Sensa: Kianalogia siku 1, kidigitali siku 7! Could there be something wrong somewhere?! Kesho mwisho! Je, ambao bado hawajafikiwa watahesabiwa?!

Anyway najua hauko serious na hoja yako sensa zote nilizo hesabiwa sikuwahi kupewa namba na hakuna kitu kama hicho kitakuja tokea.
Bila namba uchakataji wa takwimu utafanyikaje? Labda, namba atapewa Kila mtu baada ya kukusanya takwimu zote makao makuu. Nadhani namba ni muhimu katika uchakataji wa takwimu kwa usasa zaidi (Nawaza!!)
 
Mbona mimi kwangu haikuchukua dakik nyingi kuhesabiwa ? Ni kima dakik 5 tu Na maswali pia hayakuwa mengi ni kama maswali 5 t hayakuzidi apo
Inategemea karani mengine kaamua kuyapotezea!
Lkn pia Kwa wanawake waswali km umeolewa? Mmeachana ? Kwa muda gani,au ndoa Ina muda gani?
Umewahi kuzaa, au mimba iliyoharibika nk
Maswali mengi mpk unajiuliza
 
Kama dsm tu kitovu cha nchi siku ya saba leo hujahesabiwa, huku mikoani ni majanga, hadi sasa hakuna hata dalili kuwa nitahesabiwa. Sensa ya kidigitali mliyojinasibu kuitekeleza ni ipi?! Hii sensa ni ya hovyo kabisa kupata kuishuhudia!
 
At least umenifikirisha
Haingii akilini maswali km yale eti ndo sensa jmn
 
Hivi Kuna tofauti gani kati ya kayak na familia?
 
USIPOTOSHE UMMA
KAMA HUJUI TULIA

MWAKA 2012 SENSA ILIFANYIKA KAMA IFUATAVYO
1. SEMINA DODOSO REFU SIKU 14
2.SEMINA DODOSO FUPI SIKU 7
3. ZOEZI LA KUHESABU SIKU 7
TOFAUTI ULIOPO
1SEMINA MWAKA HUU SIKU NYINGI ZAIDI
2.KUNADODOSO LA MAJENGO AMBALO HALIKUWEPO MYAKAYA NYUMA
3.IDADI YA MASWALI NI MENGI ZAIDI
4. POSHO ZA MWAKA HUU NAZO PIA ZINAMVI
 
Update
Hatimaye leo nimehesabiwa!.
Pia nimemsikia Kamishna wa Sensa, Anna Makinda, ametoa tangazo kuwa yeyote ambaye hajahesabiwa, aende ofisi ya serikali ya mtaa wake, akaripoti kuwa hajahesabiwa na kuacha contact number yake, hivyo makarani wa sensa watampigia na kumfuata kumhesabu, hivyo sasa ni Watanzania wote wenye simu ndio watahesabiwa. Ikitokea wewe ni Mtanzania na hujahesabiwa, na hauna simu, then sijui utahesabiwaje?!.

Ila pio dodoso la sensa, lime miss swali moja muhimu sana, na kwangu mimi hilo swali ndilo lenye umuhimu wa pili baada ya swali la kitambulisho cha taifa, hili ni dodoso kuhusu Tin Number na umiliki wa leseni ya biashara.

Nilibahatika kuhudhuria ile semina ya Prof. Hernando De Sotto kuhusu formalization of properties, kila Mtanzania anayefanya biashara yoyote, anapaswa kuwa na Tin Number, na leseni ya biashara ili kujua the tax base!. Kulikiwa ma maswali mengi kuhusu biashara, umachinga, ufugaji, uchimbaji madini but none is as important as tin number na leseni ya biashara!.
Tukisema Tanzania bado tunatatizo la upangaji vipaumbele vyetu, tutakuwa tunajionea Tanzania bado tuna tatizo la upangaji vipaumbele vyetu, baada ya Elimu, Afya na kilimo, ilipaswa ije nishati!. Ni aibu na hatari kupikia kuni na mkaa!

Thanks kwa kuhesabiwa!.
P
 
Hivi Kuna tofauti gani kati ya kayak na familia?
Mkuu ngaiwoye kayak ni nyumba, boma, mji, familia ni kaya, families zinazoongozwa na mkuu wa kaya.

Kayak ni ile nyumba, boma, mji, au makazi, unaweza kuwa na familia moja au zaidi ya moja. Mfano ikiwa ni nyumba ya familia, then inakuwa na a single head of a family ambapo ki Afrika ni baba, Nyumba za Kiarabu na Kihindi, mtoto wa kiume akioa yule mke analetwa hapo, binti akiolewa yule mkwe analetwa hapo. Wakati wa sensa hapa japo ni nyumba moja lakini ndani yake kuna kaya kadhaa. Au kama ni nyumba ya kupangisha, kila mpangaji ni kaya inayojitegemea.

Sensa yetu ni sensa ya watu na makazi, tumeamza na kuhesabu watu, imekamilika jana, leo sensa ya kuhesabu makazi inaanza, hapa kinachohesabiwa sasa ndio hizo nyumba, kayaks, kama ni nyumba moja ina hati moja na familia 20, itahesabika ni nyumba 1. Kama ghorofa lina apartments 20 zenye hati tofauti, zitahesabiwa ni nyumba 20!.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…