Serikali fungieni mchezo wa kubeti wa Aviator (kindege), unamaliza vijana

Serikali fungieni mchezo wa kubeti wa Aviator (kindege), unamaliza vijana

Mimi mkuu kwenye betting ndio nakomaa,kama hapa nishampa England na Italy..huo mchezo aviator hata sijui wanacheza vipi
wanacheza hivi... unaweka hela kwenye hicho kindege, muda unavoenda zinaongezeka kwa kasi ya ajabu ila ndo inatakiwa uzichukue kabla ki ndege hakijasepa, kikiondoka na wewe bado hujachukua ndo unakuwa umelambwa kindege kimesepa na hela zako.
 
Huu mchezo kwa Jina 'Aviator' maarufu kindege umekuwa shida kubwa sana kwa vijana hasa watafutaji ukiingia kucheza au kuchunguza upande wa charting utaona vijana wanavyoliwa na kulaani huu mchezo ambao umewarudisha nyuma sana kimaendeleo na hata nimesikia kuna jamaa amejiua kwa kuliwa kiasi cha tsh/ 2,000,000. Shida yangu kubwa huu mchezo ni wa kitapeli huwezi kupata hela kamwe mara nyingi wao(wamiliki) ndio wananufaika sasa kwa kuwa inaingiza vijana kwenye lindi la umaskini ni bora ufutwe watu wabeti kawaida tu kama zamani .... Nawahakikishia baada ya miaka 5 mbele nchi itakuwa na machizi wengi sana waliotokana na kuliwa na huu mchezo ambao upo masaa yote 24 kila dakika kila sekunde inashawishi sana halafu hupati kitu[emoji20] angalia picha hapoView attachment 3018590
wakifungia aviator kuna super hell zote ni same shit
 
Rekebisha heading, Fungeni sio fungueni!!

Pia nimesikitika kuwa mleta mada Bado unabet, ila unalalamikia kindege!!
 
Wengine tuko makini kwenye ajira zetu

1718545950453.png
 
Dunia imeanza kuniacha.. michezo inahit mpaka inalalamikiwa na sijawahi hata kuiskia.. smh
 
Mh,hadi vitu vya kijinga mnataka Serikali iingilie kati.

Mhusika anaenda mwenyewe,hela yake mwenyewe.
Na isitoshe,lengo ni kupata pesa.
Na vp wakishinda Huwa mnakuja humu pia kutujuza🤔.

Acheni hayo mambo aise.
Kila mtu atimize akili zake,madamu hujashikiwa fimbo.
 
Aliyekuambia huwezi kupata hela ninani. Operators wanasema mchezo wa Aviator kwao sio kwaajili ya kutoa faida Bali kuvutia wateja. Maana una returns kubwa kuliko michezo mingine yeyote
Na wewe ukawaamini!!?
 
Nashukuru kuna mambo yananipita hata siyajui na sitaki kuyajua
 
Shuleni walipokuwa wanafundisha hesabu za probability walikuwa wanasema "Nitazitumia wapi" leo ndiyo mabingwa wa kucheza aviator. Ni mwendo wa kuliwa tu.
 
Aviator inalipa ada, inalipa kodo, inalipa gharama za kula bata weekend we unayetaka ifungiwe jiangalie vizuri
 
Huu mchezo kwa Jina 'Aviator' maarufu kindege umekuwa shida kubwa sana kwa vijana hasa watafutaji. Ukiingia kucheza au kuchunguza upande wa charting utaona vijana wanavyoliwa na kulaani huu mchezo ambao umewarudisha nyuma sana kimaendeleo na hata nimesikia kuna jamaa amejiua kwa kuliwa kiasi cha Tsh. Milioni 2,000,000.

Shida yangu kubwa huu mchezo ni wa kitapeli, huwezi kupata hela kamwe, mara nyingi wao (wamiliki) ndio wananufaika.

Sasa kwa kuwa inaingiza vijana kwenye lindi la umaskini ni bora ufutwe watu wabeti kawaida tu kama zamani.

Nawahakikishia baada ya miaka 5 mbele nchi itakuwa na machizi wengi sana waliotokana na kuliwa na huu mchezo ambao upo masaa yote 24, kila dakika, kila sekunde, inashawishi sana halafu hupati kitu. [emoji20] Angalia picha hapo.


Hadi sasa kuna vijana 7, nawachukulia kama wadogo zangu hapa mtaani.
Walikuwa wakielezana kuhusu huo mchezo wa aviator.
Niliamua kuwapa somo, niliwaeleza kwa fact kuwa aviator ni utapeli wa wazi.
Sina uhakika kama ni kweli wameacha, ila walinielewa na kuahidi kuacha.

Ni bora ubet kati ya Man City Vs Man United nani atashinda.
 
Kah! hao vijana hawajitambui? mpaka kila kitu ni serikali tu, waswahili wanasema serikali ya mtu ni kichwa chake, umeliwa siku ya kwanza, unaliwa tena na unaendelea kuliwa upo tu? kah!
 
 
Back
Top Bottom