Uchaguzi 2020 Sera ya majimbo itaua utaifa na uzalendo

Mbana hata Sasa maeneo yenye rasilimali nyingi hayana maendeleo Huku dar es Salam ikiwa ndyo unaonekana inaendelea zaidi kwani Ina rasilimali nyingi
 
Geita ilipo chato unajua kuna migodi ya dhahabu mikubwa inayoingizia nchi Mabilioni ya pesa za kigeni ? Au unadhani chato ni singida wanakotegemea mauzo ya alizeti
Singida nasi tutabuni vyanzo vyetu vya mapato, tatamtoza pesa inayolingana na nauli kamili kila abiria anayekatiza Singida kwenda sijui kaskazini, kanda ya ziwa au kuelekea Dom. Mbona tutaombana pooo!
 
Pigia mstari *maeneo yao*! Nikuulize maaeneo ya wasukumu ni wapi? Lakini leo wapo mpaka Lindi hadi katavi japo siyo "maeneo yao*. Nikuulize wachaga maeneo yao ni yapi? Leo tazama wachaga walivyotapakaa nchi nzima. Nikuulize maeneo ya wapemba ni wapi? Leo mpemba yupo Singida analima vitunguu.
Kwa mfumo wa akili za mtz mweusi, ujue fika mtu atakapokosa cha kufanya ndani ya *maeneo yao* hawataweza kutoka nje ya *maeneo yao*, hata walioko nje ya *maeneo yao* watarudishwa kwa lazima kwenye *maeoneo yao*. Tafakari acha ushabiki maandazi.
 
Maeneo yao maana yake ni maeneo waliko wananchi, si makabila. Huko huko walikochanganyika. Swala ni kwamba maamuzi yasifanywe na Rais pekee. Yeye kapigiwa kura, ni halali kufanya maamuzi lakini asihodhi madaraka yote. Lakini mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya, mkurugenzi wa halmashauri, wote hawa wana maamuzi makubwa kwenye 'maeneo yao', na hawachaguliwi wala kuteuliwa na wananchi wa maeneo hayo. Sera ya majimbo pengine CHADEMA wameipa jina linalotisha, lakini ina mantiki kubwa. Tuondoe upotoshaji, tujadili maana yake ya kweli.
 
Sera ya majimbo inakuwa applied sana kwenye nchi zenye eneo kubwa mfano mzuri Marekani,uchina,urusi na india wanatumia huu mfumo hata congo pia kwa mbaali unaona kama wanamajombo lakini kwetu autakuwa na maana ingawaje kwa kenya naona wanao lakini kuongeza gharama tu
 
kuanzisha kanda za uchumi Tanzania hicho ndio kitu bora zaidi kuliko kuanza na kanda za majimbo
 
Hatufanyi upotoshaji, ndo uhalisia wa nchi yetu. Nimekaa Dar, Arusha, Moshi, Mwanza na Mbeya. Mjini watu wanachanganyikana poa tu, ila ukisogea maeneo ya pembezoni kidogo mgeni unabandikwa jina Fulani hivi amazing kuonyesha kuwa siyo wa kwao. Ubaguzi utangezeka maradufu katika mfumo wa majimbo.
 
Singida nasi tutabuni vyanzo vyetu vya mapato, tatamtoza pesa inayolingana na nauli kamili kila abiria anayekatiza Singida kwenda sijui kaskazini, kanda ya ziwa au kuelekea Dom. Mbona tutaombana pooo!
Umenena vyema mkuu ila sera ya majimbo si yakukomoana maana umejuwa na hasira ghafla.
 
Kenya enzi ya KANU ilikuwa nchi ya kijinga kwelikweli ila baada ya mabadiliko ya katiba Kenya unaiona sasa ilipo? Yani khaya mazimwi yoooteee yameondoka sisi tumebaki na hili la CCM tumeling'ang'ania.
Wacha uongo! Baada ya KANU kuondoka madarakani nini kimefanyika kikubwa Kenya zaidi rushwa kuhalalishwa na rasilimali za nchi kushikiliwa na familia chache huku ukabila ukiendelea kutamalaki kila kona? Waliolilia katiba mpya kenya wameipata na shida zipo palepale.
Wananchi maskini wanabaki kusoma hadithi za enzi zile za maziwa ya nyayo tuu

Maendeleo ni action sio blah blah
 
Itakuaje kila jimbo lisimamie rasilimali zake, kila mtu aajiriwe au kufanya biashara kwenye jimbo tuu
Natafakari
Dada ungeomba ueleweshwe majimbo yanafanyaje kazi. Sikiliza clip ya Lissu jana akiwa Kagera
 
Umenena vyema mkuu ila sera ya majimbo si yakukomoana maana umejuwa na hasira ghafla.
Si mnasema Singida tunategemea alizeti tu, ndo nawapa sasa vyanzo vya mapato vyetu. Wana jimbo tutakuwa huru vyanzo vyetu vya mapato na namna ya kutumia mapato hayo. Kama mdau alivyotoa mfano wa majimbo ya Marekani kugomea bomba la mafuta hivyo hivyo Sindiga tutagomea magari mabovu mabovu kukatiza anga zetu kwani yanatuchafulia mazingira. Haya majimbo yaje tu tuoneshane makali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…