Sergio Ramos ashitakiwa mahakamani kwa kumwumiza kwa makusudi Mohammed Salah; kulipa €1bn.

Sergio Ramos ashitakiwa mahakamani kwa kumwumiza kwa makusudi Mohammed Salah; kulipa €1bn.

Wamekosa kazi.

Waarabu wameshapata sababu ya kutolewa mapema WC.
 
Hawa nao hawaishi kulialia..kwani Sarah ni mtume..ile Rafu ni ya kawaida sana sana..Ronaldo De lima aliwahi kuvunjwa serie A msimu mzima akakaa njee, Kina Suarez hadi meno walikuwa wanatumia wakiwa huko huko Liverpool..
 
Vuguvugu la fainali ya UEFA limeendelea kushika kasi hasa kuhusu suala la kuumia kwa mchezaji wa Liverpool; Mohammed Sarah ambaye baadhi wanadai aliumizwa kwa makusudi ili kuhakikisha Real Madrid inaibuka kidedea.

Huko nchini Misri, mmoja wa wanasheria nguli nchini humo aitwaye Bassem Wahba amesema atafungua mashtaka mahakamani dhidi ya bwana Ramos kwa kile anachodai kuwa katika mchezo huo, Sergio Ramos alimwumiza kwa makusudi Mohammed Sarah na kumsababishia maumivu ya kimwili na kisaikolojia yeye sarah na watu wa Misri wote.

Mwanashera huyo amesema pamoja na kupeleka malalamiko rasmi FIFA, Sergio Ramos anastahili kuadhibiwa kwa kitendo hicho. Pia aliongeza kuwa mbali na kudai fidia hiyo ya €1bn, kuna uwezekano kiwango hicho kikaongezeka.

Egyptian lawyer files €1billion lawsuit against Sergio Ramos in Champions League final | Daily Mail Online
wee pia inapaswa ushitakiwe kwa kuharibu jina la bwana Salah kwa kumpachika jinsia ya ke'
 
Vuguvugu la fainali ya UEFA limeendelea kushika kasi hasa kuhusu suala la kuumia kwa mchezaji wa Liverpool; Mohammed Sarah ambaye baadhi wanadai aliumizwa kwa makusudi ili kuhakikisha Real Madrid inaibuka kidedea.

Huko nchini Misri, mmoja wa wanasheria nguli nchini humo aitwaye Bassem Wahba amesema atafungua mashtaka mahakamani dhidi ya bwana Ramos kwa kile anachodai kuwa katika mchezo huo, Sergio Ramos alimwumiza kwa makusudi Mohammed Sarah na kumsababishia maumivu ya kimwili na kisaikolojia yeye (Sarah) na watu wa Misri wote.

Mwanashera huyo amesema pamoja na kupeleka malalamiko rasmi FIFA, Sergio Ramos anastahili kuadhibiwa kwa kitendo hicho. Pia aliongeza kuwa mbali na kudai fidia hiyo ya €1bn, kuna uwezekano kiwango hicho kikaongezeka.

Egyptian lawyer files €1billion lawsuit against Sergio Ramos in Champions League final | Daily Mail Online
Ingependeza zaidi ungejifunza tofauti ya 'L' na 'R'
 
Hivi kwa uhalifu alofanya ramos hawezi kupelekwa the hague kabisa??!!
 
hahahaha Taka taka tupu....kama wanaogopa wachezaji wao kuumia wawashauri wacheze muziki tuu au karata.....
Upuuzi mtupu
 
hakuna kesi za hivyo duniani... huyo hajui lolote
 
Ni hizo za kusuruhisha masuala ya michezo mkuu! Wakienda kwingine Sarah anafungiwa kucheza mpira.
Kesi wafungue wengine kucheza afungiwe salah? Hakuna sheria ya namna hiyo!!

Huyo jamaa anataka kumsababishia Ramos kitu kinaitwa psychological torture , ila madai hayana msingi wowote kisheria na wala kesi haitasiikilizwa.

Ila acha afungue tu, ni muhimu sana.
 
S.ramos alikuwa akifanya kazi yake akiwa katika uwanja wa vita. I wish ningekuwa wakili wake hii kesi tungeshinda 100%
 
Kuna mahakama za mpira mkuu!!
Hiyo suit imefunguliwa egypt. Means ramos atakuwa mtuhumiwa tu atakapo kanyaga ardi ya misri. Otherwise hakuna wa kumkata, na kesi itapotelea hewan na jamaa ataendelea kufunda.
 
Back
Top Bottom