Sensa ya watu na makazi: Maswali ambayo hayakupaswa kuwepo kwenye dodoso

Sensa ya watu na makazi: Maswali ambayo hayakupaswa kuwepo kwenye dodoso

Una pasi feni au brenda? Sasa inasaidia nini kwenye takwimu za nchi
Tunataka kujua kama unatumia umeme ama lah! Hata hivyo, Mimi Nina blends ya Mkono navuta uzi tu chungwa ama pasheni inachakatwa. Situmii umeme. Ama natumia pasi ya magunzi ya mahindi. Sasa wakisema natumia umeme kwa kutaja Nina pasi ama blends watanionea.
 
Hii ni sensa ya watu na makazi, lengo kuu la sensa ni kupanga maendeleo ya muda mrefu. Unapoingiza siasa kwenye dodoso utaishia kupata data ambazo ni useless ndani ya mwaka tuu.

Pia kuna data zingine ambazo tayari serikali na vyombo vyake wanazo, sikuona haja ya kuwepo kwenye dodoso, ni kuwachosha makarani tuu na kuifanya kazi ya sensa kuwa ngumu sana na inayoboa kwa anayehojiwa.

Moja ya maswali ambayo ni useless kwenye dodoso la mwaka huu ni kama yafuatayo:

1. Namba ya simu
Kila siku watu wanabadili namba, baada ya mwaka tuu nusu ya data hizi huenda ziwe useless.

2. Mahali unaposhinda
Mahali mtu anaposhinda inasaidia nini kwenye maendeleo ya taifa? Hizi data ndani ya mwaka tuu zitakuwa obsolete maana asilimia kubwa hawatakuwa wanashinda pale pa mwanzo.

3. Kitambulisho na namba ya NIDA
Hizi data tayari zipo NBS. Kuziuliza tena kwenye dodoso ni kuwachosha makarani tuu.

4. Kitambulisho cha ujasiriamali.
Huu mradi ulishasitishwa siku nyingi. Unawekwa kwenye dodoso kwa lengo gani wakati toka mwendazake aondoke na wenyewe ukasitishwa na hivi vitambulisho havitambuliki tena?

5. Simu janja na Kompyuta
Hizi data zote ziko pale TCRA, wao ndiyo wanajua exactly namba ya hivi vifaa vilivyopo hewani. Kwa vyovyote vile data watakazopata makarani hazitaendana na za TCRA maana siyo wote watatoa data kamili, kwa maswali yalivyo mengi watu wataamua kufupisha kwa kujibu "HAPANA SINA".

6. Uzazi na vifo.
Hizi data zinatumwa kila mwezi kwenye wizara zinazohusika. Kuziuliza tena kwenye dodoso ni kuwachosha makarani tuu.

7. Anuani ya makazi
Hili zoezi limefanyika juzi tuu. Kwa kuwa visimbuzi vinatumia GPS nilitegemea kila kikifika kwenye kaya husika basi automatically kidetect kama nyumba ina anuani ya makazi ama laah.


Ongezeeni mengineyo.....
Sasa toa solution ulitaka maswali gani yaulizwe ili Sensa iwe standard?
 
Kwenye SENSA hakuna swali la PASI ya Umeme ama Mkaa... labda vifaa vya TEHAMA.... Computer, Tablets ...

Aliniacha Hoi qliponiuliza, jee una pasi ya umeme? Nikamjibu ndio. Jee na ya mkaa? Nikakumbuka ninayo ila sijui kule store imewekwa eneo gani maana mara ya mwisho kuitumia ni wakati wa mgao mkali wa umeme 2009 Rais akiwa Kikwete.
Michosho mitupu!
 
Sensa ya watu na makazi? Ikimaanisha hao watu hawaishi kisiwani wanatumia simu, wanafuga mbuzi, Wanamiliki biashara n.k so ukishajua hayo "mambo mengine" ni rahisi kuandaa sera nzuri za kuwasaidia hao watu.

Mfano kama kwenye mahojiano ukagundua 70% hawana simu, Ina maana Serikali itashusha Kodi Ili simu ziuzwe Bei chini n.k sasa utasemaje hayo "mambo mengine" hayana maana
Asante, maelezo ya namna hii ni muhimu ili kupanua uwelewa wetu kwenye mambo ya sensa
 
Karani wangu katishia Nina simu ama la!! Lakini ninavyoitumia hatukufika huko.
Jiandae kulipi tozo za games.... Huko app store na play store apps zinaweza zikawekewa tozo maana mnaonekana mnacheza sana games, hamfanyi kazi.
 
KWa mfumo wa nchi yetu ,ilikua simple Sana, kutumia balozi wa nyumba kumi ,sambaza dodoso, zikajazwa na kuzipeleka KWa mkuu wa mtaa,then mtendaji wa kata, nazikatumwa panapo husika, all in all nakua na Tim ndogo KILA wilya KWa makundi mahalum, basi kuliko tumia pesa nyingi alafu ukaishia kuwa na data feki, tatizo ni Kwamba serikalin watu hujifanya wanajua KILA kitu , kumbe wapo kiupigaji tu
Siku ya pili sasa hata kalani kwangu simuoni ,KWa karibu tumepigwa na pesa imeenda
 
Kwenye SENSA hakuna swali la PASI ya Umeme ama Mkaa... labda vifaa vya TEHAMA.... Computer, Tablets ...
Huo ubishi sasa! Au alikuona hujanyoosha nguo zako akaona akaona abonyeze tuu jibu la "hakuna"?
 
Unaposema data za NIDA teyari zipo NBS..hao NBS watajuaje walio hai na waliokufa kwa usahihi bila kupta takwimu za sensa?

Ikumbukwe ni idadi kubwa ya watu wanaokufa bila kufuata certificate za vifo kutoprocess certificate ya kifo kunaikosesha serikali takwimu sahihi za vifo...

Ukiona familia inafuatilia cheti cha kifo kwa sehemu kubwa huwaga ni kwaajiri ya matumizi ya kisheria kwenye masuala ya mirathi ya Mali za marehemu ila wengi ambao hawanaga shuguli maalumu na hawana mali za kulithiwa huwaga ndugu zao hawasumbuki kufuatilia vyeti vya vifo pale RITA...
Hata usipofuatilia cheti cha kifo taarifa zinapaswa kuwepo serikalini. Kama kifo kimetokeya nyumbani taarifa hupelekwa serikali ya mtaa.
 
Kwakweli hukuninako ishi Mimi kigoma hapa mjini kunasehemu kunaitwa kwa padri nijirani nakambi yajeshi nilitegemea kuulizwa VP mnatumia barabara gani kufata huduma ndio changamoto kwetu watoto wanasoma kufata shule umbali gani huduma yasoko mnapata wapi unawatoto walisoma diploma au digee wanakazi au hawana kazi ningesifu kwakusema sensa hii imekuja kuboresha maisha lakini unakuta unaulizwa hali yandoa unasikia eti nyumbayako inavyumba vingapi na mengine sikuyapenda kabisa tuwe siriasi tuulizwe changamoto muhimu nchi tuache porojo kerokubwa ni ajira namiundombinu ambayo hayaulizwi ndiomuhimu
Hayo maswali yote yapo kwenye dodoso la sensa
 
Unaposema data za NIDA teyari zipo NBS..hao NBS watajuaje walio hai na waliokufa kwa usahihi bila kupta takwimu za sensa?

Ikumbukwe ni idadi kubwa ya watu wanaokufa bila kufuata certificate za vifo kutoprocess certificate ya kifo kunaikosesha serikali takwimu sahihi za vifo...

Ukiona familia inafuatilia cheti cha kifo kwa sehemu kubwa huwaga ni kwaajiri ya matumizi ya kisheria kwenye masuala ya mirathi ya Mali za marehemu ila wengi ambao hawanaga shuguli maalumu na hawana mali za kulithiwa huwaga ndugu zao hawasumbuki kufuatilia vyeti vya vifo pale RITA...
Usipochukuwa cheti cha kifo serikali haiwezi kuwa na takwimu za waliokufa?
 
Back
Top Bottom