Sensa: Kianalogia siku 1, kidigitali siku 7! Could there be something wrong somewhere?! Kesho mwisho! Je, ambao bado hawajafikiwa watahesabiwa?!

Sensa: Kianalogia siku 1, kidigitali siku 7! Could there be something wrong somewhere?! Kesho mwisho! Je, ambao bado hawajafikiwa watahesabiwa?!

Wanabodi,
Makala ya leo ni Swali
Sensa za nyuma tulihesabiwa Ki Analogia na ilichukua Siku 1 tuu, sasa tunahesabiana Kidigitali inachukua Siku 7!, Could There Be Something Wrong Somewhere?!. Leo ni siku ya 6, kuna kaya hazijafikiwa, kesho ni siku ya 7 ambayo ndio ya mwisho, jee kaya zote zilizobakia zitafikiwa?, Je ambazo hawajafikiwa, mpaka kesho, jee watafikiwa, jee watahesabiwa au ikibidi kuongeza siku moja au mbili, tuongeze wote tufikiwe, wote tuhesabiwe?!
View attachment 2336973View attachment 2336974
Paskali
Wee mzee unataka kumchonganisha makinda na rais Samia je unakumbuka jins makinda alivyoendesha bunge ktk wa wabunge wa cdm

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Honestly, kwa nchi kama Tanzania huwezi kufanya sensa kwa siku moja unless kama unakusudia kufanya survey na sio sensa!!

Assume una Makarani 200K wanaotakiwa kuwafikia watu 50M... hapo ina maana kila karani anatakiwa kuwafikia watu 50M/200K = 250

Again, assume unatumia dakika 10 kwa kila mtu... yaani una-include muda wa kutoka sehemu moja hadi nyingine. Hiyo maana yake kila karani atatumia Dakika 2500 kuwafikia hao watu 250.

Dakika 2500 ni sawa na saa 41... NONE STOP ambazo ni almost 4 days for 10 hours per day!!

That being said, kama siku za nyuma sensa zilikuwa zinachukua siku moja, basi tulikuwa tunapigwa manake hata hizo dakika 10 nilizotaja, ni impractical.
Anahesabiwa kila mtu ama mkuu wa kaya na spouse tu?
 
Nafikiri, moja sio kwamba hawakuona kama hizi zoezi linaweza kuwa jepesi sana ikitumika kwa kuanzia ngazi za mabalozi wa nyumba kumi tena lingefanyika kwa ufanisi wa hali ya juu sana kama ulivyosema hapo juu. Ila Nahisi kuna ushindani mle ndani na ndio matokeo yake haya ( mahala kukisha kuwa na ushindani , usitegemee kukawa na ufanisi maana hakuna kusikilizana ) kila mtu ana lake na kupitia hilo lake unakuta kalenga kupata kitu flani. Huenda mbeleni mambo yakawa mambo mazuri, maana kwa sensa hii tumerudi nyuma. Mabalozi wa nyumba kumi ni watu muhimu sana kama wanatumika kwa usahihi na lengo mama toka awali
Nadhani kweli kutakuwa na 10%. Maana kama wangetumia mabalozi hakika data zingekuwa za ukweli maana balozi hawezi danganywa mfano eti smartphone au kuhusu hali ya ndoa au watu waliolala kwenye nyumba husika.
 
Anna Makinda atakujibu.... ingawa waliohesabiwa wanaweza kutumika kutoa takwimu dhahania... makosa yalianza kwenye idadi ya maswali kuwa ya kiutafiti... mtu mmoja anahojiwa dk 40... sio rahisi kuwafikia wote.
Mi nimehisabiwa pamoja na familia yangu, nikamuuliza Mtu wa Sensa Kama kweli umetuhisabu Mimi mpaka Sasa ni no ngapi!? Lakini kashindwa kunitajia no yangu Kama kweli nimehisabiwa!!?? Huu si utapeli!? Mbona Nyumba zetu zote zimehisabiwa na zikapewa no zake kwa kila Mjengo!? Mbona sisi watu hatupewi no zetu Kama kweli tumehisabiwa!!?? Au kuna kitu nyuma ya pazia!? Ni Nani anatafutwa!!??
 
Hii ilishaborongwa tangu kwenye planning, mbaya zaidi hao planning officers hawataki kupokea ushauri wala ushirikiano inapotokea kuna jambo unawasilisha kwao

Ukiwapa ushauri wanasema hujui hiyo kazi ilivyo ngumu, ukimwambia aachie ngazi wafanye wengine hataki! Hata hivyo ni nadra sana mazoezi mengi ya serikali kufanyika kwa ufanisi. Jambo ambalo hulifanya kwa ufanisi ni wakati wa kukomoa.
 
Anahesabiwa kila mtu ama mkuu wa kaya na spouse tu?
Sina familia kwahiyo sijui! Lakini hata kama anahesabiwa Mkuu wa Kaya bado hapawezi kuwa na tofauti kwa sababu atatoa taarifa kuhusu yeye, na pia atatoa taarifa zile zile kuhusu hao wengine, na hizo taarifa zitajazwa independently.
 
Sidhani kama kweli dhamira yao SENSA, maswali ni mengi sana na yasiyo na mlengo wa Sensa ya watu, na ndio maana wanatumia muda mrefu sana kwenye kaya moja,
Baadhi ya maswali yanafikirisha na kukera,
-mimba zilizoharibika!!!! Ngapi!!
-Umewahi kuolewa!!! Mara ngapi!!
Hapo tukajikuta tumeanzisha mjadala mwingine wa yeye kuulizwa badala ya yeye kuuliza.
Wapewe mwezi mzima ndio watawafikia kaya zote kwa hilo zoezi wanalofanya.
😂😂😂
 
Nadhani kweli kutakuwa na 10%. Maana kama wangetumia mabalozi hakika data zingekuwa za ukweli maana balozi hawezi danganywa mfano eti smartphone au kuhusu hali ya ndoa au watu waliolala kwenye nyumba husika.
You can't be serious!! Katika nchi ambayo sifa ya mtu kugombea ubunge ni angalau Darasa la VII ulishawahi kujiuliza elimu za hao mabalozi especially huko vijijini?! Si utalazimika uanze kuwafundisha jinsi ya kuwasha na kuzima tablet kabla ya yote, kisha uhamie jinsi ya kufungua program inayotumika ku-key hizo data!!

Btw, mwenzetu unaishi wapi huko ambako balozi wenu anafahamu smartphones zenu, na idadi ya watu waliolala kwenye kaya husika in one particular day?! Unazungumzia Mabalozi wa Karne ya 21 au wa enzi za Nyerere?!
 
You can't be serious!! Katika nchi ambayo sifa ya mtu kugombea ubunge ni angalau Darasa la VII ulishawahi kujiuliza elimu za hao mabalozi especially huko vijijini?! Si utalazimika uanze kuwafundisha jinsi ya kuwasha na kuzima tablet kabla ya yote, kisha uhamie jinsi ya kufungua program inayotumika ku-key hizo data!!

Btw, mwenzetu unaishi wapi huko ambako balozi wenu anafahamu smartphones zenu, na idadi ya watu waliolala kwenye kaya husika in one particular day?! Unazungumzia Mabalozi wa Karne ya 21 au wa enzi za Nyerere?!
Tumshukuru sana Dkt Kikwete na Mzee Lowasa na shule zao za kata. Kila tarafa ina mhitimu wa form four. Hiki ndiyo kipindi pekee cha kuwatumia hao vijana.
 
Wanabodi,
Makala ya leo ni Swali
Sensa za nyuma tulihesabiwa Ki Analogia na ilichukua Siku 1 tuu, sasa tunahesabiana Kidigitali inachukua Siku 7!, Could There Be Something Wrong Somewhere?!. Leo ni siku ya 6, kuna kaya hazijafikiwa, kesho ni siku ya 7 ambayo ndio ya mwisho, jee kaya zote zilizobakia zitafikiwa?, Je ambazo hawajafikiwa, mpaka kesho, jee watafikiwa, jee watahesabiwa au ikibidi kuongeza siku moja au mbili, tuongeze wote tufikiwe, wote tuhesabiwe?!
View attachment 2336973View attachment 2336974
Leo ni Siku ya Sita ya Zoezi la Sensa, Ambao Hatujahesabiwa, Tutahesabiwa Kweli?.

Ama kweli, mkamia maji, hayanywi!, Waswahili walisema, jambo ukilipania saana, haliwi!, inawezekana hii sense, mimi niliipania sana!. Kwa wiki tatu mfulululizo kabla ya sensa, safu yangu hii ya kwa Maslahi ya Taifa, ilijikita kwenye kuhamasisha zoezi la sensa, sasa siku ya sense yenyewe imefika, mimi siku hesabiwa!, leo ni siku ya 6 ya zoezi la sense, bado sijahesabiwa!, kuuliza kama tutahesabiwa kweli ni genuine concern!.

Kuna ka mtindo kamezuka, ukihoji jambo lolote ambalo wewe kwa mtazamo wako unaona haliendi vizuri au haliendeshwi vema, utanyoonyeshewa kidole kuhusu uzalendo wako!. Hii sensa, hatukuanza nayo leo, tena tumeihamasisha kikamilifu.

Sensa nilianza nayo hapa Sensa: Je, kuna ubaya kuwauliza watanzania their hopes & expectations of their government? Niko tayari kuhesabiwa, wewe je? kisha nikaja hapa Agost 23, tujitokeze kwa wingi kuhesabiwa ili kuiwezesha Serikali kujipanga kimipango mkakati ya SMART, kutuletea maendeleo. halafu hapa Natoa wito Agosti 23 tujitokeze kwa wingi kuhesabiwa na hapa Sensa: Leo ni leo, Kazi ni Moja tu!, Kuhesabiwa! na hapa Shuhudia Sensa Live Kupitia TBC, Nimeshuhudia Live Rais Samia Akihesabiwa. Let's Share Experiences za Sensa na Zoezi la Kuhesabiwa Toka Maeneo Tofauti

Nimeshiriki sensa 4, ya mwaka 1978, ya mwaka 1988, ya mwaka 2002 na ya mwaka 2012, sense ya mwaka huu, 2022, ndio sensa yangu ya kwanza, kutohesabiwa siku ya kwanza ya sensa yenyewe!, na mpaka leo naandika hapa, leo ni siku ya 6 tangu zoezi la sensa lianze na bado kaya yangu, au mtaa wangu, haujafikiwa!.

Siku ya sensa niliianza vizuri kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, Rais wa JMT, amenitumia ujumbe mfupi wa maandishi, SMS kuhusu Sensa!, na nikapandisha bandiko humu Just Imagine Umepokea SMS hii "Mimi Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nakukaribisha ...."- Ungemjibu nini?
"Mimi Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nakukaribisha kushiriki Sensa tarehe 23 Agosti,2022. Nakusihi utoe taarifa sahihi".

Mimi niliupata ujumbe huu, vipi wewe mwenzagu, pia uliupata?. Umejisikiaje kupokea SMS ya Rais wa JMT kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu?.

Nani mwenye kumbukumbu yoyote ya Rais wa JMT kuwahi kutuma SMS yoyote kuhusu jambo lolote at person level "
Mimi Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nakukaribisha..."

Si lengo la makala hii kuingilia kazi ya makarani wa sensa, lakini kwa vile sense zote zilizopita, ulikuwa unahesabiwa siku ya kwanza, hivyo ile siku ya kwanza ya sensa, unakuwa umeipania sana, kila ukisikia mlango kugongwa, siku siku zote ni kumtuma dada kufugua geti, lakini siku hiyo ni baba mwenyewe unakwenda kufungua geti ili uwapokee mwenyewe makarani wa sensa, hivyo kusikia tuu geti linagongwa, lao baba mbio kwenda kufugua geti kukaribisha makarani wa sense!.

Kufika getini na kufungua geti… la haula!, kumbe ni mama wa mboga!, nusu ubamize mlango na kutaka kumfurusha mama wa watu kuwa leo hatununui mboga!, mama wa mboga, anamuulizia dada kama leo tunachukua!, kumbe dada kamsikia na kuja getini, tunachukua, pesa utapitia baadae!, dada wa mboga nae kasema, leo nimepita mapema zaidi, ili nimalize mapema na mimi niende kwangu kusubiri kuhesabiwa, hivyo naomba pesa kabisa, maana leo nikipita nimepita sirudi tena njia hii!. Uzuri wa waleta bidhaa wa nyumbani siku huna wataacha na kesho yake watapitia. Hivyo dada akamwambia tunachukua utapitia kesho!, na siku hiyo ndio baba unashuhudia mboga zikinunuliwa, kisa ni kuwasubiri makarani wa sense!.

Kwa vile sensa zote za nyuma, umezoea kuhesabiwa siku ya kwanza ya sensa, sijui kama ilikuwa ni bahati tuu, lakini kaya nyingine zilikuwa zinahesabiwa kwa siku 7, sijui!, lakini sensa hii leo siku ya 6, nina haki ya kujiuliza kama leo au kesho nitafikiwa kweli?.

Hivyo nikaanza kuwaza mbali!. Tanzania tulipopata uhuru ile miaka ya 60, kuna nchi tulipata nazo uhuru pamoja, zikiwemo nchi zinaitwa Tiger, ikiziangalia zilikuwa na nani ukilinganisha na sisi, tuna nini, nchi hizo zilikuwa hazina kitu, na sisi tulikuwa tuna kila kitu, lakini leo ukiziangalia zilipo na sisi tulipo, lazima utakubaliana na mimi, sisi tuna matatizo mahali!.

Sasa nikilinganisha zile sensa nyingine na hii sensa ya leo, kiukweli kabisa wa dhati ya moyo wangu, kuna tatizo mahali!. Hakuna mtu anaujua mtaa wake kuliko mjumbe wake wa nyumba 10, hakuna mtu anaujua mtaa wake kuliko serikali yake ya mtaa, nyumba yangu ni hatua chache kutoka ofisi ya serikali ya mtaa wangu, haiwezekani leo ni siku ya 6 makarani wa sensa hawanifikia, wakati inawachukua nusu siku tuu kwa watu wa serikali ya mtaa wangu kuwafikia wakazi wote wa mtaa wangu, kwa nini hawa makarani wa sensa hawakuwa ni wajumbe wetu wa nyumba 10 na maofisa wetu wa serikali za mtaa?!.

Kama Tanzania sasa tuna vitambulisho vya taifa, vyenye biometric data, na tuna serikali mtandao, nini faida ya vitambulisho vya taifa vyenye biometric data, na serikali mtandao, kama tunahesabina kijima hivi?!.

Nimemsikia Kamishna wa Sensa kitaifa, Mama Anna Makinda, akisema tungekuwa ni nchi za wenzetu, tungejihesabu na kutuma data, mbona kuna sisi Watanzania wengi tuu tuna simu janja, tuna vitambulisho vya taifa, nchi yetu ina serikali mtandao, si wenye uwezo wa kujihesabu na kutuma data tungetuma, na karani angepita tuu kuhakiki kwa dakika chache, zile sensa za kuhesabiwa ki analojia tumehesabiwa kwa siku moja, leo tunahesabiana kidigitali, tunasubiri siku 6 tuhesabiwe, hapa sio kuna tatizo?!.

Mbona kwenye E Passport tumeweza, E Visa tunaweza, E registrations tumeweza, TRA tunafanya E-Filing, tunashindwa vipi kwenye kitu kidogo kama kujihesabu tuu?.

Pamoja na matatizo yote, kwenye mazuri pia tupongeze, naipongeza Televisheni ya Taifa kutulea matangazo live mubashara ya sensa, tukashuhudia ile siku ya kwanza ya sensa ya viongozi, wakihesabiwa, na mpaka leo wananchi tukihesabiwa. Hongera sana Dr. Rioba na timu yako kwa kazi nzuri.

Kuna uwezekana Dr. Albina Chuwa ame over stay pale NBS, maana sijui huu ni mwaka wa ngapi pale, wenzetu wazungu wana msemo hata uwe mzuri vipi, miaka 10 ni mwisho, na ndio maana hata vipindi vya uongozi mwisho ni miaka 10, wakuu wa taasisi za umma mwisho ni miaka 10, vipi hapo NBS?.

La mwisho, mfumo wa kidigitali unarahisisha sana kazi, tukijenga mifumo imara, hatuhitaji hii duplicity ya Vizazi na Vifo, RITA, Vitambulisho vya Taifa NIDA, Idara ta Takwimu NBS, Immigration, vunja haya makitu yote, centralize all the data katika mfumo mmoja, hata ukusanyaji wa kodi, hakuna tena kushikana mashati!, kila kitu ni streamlined pamoja!.

Nasubiria Kuhesabiwa!.

Wasalaam

Paskali.
B600 kwa siku 7,mkiongeza siku na pesa zinaongezeka. Waaaoooh! Ccm mbele kwa mbele
 
Dodoso lina maswali mengi mno, na miongoni mwa hayo maswali yanaleta maswali zaidi kutoka mlengwa kwenda kwa karani. Muda unaotumia karani kumuhoji mtu mmoja utakuta inachukua zaidi ya hata saa moja.

Hadi inapelekea makarani wanadinyua ama kudinyuliwa
 
Sensa ya nyuma makarani na Wasimamizi 100% walikuwa walimu ambao waliweza kujiongeza mfano unamuona mtu amesimama vizuri amekaa vizuri anasikia anaongea viungo unaona Kuna haja Gani ya kumuuliza ana ulemavu?
Sasa Kuna watu Wana bifu na walimu wanaona wakiwapa kazi watafaidi sana ndio ikawa hivi ilivyo

Naunga mkono hoja, hili zoezi ni muhimu sana lilipaswa lisimamiwe na kada ya ualimu.

Shida tunawaonea nongwa sana walimu, lakin ndiyo kundi linaloweza fanya kazi kwa moyo na uaminifu.

Wangefanya kwa ufanisi mkubwa sana
 
Zoezi la sensa kwa tafsiri zetu wakush ni kama project ilikuwa ya lazima kutoka UNFPA na mama Marekani aliongelea na kuiombea ufadhili lakini kuna harufu ya reverse engineering ya mchwa kutafuna pesa za sensa.

Kuna kaya nyingi mpaka leo hii hazijahesabiwa bado na wengine wanaona kama story fulani za kisiasa.
 
Back
Top Bottom