Serikali iache kutujazia tozo kufidia matanuzi yao

Serikali iache kutujazia tozo kufidia matanuzi yao

Mimi napendekeza Posho za wafanyalkazi zijumlishwe kwenye Mishahara; ili mishahara iwe na uhalisia. Hakuna haja ya kumlipa mfanyakazi wa umma mshahara wa 1.2m wakati mwisho wa mwezi anakuwa amejipatia 3 to 5M kupitia Posho. Hapa tunapoteza Billions.
 
Wanatufanya kama manamba kila siku kodi tozo.....
Mwigulu na Dr. Phillipo Mpango, ni sawa na duniani na mbinguni!
Mwenzake alikuwa na ubunifu! Na hakuumiza kabisa wananchi wa kipato cha chini! Yeye hamna kitu!

Bora hata angehudumu kwenye Wizara ya Mazingira na Muungano huko. Ila siyo kwenye hii Wizara nyeti ya Fedha na Mipango.
 
Heshima sana wanajamvi,

Sote tumesikia hotuba ya Waziri wa Fedha. Kama kawaida ni mwendo wa kuturundikia kodi na tozo mbali mbali.

Hakuna serekali duniani inayoweza kujiendesha bila kodi.

Kwa upande wa Serekali yetu kuanzia Mkuu wa nchi, Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi & Makamishna wamekuwa wakiishi maisha ya anasa ungedhani nchi ina maana uchumi mkubwa labda kama Canada au Germany.

Last time nilishuhudia msafara wa Rais ukiwa na magari ya fahari zaidi ya 30 huku angani helicopter ikizurura ungefikiri labda tuko Ukraine.

Juzi nilishangaa msafara wa Naibu Waziri sijui ni maji au nini ukiwaumeambatana na zaidi ya magari 13 na vimulimuli vya police 👮‍♀️.

Haya ni matumizi mabaya ya fedha za umma (Kodi)Kwahakika hata tulipe kodi kwa kiwango gani maendeleo ya nchi yataendelea kusua sua kwasababu fedha nyingi zinatumika kugharamia magari ya anasa, mishahara minono kwa viongozi wachache,posho ambazo haziendani na hali halisi ya maisha ya waTanzania, mifumo duni ya kuzuia matumizi mabaya ya fedha za umma.

Ni wakati muafaka serekali ikafikiria kuachana na matumizi mabaya ya kodi za wananchi. Badala ya kila mara kutubandikia kodi na tozo ambazo zingeweza kupungua kama matumizi mabaya, Wizi na ufisadi ingekuwa ni ajenda muhimu.

Matumizi mabaya yamekithiri wananchi tumechoka kulipishwa kodi kugharamia starehe za viongozi.
Mods unganisha huu Uzi,tayari upo humu.
 
Wewe umetafuta nini ambacho hukioni? Huwa ukitoka kwako una drive kwenye barabara alizojenga baba yako?

Ukiugua huwa unaenda kwenye hospital kutibiwa na madakatari ambao mama yako anawalipa au?

Nadhani akili yako inatosha kwenda na kurudi chooni tuu.
Ni lini huyo hawala yako alijenga hizo barabara!!?? acha uzwazwa kenge wewe
 

Attachments

  • Screenshot_20220615-121329.png
    Screenshot_20220615-121329.png
    161.6 KB · Views: 4
Huko USA na UK nchi zinaendeshwa kwa tozo hizi hizi. Tulia tu kuwa mpole na kuwa raia mtiifu kwa serikali yake.
Ila tozo zao huko hakuna watu wanagawana kama peremende. Huku tozo zinakusanywa halafu zinadokolewa na wakurugenzi mpaka boss wao mkuu.

Ujinga kama huu huwezi kuusikia marekani. Mtu analipwa mshahara mzuri lakini bado mwizi. Halikubaliki
 
Ila tozo zao huko hakuna watu wanagawana kama peremende. Huku tozo zinakusanywa halafu zinadokolewa na wakurugenzi mpaka boss wao mkuu.

Ujinga kama huu huwezi kuusikia marekani. Mtu analipwa mshahara mzuri lakini bado mwizi. Halikubaliki
Huku wizi unaanzia juu kushuka chini
 
Tatizo tulipe kodi, tulipe tozo kila aina, then hela zetu ziibwe, zitumiwe hovyo. Tatizo ndiyo hapo.
Unaskia jamaa wanajenga ma Apartments ulaya huko kwa kupitia hela wanazodokoa huku kwetu ambazo ndio hizo tozo.
 
Back
Top Bottom