Serikali iache kutujazia tozo kufidia matanuzi yao

Serikali iache kutujazia tozo kufidia matanuzi yao

Mbona mkoloni hakuendesha nchi kwa kodi na alifanya makubwa Sana ambayo ccm itawabidi miaka elf moja waweze yafikia
Una uhakika wa unayoyasema? Unadhani mzungu atakuwacha kwa chochote kukwepa kodi kiulaini laini kama katika nchi hii?

Na ile kodi maarufu ya kichwa ilikuwa kwa ajili ya nini?
 
Hivi huwa mnafikilia kwa kutumia nini utafananiasha USA kimaendeleo na Tanzania yaani hii Nchi hata iwe na tozo 1000000 kamwe hakutokuwa na maendeleo.
Maisha ni magumu dunia nzima mkuu, ni nyakati ambazo covid19 imetoka kusumbua kila kona ya ulimwengu usitegemee masuala kuwa mazuri kama tunavyodanganyana.
 
US na UK wanalipa tozo ila kinachofanyika kinaonekana, sio Tanzania kuna tozo kinachofanyika kinaonekana na Mafisadi tu.
Tembea huko mikoani uone mahospitali na mashule yanavyojengwa kama uyoga. Toka hapo ulipo uyaone maisha halisi ili uondokane na dhana za kufikirika.
 
Una uhakika wa unayoyasema? Unadhani mzungu atakuwacha kwa chochote kukwepa kodi kiulaini laini kama katika nchi hii?

Na ile kodi maarufu ya kichwa ilikuwa kwa ajili ya nini?
Ile kodi ya kichwa ilikuwa ni kwa ajili ya kumkeep busy mwafrika awe na utamaduni wa kufanya Kazi.
 
Mkuu bado deni letu ni stahimilivu na tunakopeshekaaa!!!

Acha uoga..we ishi tuu!
 
Ila hawa waOman nafikiri kwa vile ni ndugu zetu wa damu kabisa...huenda wakaleta uwepesi.
 
Hii tabia ya wana siasa kusema uongo mfululizo ikiachwa iote mizizi bila kukemewa inaweza kuja kuleta maafa makubwa sana kwa taifa kwa kupandikiza chuki ndani ya jamii na kujikuta watanzania wazalendo wanawekwa pembeni na mafisadi ndiyo yanashika usukani wa kuongoza nchi yetu.
Mmisionari aliyeanzisha Radio Tumaini wakati anaondoka Tanzania kurudi kwao, alisema ni vigumu sana kumpata mtanzania mwaminifu. Miaka ile niliona kama anatutusi watanzania, lakini baadaye nilikuja kukubaliana naye.

Tumegeuka kuwa jumuia ya majambazi huku uraiani, serikalini na hata kwenye taasisi za kidini kama makanisani na misikitini.

Leo hii ukipewa nafasi kusimamia taasisi yoyote; iwe ya kiseikali au ya kidini, ukaifanya kazi yako kwa uaminifu bila kuiba utachekwa hata na familia yako kuwa huna akili.

Hizi kauli za kula kwa urefu wa kamba yako hazitoki kwa bahati mbaya.
 
Wanatia hasira sana. Kila siku utasikia wamesain mikataba ya mikopo kibao!! lkn hio mikopo haionekani inafanya shughuli gani hasa. Hata mawaziri husika hawatu-update nini kinaendelea kwenye hayo mamikopo na miradi wanayosema!! watz tumekuwa wajinga sana!!
Na hela wanazochapisha huwa zinaishia wapi? Ukichanganya na hizo si ni hela nyingi?
 
Huko USA na UK nchi zinaendeshwa kwa tozo hizi hizi. Tulia tu kuwa mpole na kuwa raia mtiifu kwa serikali yake.
Ni kweli lakini angalau mambo yanafanyika unayaona. Siyo huku kwetu wengi mnakamuliwa halafu hela zinaliwa na wachache. Ripoti ya CAG inatoka watu wameiba waziwazi. Na wanajulikana lakini hawafanywi cho chote. Na hiyo ni just tip if the iceberg. Mkilalamika mnaambiwa eti hamieni Burundi. Kiburi na kutojali.

Shithole country [emoji706][emoji706][emoji706][emoji706]
 
Hivi huwa mnafikilia kwa kutumia nini utafananiasha USA kimaendeleo na Tanzania yaani hii Nchi hata iwe na tozo 1000000 kamwe hakutokuwa na maendeleo.
Umeandika kwa hisia sana mpendwa dah!

Shida yetu ubinafsi. Watu wanakuwa mabilionea kwa kuiba hela za umma. Hata ubinadamu hakuna yaani. Shida yetu watu weusi masikini sijui ni nini yaani!
 
Back
Top Bottom