Sera ya faragha MIC Tanzania Public Limited Company - tiGo

Mpangaji mteja .Mwenye nyumba kutoa Siri zako hahitaji kibali Cha mahakama kuzitoa polisi

Laini za simu wewe mpangaji tu waweza wao au TCRA wakiamua wanakuzimia tu
Again, mfano ulioutoa ni irrelevant. Mwenye nyumba hajui ukitoka kwenye nyumba aliyokupangishia, unaenda kuonana na nani, unaenda kumlipa mtu gani, na wala hajui kuhusu miamala yako wala Safari zako. Tumia akili zaidi. Mfano wako ni wa hovyo kama kweli unataka kuutumia ili uweze ku justify upumbavu wa Tigo.
 
Soma vizuri historia za wanaojilipua n sababu zao kwa taarifa tu hawajilipui kama walozi ni baada ya kuwa na imani iliyopotiliza juu ya jambo fulani ( fundamentalist)
 
Ndio upelelezi wa polisi lazima u cooperate Kama customer wako ni mhalifu au jambazi au mhatarisha Usalama wa nchi .No way lazima utoe ushirikiano ndio maana mauaji yakitokea mfano ya Floyd kule Marekani owner wa supermarket alitoa ushahidi wake bila kibali Cha mahakama.

Polisi ni law enforcement agent kukitokea tukio halifu hahitaji kwenda mahakamani kuomba kibali
 
Sawa hapo mwenye nyumba wako ni kampuni ya simu waweza panga nyumba,ukapanga sehemu ingine fremu ya duka na ukapanga sehemu ingine laini ya simu ya Tigo.Hapo mumiliki laini ya Tigo ambaye ni kampuni atamwaga mboga kukuhusu wewe mpangaji wa line

Line sio yako kiuhalisia ni Mali ya kampuni ya Tigo wewe umepangishwa tu
 
Hiyo ndio practice dunia nzima lazima ufanye hivyo hata uwe Marekani au Ulaya compliance lazima

Kazi za kampuni za simu pote duniani sio kutunza Siri za wahalifu na magaidi
Fuatilia! Ni LAZIMA waende mahakamani kupata hicho kibali cha kufanya hivyo. Siyo tu kama ilivyo kwetu ambapo taasisi yoyote ya serikali inaweza kupatiwa information za mteja kama wakitaka. Tena jinsi ilivyokuwa vague. Hata polisi tu anaweza kwenda na kufanya hivyo.

Hilo tatizo lipo hata kwenye mabenki. Na ndiyo maana mwendazake aliweza kuwachungulia wafanyabiashara jinsi anavyotaka!

Unalifahamu neno “fiduciary”?
 
Polisi hwako juu ya sheria, hata hatua zao za kutafuta ushahidi lazima wafuate sheria. Na sheria yenyewe ni lazima wpate kibali cha serikali
 
Sio kweli hata sheria za kimataifa ziko nyingi hazihitaji

Mfano Kuna sheria za kimataifa za money laundering hawahitaji kibali Cha mahakama yeyote duniani kukufuatilia na kupata information

Pia Kuna sheria za ushahidi hawahitaji kwenda mahakamani kumtaka shahidi aje a testify for or against mtuhumiwa bila kujali huyo mtuhumiwa ni customer wa mtuhumiwa au la.
 
Soma vizuri historia za wanaojilipua n sababu zao kwa taarifa tu hawajilipui kama walozi ni baada ya kuwa na imani iliyopotiliza juu ya jambo fulani ( fundamentalist)
Na gaidi wa Tanzania aweza jilipua kwa laki tano kwa misimamo mikali ya kisiasa iliyopitiliza
 
Sheria gani za kimataifa unazungumzia? Ni lazima kuwepo na “warrant” ambayo huwa inatolewa na mahakama. Hata Mbowe walivyoenda kumshachi, ilikuwa ni lazima wawe na “search warrant” ambayo hutolewa na mahakama baada ya mahakama kujiridhisha. Hapa kwetu, kwa mujibu wa Tigo, polisi anaweza kwenda tu na barua ya kutaka information za Mteja...Kwa marekani Soma hapo chini kama unaelewa ukisoma...

“The U.S. Supreme Court ruled that police need a warrant to obtain cellphone location information routinely collected by wireless providers. In a landmark decision, the U.S. Supreme Court ruled Friday that police must obtain a search warrant to access an individual's cellphone location information.”

Source:
.22 Jun 2018

NPR Cookie Consent and Choices › 2018/06/22

 
Polisi hawezi kwenda kuchukua Data bila idhini ya Mahakama?!!....
 
Na gaidi wa Tanzania aweza jilipua kwa laki tano kwa misimamo mikali ya kisiasa iliyopitiliza
Ulishawahi kuona mtu mwenye msimamomkali wa kisialsa uliopitiliza tz? Nenda pwani kawaulize wana CUF ile ya malallim watakwambia maana yake??? Yaani mtu awe na msimamo makali uliopitiliza wa kisiasa Afu alipwe afu atekeleze ugaidi?????
 
Polisi hawezi kwenda kuchukua Data bila idhini ya Mahakama?!!....
Kwa Tanzania naona inawezekana, lakini siyo kwa wenzetu...

Under the Electronic Communications Privacy Act of 1986, law enforcement must obtain a court order under 18 U.S.C. §2703(d) (2703(d) order) to compel a provider to disclose more detailed records about a customer’s or subscriber’s use of services, such as the following:

  1. Account activity logs that reflect what Internet protocol (IP) addresses the subscriber visited over time.
  2. Addresses of others from and to whom the subscriber exchanged e-mail.
  3. Buddy lists. Source:2703(d) order
 

You are very right ndugu dudus...

Kwa nyongeza tu mimi nime notice mambo kadhaa;

1. KWANZA; watu waelewe kuwa hakuna shida kwa mtu aitwaye Freddy Kapala kufanya kazi tiGO kama Mwanasheria au vyovyote vile...

2. PILI, watu hawana shida na mtu aitwaye Freddy Kapala kusimama mahakamani na ku - testify against Freeman Mbowe na wenzake...

3. Watu wana shida na njia iliyotumika kupatikana kwa ushahidi huo ambayo totally ni illegal kwa kumtumia shahidi huyo anayejiita Legal Advisor wa kampuni kubwa ya mawasiliano ya tiGO, bwana Freddy Kapala...

##Na hii ndiyo inayopelekea kila mtu kujiuliza maswali kadhaa ili kujua "nia" ya serikali kwa kuwatumia Polisi ni nini hasa kumfungulia Freeman Mbowe kesi hii iwapo ushahidi tu wa ku - incriminate wanautafuta kwa "tochi" na kwa kutumia njia haramu kinyume kabisa cha kanuni, sheria na katiba ya nchi...!

Mfano;
å Kwa maelezo ya Freddy Kapala mahakamani tunapata picha kuwa, the entire management ya tiGO/MIC Company haikuwa aware kuwa kampuni yao inahusishwa na kesi hii kubwa ya ugaidi kupitia mteja wao mmoja Freeman Mbowe isipokuwa mfanyakazi wao mmoja tu aitwaye Freddy Kapala...!!

å Hivi ilikuwaje barua toka Polisi anaipokea huyu huyu Freddy Kapala, kuifanyia kazi, kuijibu na kusaini na kugonga mihuri yote bila mtu mwingine yeyote ndani ya kampuni kuhusishwa tena jambo lenyewe likihusu UGAIDI...???

å Iliwezekanaje Polisi waindakie tiGO barua kutaka taarifa za mteja fulani (hapa ni Freeman Mbowe) bila kueleza sababu au kosa kisha tiGO kwa ujinga au kwa makusudi kupitia kwa Mwanasheria wao FREDDY KAPALA bila kuhoji mambo ya msingi wakafanya vile...???

å Kwa nini Polisi hawakutumia njia rasmi kupata taarifa au data za wanayemshuku kuwa ni mhalifu na badala yake wanatumia njia ya mlango wa nyuma? Yaani wanataka kuthibitisha fulani ni mhalifu/gaidi lakini wao mwenyewe Polisi wanatumia njia za kihalifu...??

å Kuna uhusiano gani kati ya Freddy Kapala na Polisi..???

HITIMISHO:

##Hii kitu si tu imevunja SERA ya faragha ya kampuni ya tiGO bali imevunja sheria na katiba ya nchi...!!

##Hapa tiGO ili kuepuka legal consequences dhidi ya tendo hili toka kwa mteja wao Freeman Mbowe, wana options 3 tu;

1. Aidha wamkane huyu Freddy kuwa siyo mfanyakazi wao

AU;

2. Ni mfanyakazi wao lakini amefanya yeye binafsi na kwa hiyo ni mhalifu kama wahalifu wa matandao (hachers) wengine wowote duniani

AU;

3. Wakae tayari kumlipa Freeman Mbowe mabilioni kadhaa ya shilingi kwa ku disclose faragha yake kinyume cha sheria!

##Na mwisho, waombe Mungu ithibitike kuwa line ile ya simu iwe siyo ya Freeman Mbowe japo bado Polisi na Freddy Kapala wao wataingia kwenye hatia iwapo walitumia jina la mtu mwingine kusajili line ya simu ili kum - incriminate mtu huyo..!
 
dudus point kubwa hapa ni namna data za mteja zinavyoweza kupatikana. Hili la miamala na utetezi wake wala siyo muhimu. Ni lazima data zipatikane kwa njia sahihi na kusiwe na loopholes zozote za kuweza kutumia ili kwenda kinyume. Malalamiko yametokea kwa sababu imeshakuwa kama utamaduni kwa kampuni za simu kutoa mawasiano ya wateja wao bila sababu za msingi wala njia zinazokubalika.
 
Mkuu umemaliza kila kitu. Umeelezea kisheria lakini kwa lugha ya kueleweka. Big up! NB: Hili jambo ni serious sana na linatakiwa lisiachwe hivi hivi. Ni watu wengi hawataona implication zake sasa hivi na wenye akili wanajua utaratibu ulitomika ni hovyo sana na usipokomeshwa tunakoelekea ni kubaya.
 
Legal Purposes: includes any treatment justified by the need to comply with applicable legal requirements, such as meeting a requirement of a governmental or administrative entity in the exercise of its functions or by order of a competent judicial authority, or to protect the rights, property or safety of Tigo, as well as the safety of our customers, employees and the general public.
 
Kiuhalisia sio Tgo tu! Nakumbuka nliwai pata shida na mtu, polisi walifanya kila kitu kujua mawasiliano yake yooote toka VODACOM....shemeji yangu kipindi flan akapata taarifa zoooote za mkewe toka Tgo na sio kupitia polisi, aliwasliana tu na mtu Tgo akamtoa masenti akamprintia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…