Serikali baada ya kukutana na viongozi wa dini ilitakiwa irudi tena kuwapa mrejesho mapendekezo yao Serikali imefikia wapi

Ukivaa kanzu marekani au Uingereza unafatiliwa wanajua unataka kulipua mahali🤣🤣🤣
 
Rais anatumia mawaziri na wanasheria na ndio maana ya serikali. Ni taasisi pana sio mtu mmoja tu.

Wanasheria wa serikali waliongea kwa kina mbele ya maaskofu tena wale wakubwa na kuuelezea mkataba kwa kirefu kifungu kwa kifungu, na hao maaskofu wakasaini makaratasi kuonyesha kuelewa kile walichoambiwa.

Ni vigumu kujua kitu gani kiliwapata hapo katikati mpaka wakaamua kuja na waraka wa kuupinga uwekezaji na kuamua kuusambaza makanisani, ule ulikuwa ni uamuzi wenye kuwakwaza baadhi ya waumini.

Cha kufikirisha zaidi ni kwamba DPW ni mwekezaji mmoja tu kati ya watatu wanaokwenda kuwekeza katika bandari zetu. Mmoja atapewa magati hapa TPA na mwingine atakabidhiwa bandari ya Bagamoyo.

Na hao wawekezaji wawili watapingwa na maaskofu kama anavyopingwa DPW?. Wametengeneza ugumu wa uhusiano kati yao na serikali kuu kitu ambacho mbele ya safari kinaweza kuumiza utendaji wa taasisi zao pia.
 
Sasa hapo kamaanisha kakubali au kakataa ushauri ..?
 
Kwani serikali inawajibika kwa viongozi wa dini au kwa raia, inawapa je majibu kwani hao ni muhimili?
Wanafata nini makanisani namisikitini kama hawawajibiki huko? dini niimani zawananchi na serikali niyawananchi bado unadhani haiwajibiki kwao? Umewahi jiuliza kwanini Rais muisilamu anaingia kanisani au Rais mkristo kuingia msikitini? wanaenda kwa wananchi waliompa mamlaka yakuongoza haendi kuongoza ibada,,
 
Viongozi wa dini hawawezi kuwapangia serikali kitu cha kufanya halafu wawape na sharti la kuwapa wao mrejesho. Walichokisema ni ushauri ambao sio lazima kwa serikali kufanya kile watakacho wao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…