Sera ya Elimu ni janga kwa vyuo vya ualimu nchini. Ni janga kwa wasomi wa shahada za ualimu nchini!

Sera ya Elimu ni janga kwa vyuo vya ualimu nchini. Ni janga kwa wasomi wa shahada za ualimu nchini!

Mganguzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2022
Posts
1,604
Reaction score
3,715
Majuzi nimekaa kwenye bwalo la halmashauri ya Mbeya vijijini nikishuhudia machozi ya vijana wasomi wa kitanzania wakimwaga machozi baada ya kuonekana hawajapita kwenye interview ya inayosimamiwa na watu wasiojua thamani na gharama za mtu kukaa miaka mitatu akipambania shahada ya ualimu kwa jasho damu!

Mtu anapambana chuo halafu analetwa Waziri anaitwa Mkenda anatumia “vikundi vya wahuni” kwenda kuwafanyia interview wasomi wetu wenye qualifications zote kwa kuwauliza maswali ya kishenzi dakika kumi baadae anaambiwa arudi nyumbani.

Waziri Mkenda machozi ya hao watoto yatakuwa laana hata juu ya kaburi lako! Wasomi wote unaowaona leo hata wewe mwenyewe pamoja na Rais wako mliaminiwa kwa shahada zenu ndio maana wewe leo ni profesa. Acha kuwatesa watoto wa watu kwa upumbavu na kwa sera za kishenzi!

Mnajificha kwenye kichaka cha interview kukwepa maswali ya upungufu wa ajira nchini! Mnashindwa kuendeleza mfumo wa kutoa ajira kwa wasomi na kutumia mfumo wa kikoloni sasa binti zetu huko kwenye maintaview yenu wanabakwa ili kuhakikisha labda watafanikiwa.
 
Kwani interview ina ubaya gani kama kweli mtu ni mualimu na kausomea kuna ubaya gani kupewa usaili?
Imagine unahitaji kujaza nafasi 200. Kuna sababu gani ya kuita 15,000 candidates kwenye interview, kama sio kutengeneza mazingira ya rushwa? Unapaswa kuwa na filter itakayokupa a sensible shortlist ya candidates utakaowaita kwenye interview. Otherwise, utatia watu wengi hasara isiyokuwa ya lazima!
 
Mkuu wewe wataka aweke filter gani itakao kua fair kwa kila mtu.
 
Walimu wana kitu gani spesho wasipewe usaili!? Ila wengine iwe sawa!! Huoni kuwa ndiyo wakati sasa taaluma yao inaenda kupata heshima.. Mfumo umebadilika wacha na walimu waheshimu hiyo kazi yao kwa kufanyiwa usaili. Moja kabisa ya vitu vinashusha hadhi ya ualimu ni kuupata bila jasho.. Hata walimu wana jidharau. Sababu hiyo mbona private wana jitambua ni sababu ya usaili..
 
Mkuu wewe wataka aweke filter gani itakao kua fair kwa kila mtu.
Kitu rahisi hicho; you just raise the bar. Waulize vijana wanaoomba kwenda kusoma MD Muhimbili. Kupata division one hakutoshi. Ni division one ya points ngapi? Wanachukua mostly division one ya points 3, 4, 5. If you raise the bar in a similar fashion, you won’t have to invite 15,000 candidates for an interview to fill only 200 teaching positions!
 
Kitu rahisi hicho; you raise the bar. Waulize vijana wanaoomba kwenda kusoma MD Muhimbili. Kupata division one hakutoshi. Ni division one ya points ngapi? Wanachukua mostly division one ya points 3, 4, 5. If you raise the bar in a similar fashion, you won’t have to invite 15,000 candidates for an interview to fill only 200 teaching positions!
200 wengi. Kuna watu 28000+ waliitwa Kwa ajili ya nafasi 184. Ndo ujue tunaongozwa na wajinga.
 
Kitu rahisi hicho; you raise the bar. Waulize vijana wanaoomba kwenda kusoma MD Muhimbili. Kupata division one hakutoshi. Ni division one ya points ngapi? Wanachukua mostly division one ya points 3, 4, 5. If you raise the bar in a similar fashion, you won’t have to invite 15,000 candidates for an interview to fill only 200 teaching positions!
Huwezi kitumia arama za ufauli kumpima mualimu muzuri professional ya ualimu ni practice kuliko theoretical, interview inaangalia mambo mengi sio ufauli wako tu, kuna mtu anaweza na GPA ya 5. Ila asojiwe jinsi ya class management wakati wa GPA 2.5 anuwezo mkubwa katika class mangement nk.
 
Kwani mkenda ali'graduate mwaka gani? Kipindi ualimu ni deal ndo kasoma, sasa hivi waalimu wamezagaa kama nyanya sokoni ni kibaya zaidi wengi ni watoto wa wakilima peasants hawana plan B zaidi ya kuajiliwa na serikali tu.
Mkuu usiseme hivo, usione wajinga kwamba hayo yote hawayafikirii..Jaribu kuvaa viatu vyao na kama ww ulipata nafasi ya kuepukana na hiyo changamoto basi shukuru tu Mungu kisha ukae kimy.
 
Back
Top Bottom