Ambacho hujua na pengine mleta mada akuweka sawa sana. Viwango vya mishahara serikalini ni karibu sawa vikiwa na tofauti ya elfu 5 au 10 tu. Na wala CWT sio uchawi wa mishahara. Ualimu unaonekana kwakuwa wao ni Majority, kuwafanya mfano ni Rahisi sana.
Na kingine ni vile walimu hawana chakuiba huko shuleni ndio maana huwaoni kwenye ripoti za CAG.
Maafisa kilimo
Afisa maendeleo
Wahasibu wa serikali
Wanasheria wa serikali
Na wengine wengi
Wanaoajiriwa na Degree ya kwanza wooote wanacheza na laki 7 mpk 750. Kabla ya makato.
Tofauti inakuja kuwa yule muhasibu pale halimashauri mkurugenzi anaweza amka asbh akaitisha kikao cha kazi na wakagawana allowance ya laki moja moja. Kesho akaiba kwa kalamu elfu 50, kesho kutwa akapitisha malipo fulani badhirifu akapata 80 elfu. Ndani ya wiki nje ya mshahara katengeneza 230000/
Yule afisa mifugo kaamka asbh kaingia machinjioni kapewa elfu 30 kugonga mhuri kuridhia mfugo uliochinjwa, kesho tena atapewa 30 elfu na kilo 3 za nyama, wiki nzima atatengeneza 180 elfu nje ya mshahara.
Kule kuna mtendaji wa kijiji yeye mshahara ni mdogo zaidi ya mwalimu wa cheti, lakini pale kwenye kijiji anahonga mihuri tsh 3000, ana kesi za kijiji watu wanapigwa faini za kutosha, kwa wiki anatengeneza laki 2 nje ya mshahara.
Ndugu yangu mwalimu anaenda kazini jumatatu hadi ijumaa, hana hata kitu cha shilling 5 cha kuiba, akikomaa sana atengeneze nyumbani (barafu) ice-cream za maji akauze mia mia ndio arudi nyumbani na sh elfu 2 kama faida.
Shuleni hakunaga semina wala vikao vya allowance. Ukikaa kikao ni matako yako kuumia kwenye bench za shule ndio allowance yako. Huwezi iba chaki [emoji3][emoji3] utamuuzia nani?
Hapo ndipo tofauti ya ualimu na kazi zingine, mleta mada kasema walimu wengi wanatoka familia masikini maana ni masikini tu wanaruhusu watoto wao kusoma ualimu.
Hapa ndipo tunasema "They're poor because they were Poor".