Serikali baada ya kukutana na viongozi wa dini ilitakiwa irudi tena kuwapa mrejesho mapendekezo yao Serikali imefikia wapi

Serikali baada ya kukutana na viongozi wa dini ilitakiwa irudi tena kuwapa mrejesho mapendekezo yao Serikali imefikia wapi

[emoji15][emoji15][emoji15][emoji1787][emoji1787]

Kumbe unawachukia waarabu...

Wenzako wazungu pamoja na tofauti na hao watu bado hawakuzuia wasiandae fainali za kombe la dunia kule Qatar....

Dunia hii ni ya makubaliano kibiashara....

Eti kwa kuwa mimi mnyakyusa ninazichukia kanzu za waarabu ilihali babu yangu mchungaji Anyigulile Kyala kila misa anazivaa pale Moravian Matema Kyela ,nisitake Tanzania tupate TRILIONI 26 zaidi ya nusu ya bajeti ya juzi ya fiscal year(trilioni 44)[emoji15][emoji15][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Kweli chuki ni ugonjwa wa akili....haya unaye MVAA SUTI aliye na "offer" yenye "kitambi" cha TRILIONI 80?!!! [emoji1787]
Ukivaa kanzu marekani au Uingereza unafatiliwa wanajua unataka kulipua mahali🤣🤣🤣
 
Sidhani hata kama ile kauli kutolewa haikuwacsahihi kabisa

Angetoa tu mrejesho kuwa serikali imefikia wapi kwenye mapendekezo ya wananchi mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini au hata angesema tu tunaendelea kupokea mapendekezo na uchambuzi wa kina unaendelea chini ya wataalamu wetu na wewe baba askofu na wenzio mtuletee tuyafanyie kazi.kama kuna mapendekezo mlisahau kwenye yale mlituletea nk mpeni Baba Askofu atuletee yajumuishwe

Ile lugha aliyotumia Raisi ilikuwa chini ya kiwango haikuhitajika kabisa.
Rais anatumia mawaziri na wanasheria na ndio maana ya serikali. Ni taasisi pana sio mtu mmoja tu.

Wanasheria wa serikali waliongea kwa kina mbele ya maaskofu tena wale wakubwa na kuuelezea mkataba kwa kirefu kifungu kwa kifungu, na hao maaskofu wakasaini makaratasi kuonyesha kuelewa kile walichoambiwa.

Ni vigumu kujua kitu gani kiliwapata hapo katikati mpaka wakaamua kuja na waraka wa kuupinga uwekezaji na kuamua kuusambaza makanisani, ule ulikuwa ni uamuzi wenye kuwakwaza baadhi ya waumini.

Cha kufikirisha zaidi ni kwamba DPW ni mwekezaji mmoja tu kati ya watatu wanaokwenda kuwekeza katika bandari zetu. Mmoja atapewa magati hapa TPA na mwingine atakabidhiwa bandari ya Bagamoyo.

Na hao wawekezaji wawili watapingwa na maaskofu kama anavyopingwa DPW?. Wametengeneza ugumu wa uhusiano kati yao na serikali kuu kitu ambacho mbele ya safari kinaweza kuumiza utendaji wa taasisi zao pia.
 
Nimekuelewa na nimerekebisha. Mama kishasema:

"Nimeyasikia yote uliyoyasema kuhusu usalama, amani, umoja na muendelezo wa taifa letu, niliamua kunyamaza kimya, na naendelea kunyamaza kimya, nachotaka kuwahakikishia hakuna mwenye misuli na ubavu wa kuligawa taifa hili, na hakuna mwenye misuli na ubavu wa kuuza taifa hili, na hakuna mwenye misuli na ubavu wa kuharibu amani na usalama kwenye taifa letu."

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika maadhimisho ya
Miaka 60 ya KKKT.

Unalo jipya au bado hilohilo?
Sasa hapo kamaanisha kakubali au kakataa ushauri ..?
 
Kwani serikali inawajibika kwa viongozi wa dini au kwa raia, inawapa je majibu kwani hao ni muhimili?
Wanafata nini makanisani namisikitini kama hawawajibiki huko? dini niimani zawananchi na serikali niyawananchi bado unadhani haiwajibiki kwao? Umewahi jiuliza kwanini Rais muisilamu anaingia kanisani au Rais mkristo kuingia msikitini? wanaenda kwa wananchi waliompa mamlaka yakuongoza haendi kuongoza ibada,,
 
Viongozi wa dini hawawezi kuwapangia serikali kitu cha kufanya halafu wawape na sharti la kuwapa wao mrejesho. Walichokisema ni ushauri ambao sio lazima kwa serikali kufanya kile watakacho wao
 
Back
Top Bottom