikwa ili tu chattel ionekane ina watu wengi. Ili iwe mkoa na hatimaye jiji.. (Apumzike panapo mstahili)

PS

Mkoa kama wa Mbeya, una wakazi wengi, una changia Pato la serikali kwa kiasi kikubwa. Ila hamna barabara "double road"

Miundombinu duni, mji haujapangika, ardhi wana pima viwanja halafu wanapotea.. Umeme, maji, barabara kazi kwa wanunuzi kukarabati, Rejea viwanja vya iduda, mbeya peak, isyesye.
Mtaachaga lini kulalamika? Kutwa kucha... Wewe umetimiza ya familia yako yote?

Mimi mwenye napingana na mambo mengi tu yanayoendelea, lakini si kila taarifa ya Serikali ni kupinga pinga tu
 
Sio MAJIJI yenye watu wengi ni MIKOA YENYE WATU WENGI MZEE.
MWANZA INA WILAYA ZAKE KIBAO AMBAZO HAZIPO KWENYE JIJI.
 
Nawasalimu kwà jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!

Asee huku sio poa kabisa. Nipo uwanjani hapa, jua kali kinoma, sauti ndogo, bora nitoke nikatizame kwenye Tv

Naamini kwenye tv mtakua mnaenjoy sana.
Kuenjoy nini hasa
 
Rais kadanganywa kwenye namba Jumla ni 61,741,130 na sio 61,741,120

Yaleyale ya Makamba!
Data zako uhalali wake wa kisheria na kitaaluma ni upi hadi uchallenge za Mhe. Rais? Tuwekee hapa.🙏🙏🙏
 
Huo ni uongo mkubwa, yani ety kutoka 2025 mpaka 2050 tuwe zaidi ya watu 150m 😳 yani kwa miaka 10 watu wameongezeka 10m sasa kwa miaka 25 itakuaje waongezeke watu 60m.? Watu mnaleta siasa hadi kwenye uhalisia.
 
Binadamu bwana,sasa jamani si ndio pesa inazunguka hivi...kuna watu leo familia zao zitaenda chooni..ndio mambo ya riziki yalivyo..kuna watu leo Mungu kajibu maombi yao kupitia hili tukio! .
 
Huko unakoita kufuja pesa nako kunachochea uchumi.

Imagine wewe Leo ingekuwa kampuni yako inalipwa kutokana na mapambo Tu ya event husika, ungesema kuna ufujaji? serikali ikitumia hela zinarudi Kwa wananchi...ni Bora government spending kuliko kubana bana matumizi kupita kiasi
Pesa hizo pia zukitibu wagonjwa au kupeleka maji kijijini kipi nafuu sasa
 
Huo ni uongo mkubwa, yani ety kutoka 2025 mpaka 2050 tuwe zaidi ya watu 150m 😳 yani kwa miaka 10 watu wameongezeka 10m sasa kwa miaka 25 itakuaje waongezeke watu 60m.? Watu mnaleta siasa hadi kwenye uhalisia.
Fertility rate inaongezea,last sensa ilikuwa 2.7 na Kwa hesabu za Leo iko 3.2 so inazidi kuongezeka maana vijana ni wengi na wanaokufa wanakuwa wachache..
 
Huo ni uongo mkubwa, yani ety kutoka 2025 mpaka 2050 tuwe zaidi ya watu 150m [emoji15] yani kwa miaka 10 watu wameongezeka 10m sasa kwa miaka 25 itakuaje waongezeke watu 60m.? Watu mnaleta siasa hadi kwenye uhalisia.
Ulitumia kiungo gani kusikia?
Hakuna sehemu wamesema Tumeongezeka 10mil

Ongezeko ni watu milioni 16+ ndani ya miaka 10

Matarajio ni kufikia watu 100+mil mwaka 2050
 
Back
Top Bottom