Huu mchezo kwa Jina 'Aviator' maarufu kindege umekuwa shida kubwa sana kwa vijana hasa watafutaji. Ukiingia kucheza au kuchunguza upande wa charting utaona vijana wanavyoliwa na kulaani huu mchezo ambao umewarudisha nyuma sana kimaendeleo na hata nimesikia kuna jamaa amejiua kwa kuliwa kiasi cha Tsh. Milioni 2,000,000.
Shida yangu kubwa huu mchezo ni wa kitapeli, huwezi kupata hela kamwe, mara nyingi wao (wamiliki) ndio wananufaika.
Sasa kwa kuwa inaingiza vijana kwenye lindi la umaskini ni bora ufutwe watu wabeti kawaida tu kama zamani.
Nawahakikishia baada ya miaka 5 mbele nchi itakuwa na machizi wengi sana waliotokana na kuliwa na huu mchezo ambao upo masaa yote 24, kila dakika, kila sekunde, inashawishi sana halafu hupati kitu. [emoji20] Angalia picha hapo.