Serikali boresheni mishahara ya Walimu wa nchi hii

Serikali boresheni mishahara ya Walimu wa nchi hii

Acha kamba wewe..mtu apate one ya PCB aende ualimu?..si atakuwa kichaa.
Dharau si kitu kizur kabisa Ukizungumzia issue ya Ubongo Wengi wanaofaulu vzuri hutokea familia zenye support nzuri pia, Walim si wajinga ila wamekua na Umaskin toka Majumban mpaka huku serkalin.
 
Nani anaeweza tetea maslahi na haki zake katika wafanyakazi wa nchi hii ukiwaondoa hao walimu? Madaktari? Sio waliogoma wakachukuliwa wanajeshi kwenda kutibu, wengine wakang'olewa kucha bila ganzi? Hii yako sio hoja ni makasiriko tu
Kipindi cha nyuma madaktari walikuwa waanlipwa sawa na walimu...mwaka 2007 wakagoma nchi nzima wakaongezewa asilimia mia ndio gap likaonekana. Huu mgomo wa kungolewa meno ni wa juzi hapo. Kwa hiyo walimu wasitaraji mema bila kutoka jasho.
 
TGHS D1 1270,000/=

TGHS E1. 1,530,000/=

TGHS F1. 1,865,000/=

F1 ni mshahara wa Specialist anaeanza kazi.
Hivi specialist si ana masters duh mbona kiduchu namna hiyo....hata kwa madaktari hiyo bado si mishahara ya maana. Nchi hii kada nyingi watu wanajitolea tu kumbe hela gani hizo Sasa.
 
Hapa umetapika Pumba kaka, unamaanisha DUCE pale hakuna one? Zipo tena zingine nzuri tu ila walilazimika kwenda uko kutokana ba sababu zilizokua nje ya uwezo wao.
Unakosea kulinganisga ufaulu ja mshahara kwa dunia ya leo ambayo kuna MD wana three pale Kairuki na Kampala na wakija kazini wanakunja Pesa sawa na MD wa MUHAS.
Huyo ni shortsighted tu, sa hivi kuna MD wa D nne yaani Biology, Chemistry, Physics na Mathematics. Tena hao wa Diploma na Certificate ndio wengi balaa halafu wanalipwa vizuri tu.

Labla angekuja na hoja kuwa walimu wengi sana ndio mana serikali haijali inajua hata Juma akikataa Mshahara wa 771000 kuna wengine kumi wanautaka huo mshahara tena wengine hata nusu yake.
 
Hivi specialist si ana masters duh mbona kiduchu namna hiyo....hata kwa madaktari hiyo bado si mishahara ya maana. Nchi hii kada nyingi watu wanajitolea tu kumbe hela gani hizo Sasa.
Bora hao wana perdiem, extra duty, overtime, seminar na on Transit hivyo mishahara yao wengi hawaitumii.
 
Kipindi cha nyuma madaktari walikuwa waanlipwa sawa na walimu...mwaka 2007 wakagoma nchi nzima wakaongezewa asilimia mia ndio gap likaonekana. Huu mgomo wa kungolewa meno ni wa juzi hapo. Kwa hiyo walimu wasitaraji mema bila kutoka jasho.
Boss huko UALIMUNI kuna mgomo baridi ambao ndio mbaya zaidi kuliko ule wa kuingia barabarani.

Sema kwa sababu madhara yake HAYAWEZI KUONEKANA KWA HARAKA, LABLA BAADA YA MIAKA 5 AU 10 HUKOO.
 
Kwenye maslahi yao, wale jamaa ni wamoja acha kabisa.
Kama wanashindwa kuishauri au kuikemea serikali kuna maana gani ya kulipwa pesa nyingi bila tija kwa nchi, kuna mbunge anaweza changia mada mpaka ukabaki umeshika kichwa tu, hata hicho kiasi ni kikubwa sana 150,000 itapendeza
 
Tatizo linaanzia pale wengi wanaochukuliwa kuwa waalimu ni wale ambao matokeo yao ya kidato cha nne na sita ni udhaifu!

Utaratibu ungebadilishwa uwe kama vyuo vikuu ambavyo huchukua waliofaulu vizuri (cream) tu. Vinginevyo wataendelea kunyanyasika na hawawezi kijinasua kwa kuwa wanafahamu ukweli kuwa wao ni dhaifu katika masomo wanayofundisha!
Hoja Yako ni nzuri lakini kinachofanya mtu afanye kazi Kwa ufanisi ni mpaka aipende kwanza,serikali haijashawishi watu wanaofaulu vizuri kupenda ualimu.Maslahi duni,mazingira magumu ,wanafunzi mrundikano wa kutosha
 
Sasa hizo ndiyo hoja za kujadiliwa ili elimu na ualimu vipate heshima yake.
 
Sasa hizo ndiyo hoja za kujadiliwa ili elimu na ualimu vipate heshima yake.
Keki ya Taifa igawanywe kwa usawa kila mtu anufaike na Taifa lake sio hawa wanalipwa 6M halafu wengine wanalipwa 600K yaani mara kumi zaidi.

Hata kama hao ni wazalishaji kwa hilo gap Hapana huo ni unyonyaji.
 
Bora hao wana perdiem, extra duty, overtime, seminar na on Transit hivyo mishahara yao wengi hawaitumii.
Ni kweli ila nao wanatoa muda wao ambao wangefanya mambo mengine ambayo huenda yangewapa manufaa zaidi.
 
Boss huko UALIMUNI kuna mgomo baridi ambao ndio mbaya zaidi kuliko ule wa kuingia barabarani.

Sema kwa sababu madhara yake HAYAWEZI KUONEKANA KWA HARAKA, LABLA BAADA YA MIAKA 5 AU 10 HUKOO.
Mgomo baridi huwezi kumuwajibisha mwajiri atimize matakwa yao...ni heri shari kamili muda hausubiri.
 
Thamani ya walimu imekuwa chini sn na watu wengi tena wa hovyo wanawadharau sn hawa watu.Si jambo jema na si baraka kwa taifa.

Yani watu wanapiga mahela huko ya ufisadi ,badala ya kuwepo kwa usimamizi mzuri wa hela ili maslahi ya walimu yawe bora ,lakini imekuwa ni wachache tu ndo wanafaidi na kujilimbikizia.
 
Ualimu ni kada isiyozalisha,yenyewe inatumia tu,huwezi ukalinganisha na hospital,Dr.analipwa posho kutokana na wagonjwa wanalipa Ili wapate huduma,afisa wa tra anashughulikia pesa za serikali Ili walimu wapate salary so afisa wa tra atalipwa vzr.Siku hizi wanaambiwa ualimu ni kazi ya kizalendo,hata kwenye kazi ngumu kama kusahihisha mitihani wanalipwa kidogo huku wakiambiwa wao ndio wazalendo wa nchi hii.
 
Hao walimu sidhani kama serikali au mtu yeyote anawajali leo tarehe 14 april nilikuwa nafuatilia mjadala wa bunge kuanzia saa 10 hadi saa 12:15 jioni kati ya wabunge waliopata nafasi ya kuchangia ni wabunge wawili tu ndio walioongezwa maslahi ya hao walimu hasa tatizo sugu la kutowalipa malimbikizo ya mishahara kwa miaka nenda rudi.Tena waliochangia ni wabunge wa kike yule wa Tunduma na aliyechangia kabla yake .Hongera sana mna uchungu na walimu kwa sababu mna vision ya kujua kwamba mwalimu asiyejaliwa maslahi yake hawezi kunisaidia serikali kuondokana na tatizo la wanafunzi kumaliza la saba bila kujua kusoma na kuandika
 
Kama serikali haitaondokana na mind set ya kwamba maboresho ya elimu yajikite kwenye uboreshaji wa miundombinu tu pasipo kuwajali watekelezaji wa mitaala itachukua muda mrefu sana nchi hii kupata maendeleo kwa sababu hao walimu wana vinyongo mioyoni mwao hata kama hawasemi.Huko shuleni watoto hawajifunzi ipasavyo kwa sababu walimu wamekuwa stressed kwa kutolipwa arrears miaka na miaka
 
Tatizo la Elimu bure ndo Hilo , Serikali itoze Ada kwa wanafunzi then hizo Ada zitumike kuboresha Maisha ya walimu kikwete alikuwa sahihi kuweka Mfumo wa ulipaji wa Ada

Serikali yetu ni masikini Sana Kusema inaweza kutoa Elimu bure then waboreshe na mishahara ya walimu haiwezekani that all
 
Back
Top Bottom