Serikali iache kunyanyasa watumishi, Mfumo wa PEPMIS hauna uhusiano na mshahara wa Mtumishi alioufanyia kazi mwezi mzima

Serikali iache kunyanyasa watumishi, Mfumo wa PEPMIS hauna uhusiano na mshahara wa Mtumishi alioufanyia kazi mwezi mzima

Hivi ile mikaratasi inaitwa OPRAS Bado inatumika.haha
Hiyo ndo imeondoka na sasa kuna hii mpya anayoizungumzia mleta mada. Hiyo OPRAS ilikuwa mzigo mzito Sana. Nakumbuka enzi hizo ukiwa boss unakaa na mfanyakazi ambaye wewe unatathmini utendani kazi wake na kumpatia alama kwa kila kigezo kinachohitajika . Pia ilitakiwa mkubaliane naye kuhusu alama ulizompatia. Tatizo ni pale unapompatia alama za chini, yaani hamtaelewana kabisa, na inatishia maisha yako kama boss. OPRAS ilikuwa ni open yaani uwazi zaidi. Ilikuwa na idadi kubwa sana ya karatasi za kujaza kwa kumtathmini mtu mmoja. Kabla ya mfumo wa OPRAS boss alikuwa anajifungia ofisini kwake na kuweka alama pasipo mhusika kujua nini kaandikiwa.
 
Mbaya zaidi kwanzia boss hadi subordinates wa chini kabisa walikuwa hawajui kuzijaza.
 
Mbaya zaidi kwanzia boss hadi subordinates wa chini kabisa walikuwa hawajui kuzijaza.
Tulipewa semina lakini somo lilikuwa halipandi. Ni wachache Sana walielewa na hao pia hawakuweza kufikisha ujumbe kwa wenzao. Ilikuwa inachukua muda mwingi sana kuijaza kwa mtu mmoja. Sasa fikiria una watu 100 chini yako, ilikuwa kazi kwelikweli.
 
Hii nchi ina shida kubwa sana hasa uwezo wa baadhi ya viongozi kuchambua mambo kwa kina , nahisi watu wenye uwezo wa kuchambua mambo kwa kina wananyimwa nafasi au huenda hawapo hiko juu maana jambo kama hili lili hitaji maandalizi makubwa sana ya kimiundombinu kwanza , kuandaa wahusika watakao tumia huo mfumo maana kuna watu hawajawahi kutumia wala kununua hizo smartphone maana sio takwa la mkataba wa kazi na pia kutokana na aina ya mazingira wanayo fanyia kazi sasa unamsimamishiaje mshahara mtu huyo wakati majukumu yake ya kiutendaji yaliyopo kwenye mkataba wake wa kazi kayatekeleza na anasubiri ujira wake.?
Serikali inatakiwa ikianzisha hii mifumo yao, itoe elimu na muda wa kutosha kwa wahusika kujifunza na kuelewa.

Ila shida iliyopo kwa aina ya viongozi tulio nao, ni tabia yao ya kupenda kukurupuka na pia kulazimisha mambo yaende kwa haraka! Hata kama hakuna elimu kwa walengwa.

Hawa watu mwaka wa jana wamewasumbua sana wafanyabiashara na mfumo wa tausi! Na kwao mambo yalikuwa hivi hivi! Mtu unaenda ku re new leseni ya biashara, unaambiwa ukalipie kwa mfumo mpya, na ambao hata huujui!
 
Kazi kwelikweli
Hata hao waliojaza na kukamilisha taarifa zao, watumishi 7 kati ya watumishi 10 hawajui kuutumia huo mfumo.
Serikali inachotaka ni kujaza,kujaza ,kujaza😝😝😝😝
Enzi hizo tukijaza OPRAS kwa kutumia karatasi na kalamu ilikuwa kasheshe. Sasa ongeza hili la kutumia mfumo si ndio mvurugano kabisa. Si wote wana uelewa wa kujaza kwenye mitandao, sijui kama hilo waliliona hao waliotengeneza hiyo mifumo.
 
Nashindwa kuelewa hawa viongozi huwa wana tumia akili gani katika maamuzi yao.

Msidhani kila mtu anaishi mtumba hapo dodoma muwe mnafanya tafiti za kina kabla ya kuleta hiyo mifumo yenu kwanza.

Mfumo wenu unahitaji angalau 3G au H+ Internet speed ili angalau ufanye vizuri wakati huo kuna watumishi wapo vijijini huko ambako hadi leo wanapata internet yenye kasi ya GPRS na EDGE (hilo nina uhakika nalo na ushahidi ninao).

Msitumie ubabe kwenye hili mtatesa watumishi sana, mfumo bado una shida na si rafiki kwa mazingira yetu mnalazimisha nchi kuingia kwenye teknolojia ambazo ki msingi si rafiki kwa kwa aina ya watu na miundo mbinu kifupi hamjawaandaa watumiaji wala miundo mbinu.

Mtumishi ataesimamishiwa mshahara wake alio utumikia mwezi mzima kutokana na majukumu yake kwa mujibu wa makataba wake wa kazi kwa kisa hajajiunga na PEPMIS anione PM kwa masaada wa kisheria.
Kweli ukiwa mjini unaweza kuhisi mtandao upo vizuri tu kila sehemu, bwana sio kweli tembea uone. Kuna sehemu nilikuwa wiki iliyopita tena maarufu tu kuna Shule, hospitali ila hakuna mtandao. Unatuma sms unahangaika iende karibu dk 10. Hii PEPMIS tutaona mengi. Watumishi poleni PEPMIS, Sukari, Petrol,
 
Kuna mfumo wa manunuzi (nest) huo ndo majangaa sasa manunuzi ya serikali hayafanyiki kisa kuingiza mfumo bila kutoa muda watu wafundishwe wao wanalazimisha mfumo.matokeo yake huduma serikalini ni kama zimesima nakwambia hii nchii itapotea kama hamtakuwa makini kuna watu wengi wameingizwa serikalini hawana uwezo wa kufikiria kabisaa.
 
Na sisi wakulima mbona tunasahaulika tunataka na sisi mfumo wetu waziri tusaidie tuna nyanyasika.
 
Msitumie ubabe kwenye hili mtatesa watumishi sana, mfumo bado una shida na si rafiki kwa mazingira yetu mnalazimisha nchi kuingia kwenye teknolojia ambazo ki msingi si rafiki kwa kwa aina ya watu na miundo mbinu kifupi hamjawaandaa watumiaji wala miundo mbinu.

Mtumishi ataesimamishiwa mshahara wake alio utumikia mwezi mzima kutokana na majukumu yake kwa mujibu wa makataba wake wa kazi kwa kisa hajajiunga na PEPMIS anione PM kwa masaada wa kisheria.
Wenye mamlaka wapumbavu sana, fikiria tu mshahara wenyewe mkia wa mbuzi halafu uutumie kuhangaika na huo upumbavu wao, maisha yenyewe gharama juu, wanadhani kila mfanyakazi ana maisha mazuri kama wao, hawajui kuna watu hawana hata 500 ya vocha
 
kuna watu hawajawahi kutumia wala kununua hizo smartphone maana sio takwa la mkataba wa kazi na pia kutokana na aina ya mazingira wanayo fanyia kazi sasa unamsimamishiaje mshahara mtu huyo wakati majukumu yake ya kiutendaji yaliyopo kwenye mkataba wake wa kazi kayatekeleza na anasubiri ujira wake.?
Imagine kuna wapishi, walinzi nk kwenye vyuo na mashule huko wanahangaika wiki mbili nzima kukimbia kwenye cyber cafes spending lots of cash kwaajili ya mfumo, serikali itoe fedha za kumuwezesha kila mtumishi kuwa na smartphone, fedha ya bundle na mafunzo, iache uhuni na ujinga
 
#HABARI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amemuelekeza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Juma Mkomi kusimamisha mishahara ya viongozi walioshindwa kuwasimamia watumishi wao kujisajili na kujaza mipango kazi yao katika Mfumo wa Usimamizi wa Utendaji Kazi kwa Watumishi wa Umma na Taasisi za Umma (PEPMIS/PIPMIS) na kukwamisha utekelezaji wa zoezi hilo lenye masilahi mapana katika utumishi wa umma na taifa kwa ujumla.

Mhe. Simbachawene ametoa maelekezo hayo leo mkoani Iringa alipokuwa akizungumza na Wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi katika Utumishi wa Umma Tanzania Bara wakati akifungua Baraza hilo.

Amesema ujenzi wa mfumo wa PEPMIS/PIPMIS pamoja na mifumo mingine ya TEHAMA ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amedhamiria kwa dhati kuwa na Serikali ya kidijitali itakayorahisisha utendaji kazi wa watumishi wa umma kwa lengo la kutoa huduma bora kwa wananchi.

Vilevile, amekemea tabia ya baadhi ya Waajiri kukataa kuwapokea watumishi wanaohamishiwa kwenye taasisi wanazoziongoza na baadhi kutoruhusu watumishi kuhama hata pale inapoelekezwa na Mamlaka kwani kwa kufanya hivyo ni ukosefu wa maadili na ni jambo ambalo halikubaliki.

Katibu Mkuu-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza hilo amesema elimu ya utekelezaji wa Mifumo ya TEHAMA ikiwemo Mfumo wa PEPMIS/PIPMIS na Mfumo wa Kubaini Mahitaji ya Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma (HR Assessment) imetolewa nchi nzima lakini kumekuwa na kutowajibika kwa baadhi ya viongozi katika kuwasimamia watumishi wao kutekeleza zoezi hilo. #EastAfricaTV
 
Kuna mfumo wa manunuzi (nest) huo ndo majangaa sasa manunuzi ya serikali hayafanyiki kisa kuingiza mfumo bila kutoa muda watu wafundishwe wao wanalazimisha mfumo.matokeo yake huduma serikalini ni kama zimesima nakwambia hii nchii itapotea kama hamtakuwa makini kuna watu wengi wameingizwa serikalini hawana uwezo wa kufikiria kabisaa.
Hatari Sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika Taifa hili hakuna ujinga tunaofanya kama kiwahi technology wakati bado tuna mambo ya kawaida kabisa hatujayaweka sawa...
Ambayo yapo kwenye Haya mambo matatu UJINGA UMASIKINI MARADHI na kwa miaka hii limeongezeka hili la RUSHWA NA UFISADI....

Tungeshughulika na hayo mambo kwanza kwa kweli tungetengeneza taifa imara sanaa

Ni ujinga kudeal na mfumo wakati kuna shule hazina hata matundu ya choo na wanakaa chini

Ni umasikini kumlazimisha mtumishi kujisajir kwenye huu ujinga ukiwa kiwango chake cha mshahara ni 370000

Sio busara kukurupuka na mamifumo kama Haya yanayokula pesa ndefu ikiwa huduma zetu za afya zipo chini sanaaa ambapo mgonjwa anakufa kwenye hosptal ya serikali na mwili unazuiliwa

Ni upuuzi kabisa kukurupuka mavitu kama Haya ikiwa Taifa bado Lina majitu yanajilimbikizia mali nakuiba kila siku na wananchi kunyanyasika pasipo ata huyo mtumishi kuwekewa mazingira mazuri ya kazi na kulindiwa haki zake zenye maslah
 
Back
Top Bottom