speech
JF-Expert Member
- Mar 4, 2022
- 484
- 1,266
Ni sawa na kiasi gan ?TGHS D1 - FAMASIA
TGHS E1 - DAKTARI
TGHS F1- SPECIALIST
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni sawa na kiasi gan ?TGHS D1 - FAMASIA
TGHS E1 - DAKTARI
TGHS F1- SPECIALIST
ImasikitishaHawajui Walimu ndio msingi wa kila KADA za Nchi hii lakini ndio lowest paid than them all.
Yaan mtu amesoma elimu ya chuo ziadi ya miaka 8.. then anakuja kulipwa ela hyo... ???TGHS D1 1270,000/=
TGHS E1. 1,530,000/=
TGHS F1. 1,865,000/=
Na nashukuru Sana sijutii maamuzi yangu maana nimepata connection kubwa miaka michache baada ya kuacha kazi na nipengine pesa ambayo ningeipata baada ya kustaafu nilipata ndani ya miaka 2Hongera kwa kufanya maamuzi magumu.
Wengi huko UALIMUNI watu wamefugwa na UMASKINI...
Aiseeee [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Na nashukuru Sana sijutii maamuzi yangu maana nimepata connection kubwa miaka michache baada ya kuacha kazi na nipengine pesa ambayo ningeipata baada ya kustaafu nilipata ndani ya miaka 2
Ndio wakina Dr Hamis Kingwangala, Hussein Ali Mwinyi na wengine wengi waliacha kazi za kuchoma watu sindano na kuamua kwenda kwenye siasa kunako lipa zaidi.Yaan mtu amesoma elimu ya chuo ziadi ya miaka 8.. then anakuja kulipwa ela hyo... ???
Kwel ndio maana madactari wengi specialist huamua kufanya kazi nje ya nchi tu
Kuna shule moja hapa ya sekondari wamekomaa kuwa kila mwaka mwanafunzi eti apeleke ream za kufanyia mitihani.Sasa hivi waalimu wakuu shule za msingi wanapata posho ya shiling laki moja kwa mwezi, sidhani kama hawa wanaweza kuungana na wenzao kupiga kelele.
Tatizo linaanzia pale wengi wanaochukuliwa kuwa waalimu ni wale ambao matokeo yao ya kidato cha nne na sita ni udhaifu!
Utaratibu ungebadilishwa uwe kama vyuo vikuu ambavyo huchukua waliofaulu vizuri (cream) tu. Vinginevyo wataendelea kunyanyasika na hawawezi kijinasua kwa kuwa wanafahamu ukweli kuwa wao ni dhaifu katika masomo wanayofundisha!
Tatizo la kada ya Elimu ni WATEJA kuwa maskini(Wanafunzi).
Hawana cha kuwashukuru walimu wao.
Serikali ingewapa hata posho ya laki moja tu monthly..
Au iwape mikopo isiyo na riba.
Upo sahihi 100%Ambacho hujua na pengine mleta mada akuweka sawa sana. Viwango vya mishahara serikalini ni karibu sawa vikiwa na tofauti ya elfu 5 au 10 tu. Na wala CWT sio uchawi wa mishahara. Ualimu unaonekana kwakuwa wao ni Majority, kuwafanya mfano ni Rahisi sana.
Na kingine ni vile walimu hawana chakuiba huko shuleni ndio maana huwaoni kwenye ripoti za CAG.
Maafisa kilimo
Afisa maendeleo
Wahasibu wa serikali
Wanasheria wa serikali
Na wengine wengi
Wanaoajiriwa na Degree ya kwanza wooote wanacheza na laki 7 mpk 750. Kabla ya makato.
Tofauti inakuja kuwa yule muhasibu pale halimashauri mkurugenzi anaweza amka asbh akaitisha kikao cha kazi na wakagawana allowance ya laki moja moja. Kesho akaiba kwa kalamu elfu 50, kesho kutwa akapitisha malipo fulani badhirifu akapata 80 elfu. Ndani ya wiki nje ya mshahara katengeneza 230000/
Yule afisa mifugo kaamka asbh kaingia machinjioni kapewa elfu 30 kugonga mhuri kuridhia mfugo uliochinjwa, kesho tena atapewa 30 elfu na kilo 3 za nyama, wiki nzima atatengeneza 180 elfu nje ya mshahara.
Kule kuna mtendaji wa kijiji yeye mshahara ni mdogo zaidi ya mwalimu wa cheti, lakini pale kwenye kijiji anahonga mihuri tsh 3000, ana kesi za kijiji watu wanapigwa faini za kutosha, kwa wiki anatengeneza laki 2 nje ya mshahara.
Ndugu yangu mwalimu anaenda kazini jumatatu hadi ijumaa, hana hata kitu cha shilling 5 cha kuiba, akikomaa sana atengeneze nyumbani (barafu) ice-cream za maji akauze mia mia ndio arudi nyumbani na sh elfu 2 kama faida.
Shuleni hakunaga semina wala vikao vya allowance. Ukikaa kikao ni matako yako kuumia kwenye bench za shule ndio allowance yako. Huwezi iba chaki [emoji3][emoji3] utamuuzia nani?
Hapo ndipo tofauti ya ualimu na kazi zingine, mleta mada kasema walimu wengi wanatoka familia masikini maana ni masikini tu wanaruhusu watoto wao kusoma ualimu.
Hapa ndipo tunasema "They're poor because they were Poor".
Boss peleka hizo ream, usigombane na Walimu.Kuna shule moja hapa ya sekondari wamekomaa kuwa kila mwaka mwanafunzi eti apeleke ream za kufanyia mitihani.
Yaani karatasi 500 mitihani Mara nne kwa mwaka anazimaliza kweli inamana kila mtihani mtt anajibia karatasi 125 za ream mie nitakuja niende na idadi za karatasi anazojibia
MWL Mama Naa ana hoja, asikilizweAmani iwe juu yenu nyote.
Mwalimu wa Nchi hii nadhani ametengenezewa UMASKINI kuanzia anaajiliwa mpaka anastafu. Kwanza ni watu wanaotoka kaya Maskini bado akiajiliwa anaishi kwenye umaskini akistaafu bado anakutana na KIKOKOTOO.
Mwalimu akiajiriwa anaanza na mshahara wa TGTS D1 (SANAA) 771,000/= na SAYANSI ni 750,000/= na hawa ni wa Degree Moja.
Hapo Mwalimu alipe kodi ya nyumba, Maji , Umeme, asomeshe, Ale, ahudumie familia na wengine ukoo Mzima. Bado mnataka avae apendeze kama kada zingine.
Mwalimu ili apande daraja afikie TGTS E1 basi itamchukua miaka 4 mpaka 5 nayo inategemeana na Rais wa wakati huo. (SIASA).
Hivi ni kwa nini daktari umlipe TGHS D1 (1270000) tofauti ya laki tano na mwalimu wa Degree na yeye ana degree wakati wengine walisoma wote hadi F6?
Walimu ndio nguzo ya Taifa, Taifa bora linatokana na raia wake walioelimika vizuri kwa kuwa na Walimu bora.
HAKUNA WALIMU BORA BILA MASLAHI BORA.
UALIMU ni vile tu umebebwa sana na watoto wa maskini ila SIO kazi ya kufanya.
Mwalimu hana House allowance, hana perdiem, hana extra duty, hana overtime bado awe mtumishi bora, Watu wanafanya bora liende tu.
Serikali waangalieni Walimu kwa jicho la pekee kama mnataka Taifa liwe bora.
Serikali haishindwi kuhudumia vizuri walimu 250,000+ (Msingi 170,000+ na sekondari 89,000+ huku walimu wa masomo ya Sayansi na hisabati wakiwa 23,000+)
Sio haki eti Mwalimu wa Degree kufikia Mshahara wa 1280,000 ambao ni TGTS F1 ni mpaka akae kazini miaka 8 - 10+ BADO TUNATAKA TAIFA LILILOELIMIKA?
INATIA UCHUNGU SANA, WANASIASA MMEJIWEKEA MASLAHI BORA SANA ILA WATUMISHI MKAAMUA KUWAPA KIKOKOTOO.
WATZ NI KWA NINI TUMEKUBALI MBUNGE MIAKA 5 APEWE MILIONI 270+ HALAFU MTUMISHI APEWE MILIONI 40+ KWA MIAKA 30 - 40 YA UTUMISHI?
TAIFA HILI LINA LAANA WALLAH.