Sera ya Elimu ni janga kwa vyuo vya ualimu nchini. Ni janga kwa wasomi wa shahada za ualimu nchini!

Sera ya Elimu ni janga kwa vyuo vya ualimu nchini. Ni janga kwa wasomi wa shahada za ualimu nchini!

Elimu imechezewa sana na walimu vilaza, ni muda wa kuajiri vijana wenye uwezo mkubwa tu kwenye sekta muhimu kama elimu.
Kwa mshahara wa kipumbavu na mazingira ya mabovu usitegemee badiliko lolote katika elimu yetu
 
Mleta mada una hoja ila umeileta kwa mihemko na asira zisizo na maana ata elimu yako inaonekana haijakukomboa utakuwa mtu wa kufeli kila siku.Katika vitu vya ajabu kuwahi kutokea ni kuajiri watu bila kupima uwezo wake.kwa muda mrefu tumekuwa tunapata watumishi wa umma weupee kichwani na hasara tunayopata kama taifa ni kubwa saaana.sasa waziri amejiongeza na kukataa mteremko wewe unamtukana kwa kutaka tuendelee kuajiri vilaza.shauri kama unaona kuna mapungufu lakini utaratibu wa kuajiri walimu na madaktari for free ni ujinga kuliko ujinga wenyewe.nakupongeza saana mheshimiwa mkenda na serikali kwa ujumla
.
 
Kuna video niliiona anajitetea bungeni,nikagundua nchi zinazofanya interview kwa walimu ni chache sana duniani,pia nikagundua atakuwa na malengo ya kuanzisha lugha ya kiingereza toka chekechea

Ila kuna kitu cha kijinga alikisema eti walimu wawe wanajiendeleza ili wafaulu interview,mbaya zaidi hz interview hata walikuwa hawasahihishi mitihani

Mwisho wa zoezi watueleze wametumia kiasi gani kuendesha huu mradi wa kipigaji
View attachment 3236595
Kwahy mtu aajiriwe kisa amekaa muda mrefu mtaani, yn hilo tuu ndio iwe kigezo?
 
Mimi shida yangu si huo wingi, Bali ni aina ya maswali......yalikuwa favourable kwa mtu aliyemaliza mwaka jana au juzi tu lakini waliomaliza 2018 huko walitengwa kabisa......na Kwakweli wameumizwa na kudhulumiwa sana. Huruma Kwakweli. Mtu yupo mtaani miaka 8, anashighulika na kilimo tu, ghafla analetewa maswali ya kifalsafa tupu ambayo yanahitaji mtu anayesoma na kutestiwa Kila siku. Kama hilo halitoshi, pass mark ilikuwa 80😭😭😭😭. Kwa hapa, kilio changu kipo pamoja na mleta mada.....wamedhulimiwa nauli na muda wao ndugu zetu wa miaka ya 2018, 2019 na 2020
Pole sana mwalimu
 
Walimu wana kitu gani spesho wasipewe usaili!? Ila wengine iwe sawa!! Huoni kuwa ndiyo wakati sasa taaluma yao inaenda kupata heshima.. Mfumo umebadilika wacha na walimu waheshimu hiyo kazi yao kwa kufanyiwa usaili. Moja kabisa ya vitu vinashusha hadhi ya ualimu ni kuupata bila jasho.. Hata walimu wana jidharau. Sababu hiyo mbona private wana jitambua ni sababu ya usaili..
Mazoea nadhani ndo shida. Ila walimu haohao ili kufundisha private schools wanaomba kazi, wanafanyishwa interview kisha ajira. Serikalini ilikuwaga post tu..nadhani ni kubadili mindset..japo kweli inategemea hizo interview zina lengo gani ziko positive kweli kiasi cha kufanya walimu wazidi kujiimarisha wanapokuwa masomoni. Na serikali iangalie mtiririko mzima wa kuwasomesha walimu husika kuanzia sifa za kujiunga vyuo..wao wenyewe wanachukuaga wale wa grade au div. Za fair au chini na kuwapa wasome ualimu..waanze kuchukua na 1 na 2 tuone, ...kimsingi kuna mambo ya kuangalia mengi ktk kadq ya ualimu
 
Usaili umefanyika kwenye maeneo yao wanapoishi, wengine wameenda kwenye usaili kwa miguu kutokana na ukaribu, hasara ipi hy unazungumzia?
Waliwafuata mpaka huko kijijini wanakoishi baadhi yao? Gharama inakuja katika forms nyingi. Hata time spent ni gharama - time is money. Watu wameacha shughuli zao za kilimo, bodaboda, machinga, etc ili waende kwenye usaili usiokuwa na tija. Hiyo ni hasara!
 
Mifumo hii ya elimu yetu bado haijawa supportive kwa wasomi wengi japokuwa ,hizo interview zimetawaliwa na rushwa tupu
 
Utakandwa tena subiria PSRS wakuite tena utaelewa tu unashangaa miaka 10 hii hapa haujaitwa kazini nenda kuponde mawe uuze
Mkuu, mm kama waalimu wanaosubiri kuajiriwa serikalin miaka yote hy, ety mtu mzima na akili zako unalalamika kukaa mtaani miaka 10 ukisubiri kuajiriwa ualimu serikalin 😂.
 
Waliwafuata mpaka huko kijijini wanakoishi baadhi yao? Gharama inakuja katika forms nyingi. Hata time spent ni gharama - time is money. Watu wameacha shughuli zao za kilimo, bodaboda, machinga, etc ili waende kwenye usaili usiokuwa na tija. Hiyo ni hasara!
Forms nyingi zipi hizo?
Kwahy kukaa nyumbani miaka 10 sio kupoteza muda?
Kuacha kulima na shughuli zngn kwa siku moja ambayo tayari ulikuwa una ratiba nayo kuwa utaenda kwenye usaili ndo itakufanya uwe masikini wa kufa?
 
Pole kwao.

Maisha ni fumbo.

Kwenye hili la ajira wapo waliofurahi sana (walifaulu/waliopata nafasi) na kuwaombea mema au kuwashukuru walioendesha na waliosimamia usaili.

Pia wapo waliopata huzuni kwa kukosa nafasi hizo. Wapo baadhi watashukuru na kukubaliana na matokeo lakini pia wapo baadhi yao watakaolaani na kuwalaumu waendeshaji na wasimamizi wa usaili huo.

Kwa upande wa waandaaji na wasimamizi wa usaili huo kuna mawili yanayowakabili: laana na baraka yaani vyote kwa pamoja. Lipi litawapata sijui (laana au baraka au vyote)! Ndivyo maisha yalivyo: kukosa na kupata; kulaaniwa na kuabarikiwa.

Zama hubadilika, kila zama na mambo yake. Leo dunia (hasa Africa ikiwemo Tanzania) inayashuhudia ya Donald Trump ambayo zama za Joe Biden na wengine waliopita hayakuwepo. Pia tumeshuhudia haya ya usaili ambayo hayakuwepo kwa zama zilizopita.

Ukitafakari sana haya mambo yanayotokea utagundua kuna sababu ya kutokea, kuna fundisho au jambo utajifunza ukiachilia mbali kupoteza au kukosa fursa. Dunia inabadilika.

Pole sana kwa walimu waliokosa nafasi za ajira na hongera kwa hao waliopata nafasi.

Kwa waliokosa nafasi wasikate tamaa bali watambue kwamba uwezo, utu na mchango wao kwa jamii ni wa juu na muhimu sana hata bila kuwa na ajira serikalini.

Kwa waliopata nafasi za kazi watambue kwamba wanawajibu wa kutendea haki nafasi hizo, watambue kwamba kuna sababu ya wao kupata na wengine kukosa.

Kila la kheri.
 
Kuna point ya msingi anayo mathalani graduate alyesoma BA in geography and environmental studies ameitwa kwenye usaili wa somo la geography lakini maswali ya written interview unaulizwa maswali ya ualimu mwaka wa pili , hapa ndipo ujuha unapokuja na kupotezeana muda na pesa . Ujinga kabisa wa hali ya juu kwann huyu aitwee kwenye interview hali ya kuwa unajua hajasoma reaching methodology, lesson development, lesson plan ,psychology na mengine!!!!!
 
Back
Top Bottom