Sera mpya ya Elimu, nahisi inatatua matatizo binafsi ya Waziri

Sera mpya ya Elimu, nahisi inatatua matatizo binafsi ya Waziri

Vitu 2 tu vimenivutia.
1. Kufuta mitihani. Elimu ya mitihani siioendi kapisa. Mitihani inaua kabisa dhana ya kusoma, inaweka dhana ya mashindano.

2. Kupunguza miaka ya shule. Hakuna sababu ya kusoma miaka 7.

3. Tatizo ambalo sijasikia wakilitajia suluhisho ambalo ndio tatizo kuu la mfumo wetu wa elimu ni je mfumo ama mtaala mpya utawapa wanafunzi ujuzi wa kutosha wa kukabiliana na maisha ama tutaendelea kukaririsha watoto?
Tayari tuko kwenye competence based curriculum ndg, katazame mitihani ya darasa la saba 2020-2022, utaona ukweli huo. Mfano kwenye hesabu hutokuja ukuta zile hesabu za wazi mfano; 100-3=n.k. Maswali yamejikita kwenye kupima uelewa wa mambo na siyo kukariri.
 
Nchi yetu imefikia hatua sera ya nchi inaweza kutungwa ili kutatua matatizo ya familia ya waziri. Inasadikiwa Mungai alikuwa na watoto walioshindwa Sayansi ya sekondari, akaamua kuyaunganisha masomo.

Bodi ya mikopo ya elimu ya juu ilipigwa shinikizo kwa mwaka mmoja kuwapa mikopo wanafunzi wasome digrii za masters ili watoto wa waziri wapate nafasi.

Baada ya mwaka mmoja wakasema hapana! Bodi hiyo hiyo iliyolenga watoto wasio na uwezo vyuo vya serikali, ikasema sasa ni walioshinda sayansi, kiongozi mmoja akaona watoto wake wameachwa nje akasema hapana! Wote ni watanzania wapewe mikopo bila kujali ni University ya serikali au hapana.

Sasa Waziri huyu kaja na sera mpya. Ukiiangalia utadhani kuna kitu, lakini inakuja kuwabagua watoto wa maskini na matajili watakaosoma private school.

Miaka 6 sawa lakini hawasemi 7 iliharibu nini? Umri wa kuanza umeshushwa na sera lakini hawasemi akianza na miaka 7 kuna shida gani na kwa nini ilikuwa 7?

Watoto wa waziri watasoma private je, watoto wa mwanakijiji kule chini atapata wapi sekondari ya kubeba watoto wote walioko primary? Sasa hivi kuna sekondari ambazo kwa miaka 20 hazijawahi kupata mwalimu wa hisabati! Yaani sera irekebishe ubora wa elimu kizembe kiasi hiki?

Nasikitika kuona kwamba waziri wa elimu ni profesa. Au ni wale wanaoamini anajua sana kiasi kwamba wengine hawamuelewi? Kichwa cha mwendawazimu.
Waziri wa sasa nadhani hakuanzisha hili bali yule aliyepita...Pengine anajaribu kuiwrka vizuri zaidi, ebu tusubiri tuone
 
Walau kila mtu afike sekondari kami ilivyokua kila mtu kufika la saba
Sera haina shida, kinachotakiwa ni utashi wa kisiasa kutimiza malengo hayo. Mfumo tunaoenda nao unamkalisha sana mwanafunzi masomoni na umri wa kuishi ushapungua, ko lazima watu watoke masomoni mapema watumikie Taifa lao wakiwa na nguvu
 
Nimekuuliza swali hujajibu, mtoto wa miaka kumi unaweza kumuita failure kisa amekosa swali la hesabu?

Kama hajui kusoma na kuandika ktk umri huo basi yeye ni failure. Kuna Wanafunzi wanafika darasa la Saba hawajui kusoma na kuandika, hao ni failure. Lakini sera itasema wasonge mbele kwenda sekondari .
 
Don't imitate much as we admire the successful! Finland is no example to our education system. Tukiendelea kusema Finland, Singapore, etc., ni kama kusema hatujitambui. Hakuna mtoto wa Finland asiyejua kusoma na kuandika. Hata taahira anatafutiwa mbinu za kuongeza uelewa wake. Hapa kwetu hata mwalimu anafundisha asichokijua.
Acha kumdhalilisha walimu wewe, wanafundisha wasuchokijua ukimaanisha nini? Au unaanini walimu wa kizungu ndo Bora kuliko wa bongo?
 
Kama hajui kusoma na kuandika ktk umri huo basi yeye ni failure. Kuna Wanafunzi wanafika darasa la Saba hawajui kusoma na kuandika, hao ni failure. Lakini sera itasema wasonge mbele kwenda sekondari .
Mi naona bora hata iishie darasa la nne, then sekondari iwe darasa la 5-9, maana ukweli ulivyo lengo la sekondari ni kufundishia lugha ya Kiingereza. Shida inakuja mtu anaanza kidato Cha kwanza akiwa na miaka 15, wakati kisaikolojia muda wa mwisho mtu kujifunza lugha ni miaka 16. Ndo maana wengi hukariri na siyo kuwa na ubobezi wa lugha hiyo. Kwa darasa la awali hadi la nne naamini mtoto atakuwa amekijua Kiswahili ambacho pia ni lugha ya pili hapa nchini hasa maeneo ya vijijini.
 
Julius malema aliwahi kusema akichaguliwa kuwa Rais sio tu atafanya elimu kuwa bure lakn ni lazima kwa wanafunz wote kusoma shule za elimu bure. Ili kama hamtaboresha ufundishaji na watoto wa vigogo nao wafeli
 
Hii point kwako umeichukuliaje. Mitihani itakuwepo Ile ya darasani si inatosha sema lazima mtt awe anafikisha wastani kadhaa ili apande class
Kinachotakiwa ni uwekezaji wa kutosha ktk kuajiri walimu wa kutosha pamoja na kujari maslahi Yao, miundombinu ya kutosha na zana toshelezi. Hapo kila kitu kitaenda vizuri. Ilu kuendeleza ni lazma serikali iwekeze kwa dhati katika sekta kuu mbili; afya na elimu. Mengine yatajiset yenyewe ukiwezea hayo mawili makuu
 
Julius malema aliwahi kusema akichaguliwa kuwa Rais sio tu atafanya elimu kuwa bure lakn ni lazima kwa wanafunz wote kusoma shule za elimu bure. Ili kama hamtaboresha ufundishaji na watoto wa vigogo nao wafeli
Hilo haliwezekani ktk mfumo wa kibepari, utakuwa umeturudisha kwenye ujamaa jambo ambalo haliwezekani leo, maana huduma siyo elimu tu.
 
wewe mwenye uelewa maisha ni ushindani, kama unajitoa kwenye ushindani jua ni dhaifu na mbumbumbu.
Ushindani labda naokubali Ni ule you vs you na sio you vs me. Hii ya you vs me Ni big no mkuu.
Mana kila mtu Anazo talanta zake. Yaani cr7 vs bolt or tiger wood vs myweather or George soros vs Michael Jordan or Elon musk vs warren buffet.
Lazima elimu iwe ya kumfundisha mtt mazingira na upeo wa kufikiria na sio ushindani wa kimitihani.
Jana ulipata d Leo una c kesho ten b later a Iyo Ni nzuri.
Jana ulikuwa umepanga Leo uko kwako na rumu zako mbili ndio mashindano. Na sio kuwa nishindane niwe Kama bill gate.
Remember hakushindana bill gate na mtu yeyote Bali alikomalia talanta zake.
 
Kinachotakiwa ni uwekezaji wa kutosha ktk kuajiri walimu wa kutosha pamoja na kujari maslahi Yao, miundombinu ya kutosha na zana toshelezi. Hapo kila kitu kitaenda vizuri. Ilu kuendeleza ni lazma serikali iwekeze kwa dhati katika sekta kuu mbili; afya na elimu. Mengine yatajiset yenyewe ukiwezea hayo mawili makuu
Ni sawa Ila elewa lazima iyo elimu Kama kijana akaishia hapo je anawezaje akaishi mtaani lakini.

Kumbuka hata China wame move from theory to more practicals. Engineer aliyetokea Kama mfumo wa veta sijui wao wanaita polytechnic Wana value kuliko waliotokea like udsm ambapo Ni theory orientated.
 
I agree with you sir Maulaga59.

Adding to that, Finland education system is the best education system in the World.

Exam based education system kills reasoning, kills thinking, kills innovation, kills creativity and kills the whole concept of learning.

Tujifunze huko Finland, tuachane na haya mamitihani.
Tehetehe! Kwahiyo ukifuta mitihani watoto watakuwa wabunifu na wagunduzi! Labda ugundunzi wa kudanga, kubeti na kuvuta bangi.
 
I agree with you sir Maulaga59.

Adding to that, Finland education system is the best education system in the World.

Exam based education system kills reasoning, kills thinking, kills innovation, kills creativity and kills the whole concept of learning.

Tujifunze huko Finland, tuachane na haya mamitihani.
Finland ni mbali na hatufanani kwa nyanja nyingi,kuwaiga tutakuwa hatujitendei haki.
Jirani zetu Kenya/Uganda/Rwanda wamepiga hatua kubwa kwenye Elimu,kwanini tusijifunze kwao?
 
Wanapiga yowe sana humu ndani,
Matatizo tunayo mengi katika elimu hilo swala la kufuta mitihani ni upumbavu tu na swala la miaka ni upumbavu zaidi.
Elimu Tanzania haijaanza leo na Hao maprofesa wenyewe wamepita katika kanuni hizo hizo.
Point ni kutengeneza Mazingira rafiki ya ufundishaji na ujifunzaji, kuboresha mitaala na kuweka mifumo inayowasaidia watu kutimiza ndoto na elimu kuleta tija/msaada katika jamii.
Sio kutuletea hizo Story za kipumbavu za kutupotezea muda. Wazazi viraza ndio watakubaliana na hayo mawazo ya kilevi. Serikali ipo kutupotezea malengo ili tusihoji sana Kadri tunavyopenda kamseleleko katika elimu ndivyo elimu inakosa thamani.

Kazi kukaa na kucopy wazungu wanafanya nini, Wao wanayo mazingira tofauti na sisi kiuchumi kuanzia ngazi ya familia mpaka serkali.
Ufute mitihani ili iweje sasa? Afu usome miaka sita ikusaidie nini kikubwa?

Ufutiwe mitihani ili tumalize wote mpaka ambao hatujaelewa tupewe vyeti afu tukavifanyie nini wakati kila swala sasa limekaa kiushindani?
Tusome miaka 6 ili tumalize mapema afu twende wapi? Peleka mtoto shule mapema ili aende na wakati.

Siasa zimezidi kwenye Mambo ya msingi tutaumizana sana.
 
Ilikuakuaje uyo mtoto wa 10 kumi akamaliza shule? Shida inaanzia mnapoforce miaka 6 kwamba mtoto amalize mdogo kwahivyo mnataka kutetea watoto kwa kuwaondolea mitihani ili wapite tu kama Ng'ombe zizini?

Jobless watajaa kitaa na Elim itakua kama dini tu yaani utamaduni usio na tija katika maendeleo ya jamii.
 
Watoto wa masikini wamegeuzwa maabara za wanasiasa.

Wanafanya majaribio kwakua watoto wao hawasomi hizo shule.

Tunatengeneza kizazi cha kutawaliwa na waliopata elimu nzuri na kutoka familia zenye nafasi kisiasa.

Watoto wa maskini wataendelea kuwa wasindikizaji tu kwenye nchi hii.

Nkikumbuka ulivokua ukimsifia mwendazake.
Na saizi umegeuka umekuwa kama opponent.
Najiuliza kuwa umetumbuliwa ama ulikuwa chawa!!!!
 
Waziri unamonea bure huo utafiti umefanywa na ngo moja ya twaweza, lakini umeshindwa kuonyesha tatizo wanao litatua liko wapi? Kwenye system eliopo naona kuna siasa ndani mfadhili ana faida mpya huenda
Kwa hiyo waziri anaitegemea Twaweza kutengeneza sera ya elimu? Acheni mambo ya ajabu, yule waziri mi hata simwelewagi atakuja kutuachia msala wa ajabu. Kwanza kwanini waishie darasa la 6? Elimu yetu siyo kichwa cha mwendawazimu kila waziri aifanyie mazoezi. Nakubaliana na michango kwamba lugha ya kufundishia iwe kiingereza kuanzia shule za awali kiswahili imetilostisha haina misamiati ya kutosha hasa katika masomo ya TEHAMA. Mfano Ms Word inaitwa programu Andishi, Ms Excel inaitwa Programu Jedwali, mambo ya ajabu kabisa neno jedwali linaendana na Ms Excel kweli? Tunapotosha na kuwapoteza watoto wrtu jumla. Je neno Programu kiswahili chake ni nini?
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Mtoto akitaka ujuzi ajiunge na vyuo vinavyotoa fani lakini elimu ya msingi na sekondari lengo lake ni kumuandaa mwanafunzi kinadharia ili sasa ajiunge kusomea fani. Haiwezekani eti shuleni mwanafunzi asifundishwe fiziksi au kemistri badala yaje afundishwe kufuga hiyo sio elimu. Kuna ujuzi mtoto anapaswa kufundishwa,nq wazazi mfano kufua, kuoga vyombo, kupika na shughuli zinhine za famila. Shuleni ni mahali pq mtoto kupata maarifa ya kinadhqria i sasa akimaliza asomee fani.

Japokuwa sijaisoma hiyo sera mpya lakini nikikumbuka ya Mungai na jinsi alivyovuruga elimu kama JK asingesahihisha sijui ingekuwaje leo hii. Tanzania tunaendeshwa na mihemko na uanaharakati kuliko kuyaendea mambo objectively. Hivi kweli tatizo ni miaka saba? Mpaka leo kuna shule hazina madawati hazina waalimu lakini hapo inaonekqna tatizo ni miaka.
Mimi naamini sio lqzima kila ntoto afike form Iv hata kama hajiwezi kimasomo. Inatakiwa,mtu asome hadi levo inayolingana na upeo wake. Mambo haya ndiyo yalifanya huko nyuma vyuo vya kqti vikqgeuzwa kutoa degree kama uyoga ili tu kucatch up na nchi zingine kwa lengo la kuongeza uwiano wa kuwa na degree na ndio tukazalisha matatizo tuliyonayo sasa..

Elimu sio kwenda tu.
We ndiyo unachanganya mambo, kuna elimu stadi na elimu ya sekondari au ya chuo yaani formal education tusiwachanganye watu. Kuna Veta unaweza jiunga hata baada ya darasa la 7. Kawaida wanaomaliza elimu ya chuo kikuu inatakiwa wawe wachache, elimu inatakiwa iwe na pyramid shape.
 
Suala la lugha huwa wanalikwepa sana.lugha imekuwa kikwazo sana kwa watanzania waliowengi.Mfamo Mtu anasoma kwa lugha ya kiswahili darasa la kwanza hadi la sita/ saba na kidato cha kwanza unafundishwa kwa kiingereza.Hapa muda mwingi unakuwa hauelewi zaidi ya kukariri na matokeo yake watz wengi wanakuwa siyo mahiri kwa lugha zote kiingereza na kiswahili.Ili kuindoa hii lazima tuchague lugha moja hasa kiingereza maana ndiyo chenye soko kubwa.
 
Back
Top Bottom