Serikali iache kutujazia tozo kufidia matanuzi yao

Serikali iache kutujazia tozo kufidia matanuzi yao

Hizi shida zote zipo mikononi mwa Wananchi ambao ndio wenye nchi, wakiamua zitaisha ila kwasasa bado hawajaamua na sijui kama wataamua lini.
 
Ilikuwa ni kwa kumzoesha utamaduni wa kulipa kodi kwa ajili ya maendeleo yake.
Mambo yote makubwa waliyotufanyia wakoloni yangewezeka kwa kodi ya shilingi hizo mbili.
Maendeleo yote waliyotuletea wakoloni yametokana na pesa ya sekta moja tu ya kilimo,leo tuna sekta zaidi ya kumi lakini hata kufuta tu nyumba za nyasi vijijini tumeshindwa.
 
Umeandika kwa hisia sana mpendwa dah!

Shida yetu ubinafsi. Watu wanakuwa mabilionea kwa kuiba hela za umma. Hata ubinadamu hakuna yaani. Shida yetu watu weusi masikini sijui ni nini yaani!
Yaani wanafananisha na Nchi ambayo inaongozwa kwa sheria nzuri kiasi kwamba kiongozi hawezi kuiba mali ya Umma na maendeleo yanaonekana.
 
We mjinga sana. Heri hata upate Tozo Lakini sio kukaribisha machafuko. Hatutatoka huko. Nchi yetu bado maskini sana. Tukianza watatupa silaha. Then watavuna Mali zao na wewe na watoto wako hamtakuwa salama.
Heri kukosa wote mkuu.

Naunga mkono hoja
 
Shida sio kodi, mbona tunalipa kodi tena vizuri tu. Tatizo ni TOZO! Unalipa kodi, kitu kile kile unapigwa tozo, that hurts.
Tatizo ni Yule mchumi muumini wa toza anaamini KILA mtza anakula milo 7 kwa siku,
 
Yaani wanafananisha na Nchi ambayo inaongozwa kwa sheria nzuri kiasi kwamba kiongozi hawezi kuiba mali ya Umma na maendeleo yanaonekana.
Ni wakali sana kwa rushwa hizi za kinyama. Yaani ukigundulika ulichoiba utakirudisha, jela utaenda na baya zaidi ni aibu kwa jina lako na legacy yako na ukoo mzima. Na mambo yao kweli yanaenda tena kwa utaratibu mno.

Sisi bado hata ule utu tu hakuna. Mtu unaiba hela za kununulia madawa hospitalini na unaona watu wanakufa kwa kukosa dawa lakini bado unajiona mjanja kwa vile umetajirika umejenga majumba na unaendesha Range Rover. Hata nafsi haikusuti.

Wala sometimes huwa sishangai tukitupiwa maganda ya ndizi. Bado tuna tatizo mahali!
 
Ni kweli lakini angalau mambo yanafanyika unayaona. Siyo huku kwetu wengi mnakamuliwa halafu hela zinaliwa na wachache. Ripoti ya CAG inatoka watu wameiba waziwazi. Na wanajulikana lakini hawafanywi cho chote. Na hiyo ni just tip if the iceberg. Mkilalamika mnaambiwa eti hamieni Burundi. Kiburi na kutojali.

Shithole country [emoji706][emoji706][emoji706][emoji706]
Naenda katazame huduma mahospitalini zinavyoboreshwa ndio utaiona kodi yako ikitumika.

Tazama nchi inavyofikika kila mara kwa ujenzi wa barabara na madaraja, ni kodi yetu hiyo.

Mengi yanafanyika wakati huu tukiwa tunaongea, lakini hatuna utaratibu wa kupima kwa kuweka usawa kila tunachojadili.
 
Naenda katazame huduma mahospitalini zinavyoboreshwa ndio utaiona kodi yako ikitumika.

Tazama nchi inavyofikika kila mara kwa ujenzi wa barabara na madaraja, ni kodi yetu hiyo.

Mengi yanafanyika wakati huu tukiwa tunaongea, lakini hatuna utaratibu wa kupima kwa kuweka usawa kila tunachojadili.
Mwe hospital zipi hizo mkuu?
 
Naenda katazame huduma mahospitalini zinavyoboreshwa ndio utaiona kodi yako ikitumika.

Tazama nchi inavyofikika kila mara kwa ujenzi wa barabara na madaraja, ni kodi yetu hiyo.

Mengi yanafanyika wakati huu tukiwa tunaongea, lakini hatuna utaratibu wa kupima kwa kuweka usawa kila tunachojadili.
Wewe najua uko huko juu unalamba asali. Hata hujui hali ilivyo huku vijijini Misungwi. Lamba sana tena sana angalia tu isikupalie maana kupaliwa na asali ni hatari!

Ningependa kuona ripoti ya CAG ikitoka isiwe na ulambaji ule wa asali. Na cha muhimu zaidi walamba asali wote angalau warudishe walicholamba hata kama wasipoenda gerezani ni sawa. Mabilioni tunayopoteza katika rushwa yanatosha kabisa kutuondolea kero nyingi sana kwa watu wetu. Badala yake tunazidi kuwarundikia tozo na kodi [emoji706][emoji706][emoji706]

Lakini kwa mtu kama wewe mtetezi wa system huwezi kuona!

[emoji3591][emoji3591][emoji3591] Imagine mfano ujinga kama huu hapa chini. Aliyeenda kununua hii mitumba ya mabehewa si yupo? Amepiga billion ngapi kwa utopolo huu? Mbona asikamatwe na kurudisha pesa zetu?

Badala yake mnakimbilia kuongeza tozo na kodi.

Mnakera!
Screenshot_20220614-071433_Gallery.jpg
 
Sasa hivi ndio unaona mambo hayaendi sawa?.Huu sio muda wakulalamika maana wako waliolalamika toka mda mrefu ila miongoni mwetu tukawa tunawazidhaki kwa kauli za kejeli.Hii nchi kwa sasa watu wanatoa mawazo yao kwakuangalia upande wake unavyomnufaisha sio jinsi nchi itakavyonufaika.ila yanayoendelea yanatuumiza wote bila kujali nasaba.Hila haya yote ni matokeo ya chama kinachoongoza serikali kushindwa.Nchi imeshindwa kutumia rasilimali zake sawa sawa tumebaki kua watazamaji uku wengi wakiumia wachache wakinufaika.Ila nyakati zinaonyesha muda sio mrefu kutafanyika mapinduzi makubwa ya historia.
 
Heshima sana wanajamvi,

Sote tumesikia hotuba ya Waziri wa Fedha. Kama kawaida ni mwendo wa kuturundikia kodi na tozo mbali mbali.

Hakuna serekali duniani inayoweza kujiendesha bila kodi.

Kwa upande wa Serekali yetu kuanzia Mkuu wa nchi, Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi & Makamishna wamekuwa wakiishi maisha ya anasa ungedhani nchi ina maana uchumi mkubwa labda kama Canada au Germany.

Last time nilishuhudia msafara wa Rais ukiwa na magari ya fahari zaidi ya 30 huku angani helicopter ikizurura ungefikiri labda tuko Ukraine.

Juzi nilishangaa msafara wa Naibu Waziri sijui ni maji au nini ukiwaumeambatana na zaidi ya magari 13 na vimulimuli vya police 👮‍♀️.

Haya ni matumizi mabaya ya fedha za umma (Kodi)Kwahakika hata tulipe kodi kwa kiwango gani maendeleo ya nchi yataendelea kusua sua kwasababu fedha nyingi zinatumika kugharamia magari ya anasa, mishahara minono kwa viongozi wachache,posho ambazo haziendani na hali halisi ya maisha ya waTanzania, mifumo duni ya kuzuia matumizi mabaya ya fedha za umma.

Ni wakati muafaka serekali ikafikiria kuachana na matumizi mabaya ya kodi za wananchi. Badala ya kila mara kutubandikia kodi na tozo ambazo zingeweza kupungua kama matumizi mabaya, Wizi na ufisadi ingekuwa ni ajenda muhimu.

Matumizi mabaya yamekithiri wananchi tumechoka kulipishwa kodi kugharamia starehe za viongozi.
 
Tatizo wanatuona sisi ni ng'ombe. Siku ya kuwatoa madarakani kwa njia yoyote ile, nadhani hawataamini.
 
Nyie mataga hamuaminiki .
Mnamisi nchi kuendeshwe kimabavu tu, hamna lolote jipya.
 
Back
Top Bottom