Sensa 2022: Tanzania ina idadi ya watu 61,741,120

Sensa 2022: Tanzania ina idadi ya watu 61,741,120

Kutangaza idadi ya watu mpaka pawepo na misafara ya v-8 wakati uswahili maji hayatoki bombani, hizo pesa wanazochezea wangekuwa wanazitumia hata kuchimba visima ningewaona wa maana, wao wanawaza anasa tu.
Yaani mambo mengine ya aibu na yanakera sana baasi tu
 
Rais nchi hii ni sawa na demigod
Utapewa jina Baya lakini ukweli utabaki ukweli. Nilishangaa suala la Lishe kufanywa agenda kubwa wakati cha maana tulichoelezwa kinajulikana siku nyingi. Kuleni Kuku, mayai, mboga, samaki, maziwa. Msile nafaka zilizokobolewa Kwa wingi,
Hili Tu mpaka tutangaziwe na Rais na watu wakaambiwe Dodoma.
 
Sio haba, nguvu kazi tunayo ya kutosha.

sasa tupange maendeleo.

kutoka mwaka 2012 hadi 2022 kuna ongezeko la watu 16, 812,197 sawa na 3.2%
 
Yaani kutangaza tu idadi, mpaka budget.Hii nchi bwana. Miaka kumi ijayo tutakuwa million 100 . Maweeeee kwa huduma zipi za jamii ????
 
Nawasalimu kwà jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!

Asee huku sio poa kabisa. Nipo uwanjani hapa, jua kali kinoma, sauti ndogo, bora nitoke nikatizame kwenye Tv

Naamini kwenye tv mtakua mnaenjoy sana.
Kwanini ulienda?
 
Hivi angeitisha tu Press conference pale Ikulu kwa ajili ya kuutangazia umma kilichomo kwenye taarifa ya sensa akiambatana na maafisa wawili watatu wa takwimu na Msemaji wa ikulu KUNGEKUWA NA SHIDA GANI...
Au wangejifungia ikulu yoyote ile Dar au Chamwino kama wanavyofanyaga wakati wanapeana ulaji(kuapishana) na wakatuacha walala hoi tuendelee kuwakusanyia Kodi,tozo na pesa ya kununulia asali yao.
 
Mimi nimetoa mfano wa mapambo Kama kampuni moja Tu hapo kwenye event....but kutakuwa na kampuni nyingi tofauti zinaipwa Kwa kila event...
Mkuu lakini si wajua serikali ina vitengo vingi.

Kwahiyo huenda baadhi ya shughuli unazodhani imepewa kampuni fulani kumbe ni kitengo fulani serikalini/jeshini ndio husimamia na serikali haijatoa mshiko coz ni kazi yao na wana mishahara kwa kazi hiyo.

Ni kama wanavyowatumia jkt kwenye shughuli mbalimbali za kiserikali, sawa wanamegewa fungu lakini lile fungu haliwafikii wale wachakarikaji pale moja kwa moja coz wana mishahara mwisho wa mwezi.
 
Write your reply...Hili linchi ni upigaji tu kwa kwenda mbele yani kutangaza hivyo tu ndio .....ngoja niishie hapo duh
 
Back
Top Bottom