You are very right ndugu
dudus...
Kwa nyongeza tu mimi nime notice mambo kadhaa;
1. KWANZA; watu waelewe kuwa hakuna shida kwa mtu aitwaye Freddy Kapala kufanya kazi tiGO kama Mwanasheria au vyovyote vile...
2. PILI, watu hawana shida na mtu aitwaye Freddy Kapala kusimama mahakamani na ku - testify against Freeman Mbowe na wenzake...
3. Watu wana shida na njia iliyotumika kupatikana kwa ushahidi huo ambayo totally ni illegal kwa kumtumia shahidi huyo anayejiita Legal Advisor wa kampuni kubwa ya mawasiliano ya tiGO, bwana Freddy Kapala...
##Na hii ndiyo inayopelekea kila mtu kujiuliza maswali kadhaa ili kujua "nia" ya serikali kwa kuwatumia Polisi ni nini hasa kumfungulia Freeman Mbowe kesi hii iwapo ushahidi tu wa ku - incriminate wanautafuta kwa "tochi" na kwa kutumia njia haramu kinyume kabisa cha kanuni, sheria na katiba ya nchi...!
Mfano;
å Kwa maelezo ya Freddy Kapala mahakamani tunapata picha kuwa, the entire management ya tiGO/MIC Company haikuwa aware kuwa kampuni yao inahusishwa na kesi hii kubwa ya ugaidi kupitia mteja wao mmoja Freeman Mbowe isipokuwa mfanyakazi wao mmoja tu aitwaye Freddy Kapala...!!
å Hivi ilikuwaje barua toka Polisi anaipokea huyu huyu Freddy Kapala, kuifanyia kazi, kuijibu na kusaini na kugonga mihuri yote bila mtu mwingine yeyote ndani ya kampuni kuhusishwa tena jambo lenyewe likihusu UGAIDI...???
å Iliwezekanaje Polisi waindakie tiGO barua kutaka taarifa za mteja fulani (hapa ni Freeman Mbowe) bila kueleza sababu au kosa kisha tiGO kwa ujinga au kwa makusudi kupitia kwa Mwanasheria wao FREDDY KAPALA bila kuhoji mambo ya msingi wakafanya vile...???
å Kwa nini Polisi hawakutumia njia rasmi kupata taarifa au data za wanayemshuku kuwa ni mhalifu na badala yake wanatumia njia ya mlango wa nyuma? Yaani wanataka kuthibitisha fulani ni mhalifu/gaidi lakini wao mwenyewe Polisi wanatumia njia za kihalifu...??
å Kuna uhusiano gani kati ya Freddy Kapala na Polisi..???
HITIMISHO:
##Hii kitu si tu imevunja SERA ya faragha ya kampuni ya tiGO bali imevunja sheria na katiba ya nchi...!!
##Hapa tiGO ili kuepuka legal consequences dhidi ya tendo hili toka kwa mteja wao Freeman Mbowe, wana options 3 tu;
1. Aidha wamkane huyu Freddy kuwa siyo mfanyakazi wao
AU;
2. Ni mfanyakazi wao lakini amefanya yeye binafsi na kwa hiyo ni mhalifu kama wahalifu wa matandao (hachers) wengine wowote duniani
AU;
3. Wakae tayari kumlipa Freeman Mbowe mabilioni kadhaa ya shilingi kwa ku disclose faragha yake kinyume cha sheria!