Sera ya faragha MIC Tanzania Public Limited Company - tiGo

Sera ya faragha MIC Tanzania Public Limited Company - tiGo

Hii ni hatari sana!
Kiuhalisia sio Tgo tu! Nakumbuka nliwai pata shida na mtu, polisi walifanya kila kitu kujua mawasiliano yake yooote toka VODACOM....shemeji yangu kipindi flan akapata taarifa zoooote za mkewe toka Tgo na sio kupitia polisi, aliwasliana tu na mtu Tgo akamtoa masenti akamprintia
 
Kumbe hata sera zao za privacy hazimlindi mtumiaji.tigo sio mtandao kabisa
 
Muda muafaka wa kuiburuza TIGO mahakamani kwa uvunjaji wa sheria za siri za wateja wao, ningekuwa na line TIGO ningejitoa haraka sana, makampuni mengine ya simu yapigilie hapo kuchukua wateja wa TIGO na bango langu lingekuwa ile statement ya shahidi # 5 TUNATII ZAIDI MAMLAKA ZAIDI YA SIRI ZA WATEJA
 
Wala haya hayana sifa ya kuwa maoni. Huu ni ujinga wake.
Ulisha isoma sheria husika ndio inavyo sema? Au ni maoni yako tu,kimsingi pamoja na ubovu wa sheria yetu lakini imeweka utaratibu wa kisheria wa jinsi yakupata taarifa za mteja,sio kweli kuwa polisi wanaweza kuomba data za mteja bila kutoa sababu na waka pewa hapana, wanaweza wakanyimwa kama mtoa huduma hataridhika na sababu na hapo wanapaswa kuiomba mahakama itoe order kwa service provider atoe data. Sio kirahisi kama walivyo fanya tiGo rejea kesi ya Jamiiforum v/s Jamhuri.
 
Applicable law and jurisdiction

The interpretation, use, scope and termination of this Notice is governed by the laws of the United Republic of Tanzania and, in case of dispute, the courts of Tanzania will have exclusive jurisdiction.
 
Polisi ni chombo Cha kisheria mfano wewe ni jambazi umepanga nyumba unafanya matukio .Hawahitaji kibali Cha kumhoji mwenye nyumba wako kukuhusu wewe Kama customer wa mwenye nyumba.Ataitwa polisi au polisi watafika kwake kumhoji kuhusu huyo jambazi wake customer . Kwenye mitandao ya simu wewe mpangaji tu mwenye nyumba ni kampuni ya simu ukifanya uhalifu au ugaidi polisi ruksa kudai information kwa mwenye nyumba sababu sio kazi za mwenye nyumba kutunza Siri za jambazi au mhalifu au gaidi lazima atamwaga kila kitu
Usahihi wako uko kwenye hisia na si sheria. Purely layperson. Kuna haki kuna wajibu. Naona uko mbali sana katika sheria.
 
Mara mia tigo kuliko voda.voda ndio wanaweza share taarifa zako na mtu yeyote hata muuza nguo online
 
Sheria gani za kimataifa unazungumzia? Ni lazima kuwepo na “warrant” ambayo huwa inatolewa na mahakama. Hata Mbowe walivyoenda kumshachi, ilikuwa ni lazima wawe na “search warrant” ambayo hutolewa na mahakama baada ya mahakama kujiridhisha. Hapa kwetu, kwa mujibu wa Tigo, polisi anaweza kwenda tu na barua ya kutaka information za Mteja...Kwa marekani Soma hapo chini kama unaelewa ukisoma...

“The U.S. Supreme Court ruled that police need a warrant to obtain cellphone location information routinely collected by wireless providers. In a landmark decision, the U.S. Supreme Court ruled Friday that police must obtain a search warrant to access an individual's cellphone location information.”

Source:
.22 Jun 2018
View attachment 1997135
NPR Cookie Consent and Choices › 2018/06/22

Appicable law and jurisdiction

The interpretation, use, scope and termination of this Notice is governed by the laws of the United Republic of Tanzania and, in case of dispute, the courts of Tanzania will have exclusive jurisdiction.
 
You are very right ndugu dudus...

Kwa nyongeza tu mimi nime notice mambo kadhaa;

1. KWANZA; watu waelewe kuwa hakuna shida kwa mtu aitwaye Freddy Kapala kufanya kazi tiGO kama Mwanasheria au vyovyote vile...

2. PILI, watu hawana shida na mtu aitwaye Freddy Kapala kusimama mahakamani na ku - testify against Freeman Mbowe na wenzake...

3. Watu wana shida na njia iliyotumika kupatikana kwa ushahidi huo ambayo totally ni illegal kwa kumtumia shahidi huyo anayejiita Legal Advisor wa kampuni kubwa ya mawasiliano ya tiGO, bwana Freddy Kapala...

##Na hii ndiyo inayopelekea kila mtu kujiuliza maswali kadhaa ili kujua "nia" ya serikali kwa kuwatumia Polisi ni nini hasa kumfungulia Freeman Mbowe kesi hii iwapo ushahidi tu wa ku - incriminate wanautafuta kwa "tochi" na kwa kutumia njia haramu kinyume kabisa cha kanuni, sheria na katiba ya nchi...!

Mfano;
å Kwa maelezo ya Freddy Kapala mahakamani tunapata picha kuwa, the entire management ya tiGO/MIC Company haikuwa aware kuwa kampuni yao inahusishwa na kesi hii kubwa ya ugaidi kupitia mteja wao mmoja Freeman Mbowe isipokuwa mfanyakazi wao mmoja tu aitwaye Freddy Kapala...!!

å Hivi ilikuwaje barua toka Polisi anaipokea huyu huyu Freddy Kapala, kuifanyia kazi, kuijibu na kusaini na kugonga mihuri yote bila mtu mwingine yeyote ndani ya kampuni kuhusishwa tena jambo lenyewe likihusu UGAIDI...???

å Iliwezekanaje Polisi waindakie tiGO barua kutaka taarifa za mteja fulani (hapa ni Freeman Mbowe) bila kueleza sababu au kosa kisha tiGO kwa ujinga au kwa makusudi kupitia kwa Mwanasheria wao FREDDY KAPALA bila kuhoji mambo ya msingi wakafanya vile...???

å Kwa nini Polisi hawakutumia njia rasmi kupata taarifa au data za wanayemshuku kuwa ni mhalifu na badala yake wanatumia njia ya mlango wa nyuma? Yaani wanataka kuthibitisha fulani ni mhalifu/gaidi lakini wao mwenyewe Polisi wanatumia njia za kihalifu...??

å Kuna uhusiano gani kati ya Freddy Kapala na Polisi..???

HITIMISHO:

##Hii kitu si tu imevunja SERA ya faragha ya kampuni ya tiGO bali imevunja sheria na katiba ya nchi...!!

##Hapa tiGO ili kuepuka legal consequences dhidi ya tendo hili toka kwa mteja wao Freeman Mbowe, wana options 3 tu;

1. Aidha wamkane huyu Freddy kuwa siyo mfanyakazi wao

AU;

2. Ni mfanyakazi wao lakini amefanya yeye binafsi na kwa hiyo ni mhalifu kama wahalifu wa matandao (hachers) wengine wowote duniani

AU;

3. Wakae tayari kumlipa Freeman Mbowe mabilioni kadhaa ya shilingi kwa ku disclose faragha yake kinyume cha sheria!
Shukrani sana kiongozi; umehitimisha thread. Hata hivyo sentensi ya mwisho kabisa umegusia "faragha yake kinyume cha sheria".

Nina mashaka kama nchi hii ina sheria inayohusika na personal data protection.
 
... tatizo la msing kwenye hili suala la tiGO ku-expose taarifa za wateja ni namna walivyo-expose! Walitakiwa ku-expose kwa amri ya mahakama ila kuto-expose kabisa isingewezekana. Suppose ni wewe umepata madhara na njia iliyosababisha madhara hayo ni kupitia mawasiliano ya simu na ushahidi wa madhara hayo njia pekee ya kuuthibitisha ni kupitia data kutoka mtandao husika; ungepinga kwamba wana-expose taarifa za wateja? Tuwe tu wakweli.

Hata hivyo kwamba Mbowe alituma mwamala tarehe fulani sio issue kwa sababu hakuna cha ajabu kwa Mbowe kufanya hivyo kama ambavyo wateja wengi wanafanya! Anyway, labda mashahidi na polisi watathibitisha fedha hizo zilitumika kufanya uhalifu. Ila ikumbukwe, Mbowe hajaanza kujitetea; huenda akabomoa kila aina ya ushahidi unaoelekezwa kwake! Mechi haijaanza, bado ni hatua ya "kupasha misuli".

Leo Mbowe na wenzake walionekana wakicheka mahakamani baada ya shahidi wa Jamhuri kushindwa kutokea; hiyo ni meseji kubwa sana.
Nadhani msingi wa malalamiko ni namna zilivyotolewa.
Kama ulivyosema kwa amri ya mahakama.
 
Kilichoandikwa hakina maana kama kilichofanyika na kilichosemwa na mwakilishi wa sheria wa tigo kiko tofauti,ukweli ni kuwa hata kama mna ugomvi binafsi na askari anaweza kwenda tigo muda wowote apendao na akafanya atakavyo,hii kesi imetufungua macho na masikio kiasi cha kushangaza mno
Sheria ya nchi inaruhusu Law Enforcement Agencies na Court kupewa taarifa yoyote wanayoitaka na wala hawalazimishwi kukueleza sababu ya kutaka taarifa hiyo. Someni sheria mbalimbali acheni kuwa utopolo kwa kila kitu! Hata Tigo hapo wameeleza vizuri. Na hii ni kwa duniani kote. Pia kumbuka Law Enforcement Agencies wanaweza kupata taarifa zako wakati wowote hata kama TIGO asipotaka acheni kupoteza muda kwa kitu ambacho ni obvious!!
 
Ila kusema kweli Tz ubongo wao wa kuchambua mambo ni mdogo sana!!?
They are full of jokes.......
Mamlaka si ndio inatoa leseni ya biashara....
Mlitaka yule shahidi aseme wanatii zaidi wateja kuliko mamlaka!!??
Kwani wewe unatakaje labda?

Sent from my SM-M315F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom