Nimesoma post zote 1-20 naona shida kubwa sana.
Moja hata mleta mada hajui anataka Nini, maana ukweli hakuna ajira isiyo na interview, na nimeshiriki interview nyingi sana kwenye ajira za walimu shule za Private. Yeyote aliyetimiza vigezo vya Tangazo aliitwa kwenye usaili. Mfano Kuna shule mpya ilikuwa Dar tulihitaji walimu 9 tukipata applications 391 na wote walimeet initial screening procedure. Sheria inatak uwaite.
Baada ya hapo tuliscreen na kupata walimu 36 tukawapa interview ya pili wakabakia 19 then tunafanya mwisho tukipata serious teachers 9. Na shule ipo vizuri sana sana(form two mbili zilizopita wote division one) mwaka huu itakuwa na form four ya kwanza.
Hakuna kubebana wachaga waitwe kwenye usaili lakini pia best teacher sio GPA hata kidogo bali uwezo binafsi wa mwalimu. Mfano: Kuna walimu wa kiingreza hawawezi kuzungumza kiingreza five minutes leave alone grammar.
Jambo la pili naona walimu wengi wamefocus kuaniriwa tena serikalini. SI lazima uajiriwe unaweza kujiajiri (walimu watatu au wanne anzisheni tuition center, QT, n.k) huku mnaeeza kujenga majini na kupata ajira. Ombeni kufundisha remedial classes kwenye shule hizo mnagawani mshiko na walimu). Lakini pia mnaeeza kuandaa notes, pamphlets, compendium au vitabu kwenye maeneo yenu ya ubobezi. Etc
Mnamlaumu Prof. Mkenda as if yeye ndio yupo kwenye Halmashauri.,
Mwisho kama walimu wengi ni watoto wa wakulima m ona hatuoni wakikwasaidia wazazi wao kuongeza tija kwenye kilimo na ufungaji badala yake wapo TikTok, X, fB etc. wasaidieni. Kwenye kilimo Kuna tija kubwa sana