Sera ya Elimu ni janga kwa vyuo vya ualimu nchini. Ni janga kwa wasomi wa shahada za ualimu nchini!

Sera ya Elimu ni janga kwa vyuo vya ualimu nchini. Ni janga kwa wasomi wa shahada za ualimu nchini!

Mleta mada unalalamika bure pasipo hoja. Suala la usaili kabla ya kuajiriwa ni jambo la msingi katika fani zote dunia nzima. Unaweza kuwa na maoni tofauti kuhusu namna ya kuendesha usaili lakini huwezi kukwepa uwepo wa usail.

Kwanini mwalimu yeye tu hataki kusailiwa?
Kama kuna maelfu ya wahitimu wa ualimu mtaani huku nafasi za kuajiriwa zikiwa chache, kwanini usaili usitumike kama ndio njia bora ya kuwashindanisha?
 
Usaili ni lazima na muhimu, kama hutaki endelea kukaa kwenu ukisubiri muujiza.
 
Wakichaguliwa bila usaili maneno mengi, wakifanyiwa usaili maneno mengi.
Kwahiyo serikali iajiri malaki yote ya walimu wanaohitimu kila leo?
 
Siyo kutengeneza ajira tu, pia ni kuweka mazingira mazuri kwaajili ya wananchi kujiajiri.

Serikali haiwezi kuajiri watu wote waliohitimu.
Nadhani tuko pamoja, kutengeneza ajira siyo kwamba yenyewe ndiyo iwe mwajiri, ni pia unalosema la kutengeneza mazingira ya ajira silipendi neno kujiajiri kwakua Lina madhara pia katika kutengeneza ajira maana watu wanapata kichaka Cha kujificha udhaifu wao.

Mbaya zaidi katika nchi zetu Africa na Tanzania in specific wengi hawaelewi hata maana ya kutengeneza ajira ni nini, ndiyo sababu hawajui chakufanya lakini wanawaambia wenzao wajiajiri wakati wao wameajiriwa na bado wanafunga masikio hata wakielezwa hawataki kufungua akili zao waelewe tunachokisema ni kipi...Ajira zimebaki zile zile alizoanzisha mkoloni.. ndiyo sababu Sina huruma Kwa hao wafanya maamuzi ambao wanataka ku shift burden Kwa raia ilihali ni jukumu lao kutengeneza ajira na kuwatengeneza waajiriwa wawe effecient and productive; mara nyingi wao ndiyo vikwazo number moja
 
Anajifanya anajua sana ubora wa elimu ila hajali maumivu wanayopitia watoto wetu afu hajali kabisa upungufu wa walimu vijijini hali ni mbaya sana hadi wanafunzi wameanza kurudia kama zamani.
Wewe ulitaka kila aliyeitwa kwenye usaili apate ajira sio? Au apewe chai, nauli nk.
 
Kama sera mpya ya ELIMU ndo imeweka utaratibu wa usaili kwa walimu basi hiyo sera inafaa sana!
Ualimu na mchakato wa kuwaandaa walimu ulifanywa kama wa kuwatakatisha na kuwatunuku waliofeli vyeti vya taaluma!
Walimu wengi mashuleni wamebweteka. Wengi hawana morali. Wachache wanaojitambua bado wana uelewa mdogo sana.
Ni kama ajira na maslahi kwao ni fadhila...
Wengi wapo kazini kwenye mazingira na vituo vya kazi chakavu na hatarishi lakini hawajali!
Kifupi walimu ni chanzo cha kushuka kwa UBORA wa ELIMU nchini!

No wonders hawapendi usaili (interviews)
 
Sikia ndugu mtu amekaa chuo miaka mitatu unampimaje kwa interview ya nusu saa?
Zipo kada nyingine zilizokaa chuoni zaidi ya hiyo miaka mitatu na bado zinafanyiwa interview kwa muda huo huo, kuna taasisi za kimataifa unapewa dakika 10 tu wanakuwa wameshafanya tathmini ya kutosha na huko wanachukua mtu aliyeanzia level ya Master's inamaana amekaa chuoni miaka 5+
 
Kitu rahisi hicho; you raise the bar. Waulize vijana wanaoomba kwenda kusoma MD Muhimbili. Kupata division one hakutoshi. Ni division one ya points ngapi? Wanachukua mostly division one ya points 3, 4, 5. If you raise the bar in a similar fashion, you won’t have to invite 15,000 candidates for an interview to fill only 200 teaching positions!
Bado wanaoapply MD Muhimbili sio wenye Division 1 ya 3, 4 na 5 tu. Hawajafunga mlango kwa wengine, nimeambatanisha vigezo vyao hata mtu mwenye division 2 ya point 12 anaweza kuapply na huwa wanapokea maelfu ya maombi wakati wa udahili ila wanaohitajika si zaidi ya 250
1000023276.jpg
 
Sera ya elimu inatakiwa kuwa sambamba na dira ya taifa.

Unawezaje kuitangaza sera ya elimu, kabla ya kutoa dira ya taifa.

Kwetu ni sawa, ila wazungu wanatuona mataahira tu,

Like serious huko serikalini kuna watu wana undergraduate degrees za management of all sorts.

Better still kuna watu wana MBA’s of all sorts.

Kwa upuuzi wa nafasi tunazopeana kwa ujinga, kwa nchi zilizoendelea ni rahisi sana kuona uwezo mdogo wa hao watu. Na wana uwezo mdogo kweli kweli.

If you know anything about strategic planning dira ya nchi inakuja kwanza (national objective), then strategic planning follows. Ambayo ina mengi kufikia national vision/objectives.

Sasa unawezaje panga dira ya national curriculum, kabla ya dira ya taifa.

Civil services imejaa watu wenye uwezo mdogo mno.

Let me remind you, usalama wa taifa ni mchezo wa watu wenye akili.

Na asilimia kubwa ya wachangiaji wa JF you can tell, hawana ata basics za lines of reasoning za siasa.

Shida ni uwezo mdogo

98% ya wachangiaji wa jukwaa la siasa hawana technical knowledge ya mambo wanayoongelea.

Ujinga mtupu

Ndio ukweli

Wazungu wenye akili sio uwezo tu, jamaa wanasoma. Asilimia kubwa ya wachangiaji wa JF hawana hata abc za topic husika.

Ukisoma post ujinga mtupu unao onyesha uelewa mdogo wa mambo na kugongeana likes.

Hamna uwezo
 
Kwani interview ina ubaya gani kama kweli mtu ni mualimu na kausomea kuna ubaya gani kupewa usaili?
Mtu kasomea ualimu au nursing, hakuna matawi au vipengele ndani yake. Amesoma hatua kwa hatua kwa usimamizi wa chombo maalum cha taaluma husika kisha akapimwa kwa kipimo mahsusi kinachosimamia taaluma na kufauli kwa nadharia na vitendo. Na vyeti vipo.

Interview inakujaje hapo?

Kama ndivyo, ifahamike kuwa vile vyuo vya ualimu na nursing vya serikali, navyo haviaminiki. Tuwape interview hadi wahitimu wa majeshi yote pia.
 
If you anything about strategic planning. Huwezi kuwa na dira ya elimu, kabla ya dira ya nchi, policies/laws (implementation strategies) and training/skills required to execute the strategy.

Kitendo cha kuwa na dira ya elimu kabla ya serikali kutoa dira ya maendeleo (ni upuuzi uliopita kiasi).

Hiyo dira ya Mkapa hata kuongelea ni ujinga.

Ni hivi usalama wa taifa ni mchezo wa watu wenye akili. Na usalama wa taifa unaanza na senior civil servants.

Katibu mkuu kiongozi, mkurugenzi wa wizara, secretary wa waziri na senior civil servants wengine sio watu wa kuokota tu; wanatengenezwa na system.

Mnaweza kujiongopea ujinga, lakini watu wa nje wanaona.

Asilimia kubwa ya senior civil servant Hawana uwezo kwa mambo ya ujinga kama haya ukisoma.

Ndio ukweli
 
Mtu kasomea ualimu au nursing, hakuna matawi au vipengele ndani yake. Amesoma hatua kwa hatua kwa usimamizi wa chombo maalum cha taaluma husika kisha akapimwa kwa kipimo mahsusi kinachosimamia taaluma na kufauli kwa nadharia na vitendo. Na vyeti vipo.

Interview inakujaje hapo?

Kama ndivyo, ifahamike kuwa vile vyuo vya ualimu na nursing vya serikali, navyo haviaminiki. Tuwape interview hadi wahitimu wa majeshi yote pia.
Sasa kama umepita huko kote unaogopaje usaili 😂
 
Back
Top Bottom