Sera mpya ya Elimu, nahisi inatatua matatizo binafsi ya Waziri

Siyo tu mwalimu, hata maprofesa wanafundisha na kutafiti wasiyoyajua!! Wizara zinaendeshwa na akina 'maimuna'. Tangu waziri, katibu mkuu na wakurugenzi.
 
Siyo tu mwalimu, hata maprofesa wanafundisha na kutafiti wasiyoyajua!! Wizara zinaendeshwa na akina 'maimuna'. Tangu waziri, katibu mkuu na wakurugenzi.
Acha dharau na ujuaji...hiyo sera inaanza kutekelezwa lini?
 
Katiba mpya itaboresha mengi
mm bado sijaona kama huo mfumo unafaa.kama humpimi mwanafunzi utajuaje uelewa wake?pia kwa sasa mtoto anaanza shule akiwa na miaka sita na atamaliza la sita akiwa mdogo sana.je ktk umri huo huyo mtoto ataweza kujitegemea?pia nataka nielezwe kama mfumo uliopo una mapungufu yapi mpaka umepelekea kufanyiwa maboresho hayo?ninavyoona kuna bomu linaandaliwa hapa na kama kweli huu utafiti ulifanywa na TWAWEZA basi kuna shida.
 
Watu mna maudhi nyie
 
Mbona unatoa mifano ya china utadhani ni dunia ambayo watu hawajawahi fika? Ni kweli umefika China ukakuta wanafunzi mashuleni na vyuoni wako 'more practical' kama unavyosema? Elimu huanza na nadharia kote Duniani mambo ya practical yako shule maalumu kama sisi ilivyokuwa technical schools na colleges.

Tatizo ni hao wanaojiita serikali walioondoa technical schools na kuzifanya ni sekondari za kawaida. Wakafunga technical schools na kuzifanya ni vyuo vikuu. It was a hopeless move! sasa hivi tena Wizara imejaza maelezo hovyo, replica of abracadabra!
 
Kuna swali muhimu linaulizwa hapa. Kwa nini tangu enzi ya mkoloni walisema umri wa kuanza shule ni miaka 7? Na kwa nini sasa Wizara inataka miaka 6? Haya ndo matatizo ya familia ya waziri eti? Nadhani tuna shida kubwa vichwani kuiachia elimu yetu mikononi mwa waziri na watu wake pale wizarani.

Wamepiga pesa ndefu ya sera mpya. Nasikia walileta mshauri toka Uingereza ili awape wasioyajua, Lakini tunafahamu ilikuwa ni dili tu!
 
Niliiona taarifa serikali ineikubali hiyo sera,swali langu inaanza lini?
Kawaida sera ikipitishwa na baraza la mawaziri, tayari inakuwa operational. Ilipotajwa kwa ufupi na waziri alimaanisha imekamilika na anaipeleka baraza la mawaziri. Kinachouma tunaelezwa eti imepitiwa na wadau wakati nasikia sehemu kubwa wamefuata maoni ya Haki Elimu utadhani hao ndo wadau wa maana.
 
Inaanza lini?..mwakani?..haki elimu wanahangaika na elimu ya nchi hii kitambo
 
Mtihani ni mhimu kuliko ujuavyo.
 
Elimu ya Tanzania inachezewa sana,kila anayeingia kwenye ngazi za juu anakuja na yake

Ushauri wangu kuhusu Sera mpya ya Elimu isitishwe kwanza.
Serikali itekeleze sera iliyopo kwa asilimia mia (100%) ndio tuje tupime kasoro au faida zake.
Mfano:
1.Waajiriwe walimu kadri ya mahitaji.yaani wanafunzi 45 mwalimu moja.
2.Pawepo na vitabu vya kiada angalao watoto wawili kitabu kimoja.
3.Walimu wapatiwe maslahi bora,vifaa vya kufundishia vitoshee mahitaji.
4.Vyumba vya darasa kama havitoshei kuwepo na awamu mbili za kuja shuleni ili watoto wote waweze kushirikiana vyumba vichache vilivyopo.
Hapo sasa ndio tupime ufanisi wa mtaala wetu kwa kufuatilia mwenendo wa kitaaluma wa mwanafunzi na mwenendo wa kitaalamu wa mwalimu.
Kubadili mara kwa mara sera,huku sera zilizopo hazitekelezwi ipasavyo ni kujidanganya na kupoteza fedha za umma.
Pia kuongeza vyumba vya madarasa huku idadi wa walimu haitoshei ni kujidanganya.
Serikali/wanasiasa wamejikita kwenye ongezeko la idadi ya vyumba vya madarasa na madawati kama ndio kuboresha elimu huku idadi wa wanafunzi kwa mwalimu moja ikiwa ni kubwa,haiwezi kuleta matokeo chanya hata siku moja.
 
Kingereza kina faida gani hapo kwenye kumalizia?ila sisi waafrika wazungu walituweza sana
 
Empty mind in place.
 
Kingereza kina faida gani hapo kwenye kumalizia?ila sisi waafrika wazungu walituweza sana
Labda upeo wako ni mdogo sana juu ya mambo ya kimataifa, ujue tu kuwa hata nchi za ulaya zilizo na uchumi imara na utaifa watu wake wengi wanajua hicho Kiingereza. Ukitaka kufanya kazi kwenye mashirika ya kimataifa na hata UMOJA wa mataifa lugha ya kwanza ni kiingereza. Hata Urusi viongozi wake wanajua Kiingereza unadhani wamejifunza ukubwani kama siyo shuleni.

Umewahi kusikia balozi wa nchi yoyote Duniani aliyeko hapa Tanzania hajui Kiingereza? Au unadhani walijifunza baada ya kuteuliwa? Kama wewe umejiandaa kuwa mtendaji wa Kijiji au kata Baki na kiswahili chako, na hiyo lugha ya mkoloni waachie wenye kusaka fursa popote duniani.
Kiispania ni Moja ya lugha yenye wazungumzaji wengi duniani, hata wachina Wana lugha Yao lakini sifa kubwa lazima kiingereza. Achaneni na mambo ya kina Walter Rodney kwamba Africa na Ulaya zilikuwa sawa kabla ya ukoloni, mtu uliye naye sawa Kila kitu anakutawala vipi? Kiingereza ni kiswahili Cha Dunia.
 
Tutamkumbuka Merehemu (RIP). Nimemkumbuka yule mama aliyejidai kujitangazia eti amefuta kozi za certificate ya ualimu na kutunga digrii za ualimu wa shukle za msingi. Kwa hili la sera, Jiwe angekwisha lala sambamba na wasanii hawa wa elimu.

Sasa eti rais naye anatutolea mifano ya Kishimba wa Bungeni, halafu wanaoitwa wataalamu wameibeba na kuondoa darasa la 7! Kama wanataka maprofesa waende vijijini wakafundishe kukamua ng'ombe ili mtoto wa kishimba ajue kukamua, asimsumbue.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…