Sensa ya watu na makazi: Maswali ambayo hayakupaswa kuwepo kwenye dodoso

Una pasi feni au brenda? Sasa inasaidia nini kwenye takwimu za nchi
Tunataka kujua kama unatumia umeme ama lah! Hata hivyo, Mimi Nina blends ya Mkono navuta uzi tu chungwa ama pasheni inachakatwa. Situmii umeme. Ama natumia pasi ya magunzi ya mahindi. Sasa wakisema natumia umeme kwa kutaja Nina pasi ama blends watanionea.
 
Sasa toa solution ulitaka maswali gani yaulizwe ili Sensa iwe standard?
 
Kwenye SENSA hakuna swali la PASI ya Umeme ama Mkaa... labda vifaa vya TEHAMA.... Computer, Tablets ...

Aliniacha Hoi qliponiuliza, jee una pasi ya umeme? Nikamjibu ndio. Jee na ya mkaa? Nikakumbuka ninayo ila sijui kule store imewekwa eneo gani maana mara ya mwisho kuitumia ni wakati wa mgao mkali wa umeme 2009 Rais akiwa Kikwete.
Michosho mitupu!
 
Asante, maelezo ya namna hii ni muhimu ili kupanua uwelewa wetu kwenye mambo ya sensa
 
Karani wangu katishia Nina simu ama la!! Lakini ninavyoitumia hatukufika huko.
Jiandae kulipi tozo za games.... Huko app store na play store apps zinaweza zikawekewa tozo maana mnaonekana mnacheza sana games, hamfanyi kazi.
 
Siku ya pili sasa hata kalani kwangu simuoni ,KWa karibu tumepigwa na pesa imeenda
 
Kwenye SENSA hakuna swali la PASI ya Umeme ama Mkaa... labda vifaa vya TEHAMA.... Computer, Tablets ...
Huo ubishi sasa! Au alikuona hujanyoosha nguo zako akaona akaona abonyeze tuu jibu la "hakuna"?
 
Hata usipofuatilia cheti cha kifo taarifa zinapaswa kuwepo serikalini. Kama kifo kimetokeya nyumbani taarifa hupelekwa serikali ya mtaa.
 
Hayo maswali yote yapo kwenye dodoso la sensa
 
Usipochukuwa cheti cha kifo serikali haiwezi kuwa na takwimu za waliokufa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…