Sera mpya ya Elimu, nahisi inatatua matatizo binafsi ya Waziri

Vitu 2 tu vimenivutia.
1. Kufuta mitihani. Elimu ya mitihani siioendi kapisa. Mitihani inaua kabisa dhana ya kusoma, inaweka dhana ya mashindano.

2. Kupunguza miaka ya shule. Hakuna sababu ya kusoma miaka 7.

3. Tatizo ambalo sijasikia wakilitajia suluhisho ambalo ndio tatizo kuu la mfumo wetu wa elimu ni je mfumo ama mtaala mpya utawapa wanafunzi ujuzi wa kutosha wa kukabiliana na maisha ama tutaendelea kukaririsha watoto?
Kwamba mtihani Hauna maana zaidi ya ushindani, na ni nani kasema ushindani ni mmbaya au kosa. Tunapenda kukariri misemo na mawazo ya watu bila tafakuri. Sijui umewahi kupata muda wa kufikiri elimu, au kusoma bila kipimo Cha mitihani?. Ni nchi Gani duniani wanasoma bila kipimo Cha mitihani, vpi ukienda shule au chuo ambacho Hakina mitihani?
 
Wewe akili huna.

Huelewi hata mantiki ya elimu ni nini.

Kwa kukusaidia, elimu mantiki yake ni kumpa mtu ufahamu na uelewa na ujuzi wa kukabiliana na mazingira yanayozunguka.

Sasa kujifunza namna ya kukabiliana na mazingira yanayolizunguka unahitaji kushindanishwa na mtu tena? Unashindanishwa ili iweje?

Elimu sio mashindano. Hushindani na mtu bali unatakiwa uwe na uwezo wa kukabiliana na mazingira na changamoto zinazokuzunguka.

Rudi shule uongeze ufahamu ndio uje hapa tujadiliane. Shida yako ni shule ndogo.
 
Vitu 2 tu vimenivutia.
1. Kufuta mitihani. Elimu ya mitihani siioendi kapisa. Mitihani inaua kabisa dhana ya kusoma, inaweka dhana ya mashindano.

2. Kupunguza miaka ya shule. Hakuna sababu ya kusoma miaka 7.

3. Tatizo ambalo sijasikia wakilitajia suluhisho ambalo ndio tatizo kuu la mfumo wetu wa elimu ni je mfumo ama mtaala mpya utawapa wanafunzi ujuzi wa kutosha wa kukabiliana na maisha ama tutaendelea kukaririsha watoto?
Hatujafikia kiwango cha kufuta mitihani na kujisifu. Ni upuuzi mwingine ktk elimu yetu. Lengo ni nini? Muhimu kabisa tunahitaji elimu. Elimu haipatikani kwa kusukuma wanafunzi mbele bila sababu.

Ningefurahi kama wangefuata mfumo wa Singapore. Kijana asome na kupewa mtihani hadi aelewe kwa kiwango fulani, bila kujali idadi ya miaka aliyotumia shuleni. Fast learner watumie hiyo miaka 7, lakini slow learners watumie hata miaka 10!
 
Nimeambiwa kuna jambo limejificha. Sera imeweka mifumo miwili, kwamba kuna wanafunzi hawataruhusiwa kuendelea na elimu ya sekondari, watapelekwa vyuo vya ufundi baada ya darasa la 6. Guess what? Watoto wa wenye uwezo watapelekwa private schools! Mwanakijiji ndo ataambiwa wewe ni wa ufundi tu. akawe seremala!

Hii wizara ni feki tu!
 
Nchi yetu imefikia hatua sera ya nchi inaweza kutungwa ili kutatua matatizo ya familia ya waziri. Inasadikiwa Mungai alikuwa na watoto walioshindwa Sayansi ya sekondari, akaamua kuyaunganisha masomo.

Bodi ya mikopo ya elimu ya juu ilipigwa shinikizo kwa mwaka mmoja kuwapa mikopo wanafunzi wasome digrii za masters ili watoto wa waziri wapate nafasi.

Baada ya mwaka mmoja wakasema hapana! Bodi hiyo hiyo iliyolenga watoto wasio na uwezo vyuo vya serikali, ikasema sasa ni walioshinda sayansi, kiongozi mmoja akaona watoto wake wameachwa nje akasema hapana! Wote ni watanzania wapewe mikopo bila kujali ni University ya serikali au hapana.

Sasa Waziri huyu kaja na sera mpya. Ukiiangalia utadhani kuna kitu, lakini inakuja kuwabagua watoto wa maskini na matajili watakaosoma private school.

Miaka 6 sawa lakini hawasemi 7 iliharibu nini? Umri wa kuanza umeshushwa na sera lakini hawasemi akianza na miaka 7 kuna shida gani na kwa nini ilikuwa 7?

Watoto wa waziri watasoma private je, watoto wa mwanakijiji kule chini atapata wapi sekondari ya kubeba watoto wote walioko primary? Sasa hivi kuna sekondari ambazo kwa miaka 20 hazijawahi kupata mwalimu wa hisabati! Yaani sera irekebishe ubora wa elimu kizembe kiasi hiki?

Nasikitika kuona kwamba waziri wa elimu ni profesa. Au ni wale wanaoamini anajua sana kiasi kwamba wengine hawamuelewi? Kichwa cha mwendawazimu.

matukio yote uliyosema hapa yoote make sense kwa mtu yeyote yule ambae ataamua kukaa chini kwa dakika tano tu kuangalia namna na wakati maamuzi haya yalipotokea. Naamini wapo watanzania tele wanaolilalamikia hili na mfum mzima wa elimu ya ndugu zetu masikini hasa vijijini. Wote tunajua sababu kuu ya elimu duni ni ccm na uongozi wake lakini subiri hadi uchaguzi uone wale wale wanaolalamika kwa elimu duni, huduma mbaya za afya na mengine mengi wakishangilia wagombea wa ccm na kuwapa kura zao. Bila ya mabadiliko ya chama tawala nchi japo kwa muhula mmoja Tanzania haitaweza kubadilika na mfumo wa kujinufaisha binafsi kwanza.
 
Hatujafikia kiwango cha kufuta mitihani na kujisifu. Ni upuuzi mwingine ktk elimu yetu. Lengo ni nini? Muhimu kabisa tunahitaji elimu. Elimu haipatikani kwa kusukuma wanafunzi mbele bila sababu.

Ningefurahi kama wangefuata mfumo wa Singapore. Kijana asome na kupewa mtihani hadi aelewe kwa kiwango fulani, bila kujali idadi ya miaka aliyotumia shuleni. Fast learner watumie hiyo miaka 7, lakini slow learners watumie hata miaka 10!
Mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi Hauna maana yoyote,elimu ya sekondari iwe elimu ya lazima kwa kila mtanzania,wajinga wengi Sana kwenye jamii
 
Nimeambiwa kuna jambo limejificha. Sera imeweka mifumo miwili, kwamba kuna wanafunzi hawataruhusiwa kuendelea na elimu ya sekondari, watapelekwa vyuo vya ufundi baada ya darasa la 6. Guess what? Watoto wa wenye uwezo watapelekwa private schools! Mwanakijiji ndo ataambiwa wewe ni wa ufundi tu. akawe seremala!

Hii wizara ni feki tu!
Hizo ni hisia zako tuu.
Ingekuwa hivyo hata sasa watoto wa masikini wasingekuwepo Vyuo Vikuu.
Watoto wa masikini wasingepata mikopo.

Tanzania haina Ubaguzi kiasi hicho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hisia zako ni zipi? Huijui nchi yako na matatizo yake. Umefika MUHAS na kufahamu profile ya vijana wanaosoma udaktari wametoka shule zipi na familia zipi? Mengine hayahitaji utafiti, tumia tu uwezo wa maumbile ya kibinadamu. Angalia waliochaguliwa na shule walizotoka, uieleze JF ni wangapi wametoka shule za serikali, za kata.
 
Mimi nimesoma hapa Tanzania, kuanzia Primary mpaka Chuo kikuu.
Kote nilikopita nimekutana na watoto wa hali ya chini kibao. Wanasoma shule hizo na wengi waliofaulu vizuri walipata nafasi Vyuo vikuu na mkopo juu.
Hao wanakosa nafasi Muhas, ni kwasababu ufaulu wao uko chini.
Chuo hakiwezi kumdahili mwanafunzi kwa kigezo kwamba ni mtoto wa masikini.
Na kwangu mimi huo sio Ubaguzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe akili huna.

Huelewi hata mantiki ya elimu ni nini.

Kwa kukusaidia, elimu mantiki yake ni kumpa mtu ufahamu na uelewa na ujuzi wa kukabiliana na mazingira yanayozunguka.

Sasa kujifunza namna ya kukabiliana na mazingira yanayolizunguka unahitaji kushindanishwa na mtu tena? Unashindanishwa ili iweje?

Elimu sio mashindano. Hushindani na mtu bali unatakiwa uwe na uwezo wa kukabiliana na mazingira na changamoto zinazokuzunguka.

Rudi shule uongeze ufahamu ndio uje hapa tujadiliane. Shida yako ni shule ndogo.
Hapo ulipojipambanua kuwa wewe unaelewa zaidi yangu tayari umeingiza ushindani. Nadhani una turudisha kwenye elimu ya mababu kabla ya ukoloni, (informal education)lakini elimu ya Darasani yenye kufuata mitaala na mfumo wa kukaa darasani haiwezi kukosa mtihani hakuna wanapotoa vyeti bila mitihani. Mitihani inasaidia kupima uelewa na kusaidia kutoa viwango vya ufaulu. Mtihani utakuwepo kidato Cha nne na kuendelea hivyo sera haijafuta mitihani, wewe mwenye uelewa maisha ni ushindani, kama unajitoa kwenye ushindani jua ni dhaifu na mbumbumbu. Acha kukariri misemo ya watu tumia akili vizuri kutafakari. Wewe ulipoenda shule hakuna aliyekwambia umekuja kushindana Bali kusoma, kama ulishindana ulijichochea mwenyewe. Being a evil genius itself sounds a bit fishy.
 
Naona hueleweki. Ndo maana nimesema huijui nchi yako.
 
Nikuulize swali mtaamu, mtoto wa miaka 10 hadi 12 ameshindwa mtihani unamwambia ni failure, kwamba hajui chochote wewe unaona hiyo ina mantiki?

Mtoto bado mdogo, bado anajifunza, bado akili yake ina explore mazingira na kujifunza halafu unamwambia ni failure kitaifa eti kisa kakosa swali la hesabu, hiyo ni akili ama mavi? Yaani how comes a 10 years old kid awe ni failure?

Halafu kwa nini uniambie mimi ni failure tu kisa nimeshindwa swali la hesabu, kwani hakuna vitu vingine ambavyo najua na hukuniuliza?

Finland ndio case study ya Dunia kwa sasa kwa kuondoa huu uhayawani na watoto wao ni best kwenye kila kitu, sciences, mathematics, IT, reasoning, thinking etc. Sasa na mamitihani yako wewe una watoto wana akili kuliko wa Finland?

Hata Chama cha Labor cha UK wamesema wakishinda uchaguzi wanaondoa mitihani yote. Wasikilize hapa.
 
Wewe akili huna.

Huelewi hata mantiki ya elimu ni nini.

Kwa kukusaidia, elimu mantiki yake ni kumpa mtu ufahamu na uelewa na ujuzi wa kukabiliana na mazingira yanayozunguka.

Sasa kujifunza namna ya kukabiliana na mazingira yanayolizunguka unahitaji kushindanishwa na mtu tena? Unashindanishwa ili iweje?

Elimu sio mashindano. Hushindani na mtu bali unatakiwa uwe na uwezo wa kukabiliana na mazingira na changamoto zinazokuzunguka.

Rudi shule uongeze ufahamu ndio uje hapa tujadiliane. Shida yako ni shule ndogo.
Mitihani haina dhana ya kushindanisha, bali wanafunzi wenyewe wanaijenga dhana ya kushindana kwenye mitihani!

Dhana ya mtihani Ni upimaji wa kutathmini Ni kwa kiwango gani anaejifunza amejenga ufahamu, uwezo na uelewa!

Hata nyumbani ukishamwelekeza mtoto jambo lolote utahitaji ujue ameelewa kwa kiwango gani,

Kama mitihani hii haikidhi uwezo wa kutoa tathmini, maana yake ni lazima kuweka namna nyingine ya kutathmini!

Namna yoyote ya kutathmini uelewa na uwezo wa wanaopewa mafunzo, bado itaitwa Ni mtihani
 
Nikuulize swali mtaamu, mtoto wa miaka 10 hadi 12 ameshindwa mtihani unamwambia ni failure, kwamba hajui chochote wewe unaona hiyo ina mantiki?

Mtoto bado mdogo, bado anajifunza, bado akili yake ina explore mazingira na kujifunza halafu unamwambia ni failure kitaifa eti kisa kakosa swali la hesabu, hiyo ni akili ama mavi? Yaani how comes a 10 years old kid awe ni failure?

Halafu kwa nini uniambie mimi ni failure tu kisa nimeshindwa swali la hesabu, kwani hakuna vitu vingine ambavyo najua na hukuniuliza?

Finland ndio case study ya Dunia kwa sasa kwa kuondoa huu uhayawani na watoto wao ni best kwenye kila kitu, sciences, mathematics, IT, reasoning, thinking etc. Sasa na mamitihani yako wewe una watoto wana akili kuliko wa Finland?

Hata Chama cha Labor cha UK wamesema wakishinda uchaguzi wanaondoa mitihani yote. Wasikilize hapa.

Na umekaa hapo unaamini mitahani ikifutwa kwa level hiyo ndo tukuwa kama wafinland (finnish)? Labda ugomvi wako mkubwa ni Nini na mtihani? Elimu yetu Bado ni very theoretical ., Acha chama Cha labour na wa-finnish wafute mitihani wanozo nyenzo na zana za kufanya hivo wana elimu iliyojikita kwenye vitendo, unisaidie unaenda kumpima vipi mtu aliyeelewa alichofundishwa kama huwezi kwa vitendo?, Hata South Korea wameendelea lakini Bado ndo nchi yenye mitihani migumu Zaidi. Hata elimu ya zamani ya ujuzi wa kurithi Toka kwa mzazi, ulikuwa ukifundishwa lazima uoneshe kwa kupimwa kuwa umefuzu.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Don't imitate much as we admire the successful! Finland is no example to our education system. Tukiendelea kusema Finland, Singapore, etc., ni kama kusema hatujitambui. Hakuna mtoto wa Finland asiyejua kusoma na kuandika. Hata taahira anatafutiwa mbinu za kuongeza uelewa wake. Hapa kwetu hata mwalimu anafundisha asichokijua.
Hahahahaaaaaa ! Mwalimu anafundisha asichokijua . Tatizo la msingi ni lugha ya kufundishia ichaguliwe moja ama kiswahili ama kiingereza kuanzia chekechea hadi Chuo Kikuu vinginevyo hata ufanye mabadiliko gani ni kazi bure, Profesa unafeli wapi?
 
Na umekaa hapo unaamini mitahani ikifutwa kwa level hiyo ndo tukuwa kama wafinland (finnish)? Labda ugomvi wako mkubwa ni Nini na mtihani? Elimu yetu Bado ni very theoretical ., Acha chama Cha labour na wa-finnish wafute mitihani wanozo nyenzo na zana za kufanya hivo wana elimu iliyojikita kwenye vitendo, unisaidie unaenda kumpima vipi mtu aliyeelewa alichofundishwa kama huwezi kwa vitendo?, Hata South Korea wameendelea lakini Bado ndo nchi yenye mitihani migumu Zaidi. Hata elimu ya zamani ya ujuzi wa kurithi Toka kwa mzazi, ulikuwa ukifundishwa lazima uoneshe kwa kupimwa kuwa umefuzu.
Mitihani inafutwa sio kwa sababu ya kutaka kufanana na Finland.

Nimekuuliza swali hujajibu, mtoto wa miaka kumi unaweza kumuita failure kisa amekosa swali la hesabu?

Najaribu kukuuliza maswali yenye simple logic angalau na wewe ufikiri ila naona hakuna kitu.
 
Hahahahaaaaaa ! Mwalimu anafundisha asichokijua . Tatizo la msingi ni lugha ya kufundishia ichaguliwe moja ama kiswahili ama kiingereza kuanzia chekechea hadi Chuo Kikuu vinginevyo hata ufanye mabadiliko gani ni kazi bure, Profesa unafeli wapi?
Ni kweli, kuna baadhi ya vitu walimu hufundishwa bila kuvijua.
Unakuta mwalimu wa Baiolojia anafundisha malaria huenezwa katika jamii na mbu aina ya anofelesi. Sasa mwekee mbu wa aina tofauti afu mtake amtofautishe huyo anofelesi kutoka katika hilo kundi utaujua uhalisia wa mfumo wa elimu yetu!
 
Mitihani inafutwa sio kwa sababu ya kutaka kufanana na Finland.

Nimekuuliza swali hujajibu, mtoto wa miaka kumi unaweza kumuita failure kisa amekosa swali la hesabu?

Najaribu kukuuliza maswali yenye simple logic angalau na wewe ufikiri ila naona hakuna kitu.
Nakujibu NDIYO ni failure kabisa kama wenzake wamepata mia,tisini, themanini, sabini, sitini na yeye akaishia kupata kumi yeye ni kweli amefeli. Mtoto mdogo siyo failure wa maisha lakini kwenye kusoma ni failure. Nimejibu lakini si kama unavyotaka wewe. Nipe umri wa mtoto kuanza kufeli masomo.

Kama hutaki mitihani basi hata mazoezi ya Darasani hayafai, kwasababu vyote ni vipimo isipokuwa mtihani ni kipimo kikubwa baada muda Fulani wa mafunzo. Profesa panua uelewa wako, acha kung'anga'ana na hoja za umri wa failure.
 
Mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi Hauna maana yoyote,elimu ya sekondari iwe elimu ya lazima kwa kila mtanzania,wajinga wengi Sana kwenye jamii
Wajinga hawataisha, hata tukiifanya Elimu ya chuo kikuu kuwa ya lazima.
Sera hii ndiyo inaenda kutengeneza wajinga wengi. Tusubiri tuone.
 
Back
Top Bottom