Sensa na Changamoto ya Intaneti: Karani wa Sensa Akutwa Juu ya Mti akitafuta Mtandao Butiama, Mara

The Palm Beach

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2015
Posts
1,967
Reaction score
4,267
Ni huko wilaya ya Butiama kwa Baba wa taifa hili Mwl J. K. Nyerere.

Kwa jinsi ambavyo viongozi wetu wasivyopenda kukosolewa, si ajabu karani huyu wa sensa anafukuzwa kazi kwa kuposti picha hii na kueleza changamoto hii.

Anaweza kuwa charged kuwa anahujumu zoezi la sensa.

========

Makarani wa sensa wilayani Butiama mkoani Mara wakabiliwa na tatizo la ukosefu wa mtandao wa hatua inayowalazimu kupanda juu ya miti na vilima ili kuweza kupata mawasiliano .

Mwenyekiti wa kamati ya sensa wilayani humo Moses Kaegele ameyasema hayo katika kikao Cha dharura kujadili. Maendeleo ya shughuli hiyo huku akiitaka kamati kusaidiana kutatua tatizo hilo.



Chanzo: RFA Online
 
Huyo tayari lazima, akatwe kichwa kuna amekwenda kinyume na maadili ya kazi!!!hahaaa, yaani wana siasa wao huwa hawapendi kuonyeshwa mapungufu, kwani huwa wanaona ni kama kudharirika, wakati mapungufu ndio yana kuwezesha kuboresha.
 
Hivi ikitokea watu wa sensa wamekuja kwenye nyumba uliyopanga ,alafu mwenye nyumba amekusahau .unatakiwa ufanye Nini?

Mimi nilikuwa ndani nimelala.natoka ananiambia kumbe ulikuwa ndani tumeshahesabiwa.
 
Hivi ikitokea watu wa sensa wamekuja kwenye nyumba uliyopanga ,alafu mwenye nyumba amekusahau .unatakiwa ufanye Nini?.
Mimi nilikuwa ndani nimelala.natoka ananiambia kumbe ulikuwa ndani tumeshahesabiwa.
Subiri Call number itawekwa punde kwa ajili yenu
 
Hiyo milioni wanayolipwa itawatoka puani🤣
 
Huyo tayari lazima , akatwe kichwa kuna amekwenda kinyume na maadili ya kazi!!!hahaaa, yaani wana siasa wao huwa hawapendi kuonyeshwa mapungufu, kwani huwa wanaona ni kama kudharirika, wakati mapungufu ndio yana kuwezesha kuboresha.
Kwa CCM kukosoa au kusema ukweli wao wanaita uchochezi. Hii mijitu ya ovyo sana kuwahi kutokea duniani
 
Itapendeza ukifuatilia jambo hili kwa karibu.
Huyo mfanyakazi akifukuzwa kazi sote tupate taarifa hiyo muhimu.
 
Harafu Jana usiku wale jamaa wa Takwimu wanasema hakuna mahali ambapo karani anahitaji mtandao..

Sasa sijui walikuwa wanamdanganya nani na Kwa maslahi ya nani? Ujue watu wanaojiita wasomo huwa ni wapumbavu Sana mara nyingi huwa wanaamini Wana akili sana na wasioenda shule hawana akili wakati mambo ya IQ Wala hayahitaji shule za madarasani.
 
Mwalimu Mwalimu Mwalimu, Yes teacher mchonga kwa nini uliyaruhusu haya (Iliimba kwaya moja ya Rwanda), Butiama ilitakiwa kuwa kwa sasa zaidi ya Pretoria, yani Butiama ya kukosa mtandao karne hii ya 21, basi uliowaachia ukitegemea uzalendo utashika nafasi yake ili panyanyuke pamebakia vile vile ndio had leo hakuna mtandao [emoji848]
 
Nimekuelewa sana bwashee
 
Hivi ikitokea watu wa sensa wamekuja kwenye nyumba uliyopanga ,alafu mwenye nyumba amekusahau .unatakiwa ufanye Nini?

Mimi nilikuwa ndani nimelala.natoka ananiambia kumbe ulikuwa ndani tumeshahesabiwa.
Siyo jukumu la mwenye nyumba kuhangaika na wajingawajinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…