Serikali iache mzaha; kuruhusu watoto waliopewa mimba kurudi shule ni anguko la taifa la kesho

Serikali iache mzaha; kuruhusu watoto waliopewa mimba kurudi shule ni anguko la taifa la kesho

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
SERIKALI IACHE MZAHA; KURUHUSU WATOTO WALIOPEWA MIMBA KURUDI SHULENI KUSOMA NI ANGUKO LA TAIFA LA KESHO.

Anaandika Robert Heriel.

Naiomba serikali, viongozi wakubwa msikie Jambo hili, tena msifanye mzaha. Huruma huruma za ajabu ajabu katika baadhi ya ishu ni hatari Kwa ustawi wa taifa.

Nafahamu wapo watu wenye roho laini, wenye huruma, lakini siku zote huruma ikizidi huleta Matatizo.

Kuruhusu watoto wakike waliopata mimba kuendelea na shule kimantiki ni Kuruhusu watoto wakike wapewe MIMBA. Yaani mi Kuruhusu mimba mashuleni Kwa lugha ya kawaida.

Nyakati za Magufuli, moja ya mambo niliungana naye ni pamoja na hili. Hatuwezi kuwa wapole na wenye huruma katika masuala haya ya Msingi.

Nani asiyejua nchi yetu ni masikini, Nani asiyejua familia zetu nyingi ni familia zilizozidiwa na ufukara. Kuzaa kunahitaji maandalizi, kuzaa kunahitaji mipango, kunahitaji wazazi wawili wenye akili iliyokomaa. Kuruhusu watoto waliopewa ujauzito waendelee na shule ni kuongeza matatizo ya kimaadili na kiuchumi.

Niliwahi kuandika kuwa serikali Kwa sehemu kubwa inachangia kumomonyoko Kwa maadili ya jamii.

Unamsomesha aliyepata mimba shuleni na wakati huo huo unamfunga miaka 30 aliyembebesha mimba huyo binti, hiyo ni Akili kweli, embu tutafakari. Kama tumeamua kuwapa watu adhabu acheni wapewe adhabu.

Huyu apoteze haki ya kusoma Kwa kukubali kudanganywa akapewa mimba, huyu mwingine afungwe Kwa kushindwa kujizuia hisia zake na kumpa mimba mtoto wa kike.

Mtoto yeyote aliyebalehe mwenye uwezo wa kubeba mimba ni Mkubwa, na anavigezo vyote vya kuitwa mama ndio maana akabeba mimba.

Kuhusu suala la akili ni ishu nyingine kabisa Kwa maana wapo watu wazima kiumri lakini hawana akili za kikubwa, na wapo watu wenye umri Kati ya 15-18 ambao wanaakili za kikubwa. Hivyo logically hatuwezi kusema Umri ni Akili au akili ni Umri ikiwa wapo wenye umri mkubwa wanazidiwa akili na wenye umri mdogo.

Kuruhusu wanafunzi waliopewa mimba wasome ni kuidhinisha zinaa ndani ya nchi. Ni kuitangazia dunia kuwa nchi yetu inaruhusu zinaa. Hapatakuwa na hofu yoyote Kwa mabinti kushiriki tendo la ndoa.

Serikali na watu wote tutambue kuwa moja ya mambo yanayowatisha mabinti wa kike wasifanye zinaa ni Kama ifuatavyo;

1. Kasumba ya kuumia wakati WA kutolewa Bikra.( Hii ni Kwa ambao hawajawahi kufanya kabisa).

2. Aibu ya maumbile. Wasichana kuogopa kuonekana nyuchi na maungo Yao ya Siri kwani wanahofia Kuambiwa wanamaumbile mabaya.

3. Kupata MIMBA
Mabinti wengi huogopa zaidi mimba kuliko magonjwa ya zinaa.

4. Kupata magonjwa ya zinaa Kama UKIMWI
Japo hii sio Sana lakini ni moja ya sababu kuu nne zinazowafanya mabinti waogope kuingia kwenye tendo la ndoa.

5. Maadili ya Dini na wazazi
Wapo watoto waliolelewa wakaleleka. Hawa huogopa kujiingiza kwenye tendo la ndoa mapema Kwa sababu ya Mafunzo waliyopewa. Hawa ni wachache.

Sababu namba tatu ambayo ni kupata mimba ni sababu nyeti mno ambayo mabinti huogopa kufanya ngono hovyo hovyo. Hii ni kutokana na kuwa mimba huwafanya wafukuzwe shule, lakini la pili mimba ni aibu kwao wenyewe na wazazi wao. Mimba huwaumbua kwa Yale waliyofanyia gizani sasa hutokea hadharani Kwa tumbo kuvimba.

Kuruhusu mimba shuleni ni Kuruhusu watoto wasio na Baba.

Kuruhusu Mimba shuleni ni Kuruhusu watoto wa mitaani kwani familia nyingi za kibongo ni Masikini.

Kuruhusu Mimba shuleni ni Kuruhusu ongezeko la single Mama hapo Baadaye ambalo kimsingi linaathari hata hivi sasa.

Kuruhusu Mimba shuleni ni Kuruhusu taifa kuelemewa na Kundi tegemezi ambalo halilisaidii TAIFA.

Kuruhusu Mimba shuleni kutaathiri maadili ya watoto kwenye malezi kwani wamama wazazi watakuwa shuleni wakisoma wakati Mtoto akiachwa Kwa mfanyakazi wa ndani, sasa jiulize ni familia ngapi zinauwezo WA kuajiri mfanyakazi wa ndani.

Kuruhusu Mimba shuleni ni kuhujumu nguvu kazi ya nchi; kwani Mwanaume atafungwa, mama atarudi shule, Bibi naye Kwa vile bado ni kijana afanyaye kazi labda ni kilimo au ujasiriamali au kazi za ualimu, uhasibu n.k watabidi waache kazi zao wadili na mtoto au waajirifanyakazi WA ndani ili wamlipe Mshahara Mdogo usiozidi 50,000 ambao pia ni uhujumu uchumi.

Serikali iache zile sheria za shule Kama zilivyo.
Atakayempa mimba mwanafunzi apate miaka yake 30 jela, na mwanafunzi afukuzwe shule. Kumbuka nimesema hakuna mtoto anayebeba Mimba.
Mtu au kiumbe chochote chenye uwezo wa kubeba mimba ujue kimekomaa, imefikisha umri wa kuitwa Mkubwa.
Kwenye nature au asili, kubeba mimba au kutungisha mimba ni moja ya ishara ya ukubwa.

Serikali na wazazi tusiendekeze mambo haya. Nafahamu Sisi sote tuwazazi, wanaopata mimba ni binti zetu, dada zetu, watoto wetu n.k lakini lazima tuwe wakali katika hili.

Mtoto aambiwe angali mdogo, ukipata mimba shule unafukuzwa, nyumbani unafukuzwa, yaani mtoto akijua Jambo hilo hawezi pata mimba ninauhakika. Hofu ndiyo ilifanya kizazi kilichopita kubaki na maadili.

Familia zinazoendekeza watoto ndizo hupata madhara ya watoto kupatwa na mimba wakiwa shuleni, kuwa mashoga, kuvuta bango na kutumia madawa ya kulevya.

Nafahamu kuna Exceptional katika mambo mengi, hivyo hata katika Jambo hili wapo wanaopatwa na madhara Kwa bahati mbaya tuu Kama kubakwa Kwa lazima, kulazimishwa kunywa madawa ya kulevya, kulawitiwa n.k. lakini kundi hili wapo wachache mno,
Wengi Hufanya Kwa hiyari Yao wenyewe.

Serikali nafahamu inaweza ikawa inahitaji pesa Fulani kutoka nchi za nje, ikiwa ni hivyo nasi itumie Siasa katika Jambo hili. Kwenye media iwe mataifa wanajua kuwa tunaruhusu wanafunzi waliopewa mimba kuendelea kusoma lakini kiuhalisia hakuna kitu Kama hicho.

Kalagabaho!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa OSTERBAY, DAR ES SALAAM
 
Naunga mkono hoja yako.

Ila Kuna mahali nakupinga[emoji116]
Unaposema,
"Kuruhusu mimba shulen kutaongeza watoto wengi wa mitaani"

Kwa maoni yangu,
Maamuz ya awali ya kuwafunga baba wazazi miaka 30 jela ndo iliongeza watoto wa mitaani,

Maana binti alopewa mimba anabaki Kama yatima, mtoto analelewa na mama pekee asiye na chochote kuweza kukidhi mahitaji.

Mwisho wa sikU,
Binti anatelekeza mtoto.
Na ndo watoto wengi wa mitaani tunaowaona Sasa.
 
Tunatumia muda mwingi kupromote na kutetea mambo ya hovyo kwenye jamii.

Yani asiyefuata maadili anaenda kuchanganywa na wanaofuata maadili baada ya miaka 10 wote unakuta wameoza.

Wamemwandaa nani wa kuacha shughuli zake alee hao watoto watakao zaliwa na kuachwa na wazazi wao? Maana baba ataenda jela miaka 30 na mama atarudi shule.

Muda si mrefu na haki ya vilainishi itaruhusiwa
 
Sisi runwmpinga jiwe kwani hakuwa na jema hata moja...hata CHADEMA NA CCM NA ZITO WANAKUBALINA NA HAYA MAONI YANGU
 
Nimeshangaa sana unapokomalia kuwa kila anayepata mimba n mkubwa na anajielewa ungekua kwenye jamii zetu ukaona vibinti vidogo hata balehe bado vinafanya ngono bila kujua madhara yake ungekomaa na Serikali waendelee kutoa elimu ya jinsia kwanzia primary school kunusuru kizazi na sio kufukuza wenye mimba shule. Zipo cases nyingi za waliorudi shule na wakafaulu vzr zaidi tuwasaidie watt wetu
 
Kwenye media iwe mataifa wanajua kuwa tunaruhusu wanafunzi waliopewa mimba kuendelea kusoma lakini kiuhalisia hakuna kitu Kama hicho.
Kuna NGO zipo kumonitor masuala ya jamii zikiona hilo Gap haraka mnoo misaada itasitishwa.

SERIKALI IACHE MZAHA; KURUHUSU WATOTO WALIOPEWA MIMBA KURUDI SHULENI KUSOMA NI ANGUKO LA TAIFA LA KESHO.
Zaidi ya watoto elfu 50 huacha shule kila mwaka kwa sababu mbalimbali ikiwemo ujauzito. Sasa basi unataka uwanyime hao mabinti haki ya kupata elimu kisa ana ujauzito???

Kama issue ni kuwatisha basi inatakiwa hiyo jela miaka 30 ndio iwatishe wanaume ili wasiwarubuni mabinti.

Nimewahi sema humu na narudia, jamii nzima imechafuka na maadili yameporomoka kote sasa utaadhibu vipi kundi fulani la jamii tena kwa kuwanyima haki ya kusoma ili wawe na future nzuri baadae ILIHALI kuna wababa na wamama watu wazima wanaendekeza uzinzi na rudhwa ya ngono makazini lakini sijawahi sikia mkisema na wao wafutiwe digrii zao!!

Wapewe adhabu ya fine au kazi ngumu ila sio kukosa elimu. Sijui kwanini mnawaza ujinga kiasi hiki. Kwa hili nasimama na serikali!!
 
TL DR

Upo Oysterbay Dar so unaongea kama mtu ambaye ana uzoefu na Dar.

Nimeishi mikoa kadhaa kama Makete, Mbeya, Njombe, Lindi, Tanga na huko kote nilikua naishi maeneo ya ndani ndani. Isipokua Dar, Dar nimeishi uswahilini.

Katika mikoa hiyo yote ukiachilia Dar mtoto wa kike anazaliwa akiwa tayari destiny yake ni kuolewa haijalishi kama ana akili nyingi ama la. She will grow up huku jamii inayomzunguka ikimtarajia aolewe.

Kwa Dar kuna kumvumilia amalize form four ila siyo hiyo mikoa niliyoishi. Mkumbara mtoto wa miaka tisa atatolewa mahari. Wanaume kuanzia wazee mpaka wanafunzi wenzake wanamuwinda huyo binti ili walale naye. Katika maeneo ambayo uchumi wao haupo sawa ni ngumu binti kukataa watu wote in fact anaweza kuwakubali watu wote vilevile

Hawa mabinti wana chansi, na chansi waliyonayo ni kupitia kwenye elimu. Serikali iliunda sera kwa kuzingatia changamoto za mtoto wa kike ndiyo sababu hata ufaulu wao upo lax kulinganisha na mtoto wa kiume. Hili taifa litaokolewa na elimu na hakuna namna tutaacha kumpatia elimu eti kisa alipata mimba.

Kama watu wote tukielimika tutagundua kwamba elimu inapaswa imguse kila mtu, taifa lina wajinga wengi serikali inakazana kuwapunguza yet few people wanakandamiza hizo juhudi kwa kigezo cha maadili.

Ukiachilia hilo, hii nchi iliingia mikataba ya kimataifa ya haki za binadamu haki mojawapo ni elimu. Kila mtu ana haki ya elimu, ukipata mimba do you stop being a human?

Marehemu Magufuli aligomea elimu kwa wanafunzi waliopata mimba na taasisi mbalimbali zilitoa matamko that's because elimu ni basic human rights. Mwanafunzi wa kike akishanyimwa elimu asipoolewa na kwao kukiwa na umaskini huyu mwanae atasoma kweli? So tutakua tumetengeneza wajinga wawili kwa sera moja ya kipuuzi.
 
Nakubaliana na wewe leo.ELIMU kwanza Hizo mimba ni miezi tisa tu kishaa anapewa nafasi ya kunyonyesha then anapambana na kitabu.PERIOD
 
Anguko ni kumnyima elimu wakati ana mtoto anaye mtegemea.JUST THINK.BABA unamtandika 30 kwa kubaka halafu mama unamnyima elimu unafikiri huyo kiumbe alozaliwa utamlea wewe?
Ndio maana ya Adhabu

Lengo la adhabu ni kukuonya na kumfundisha mtu.

Huyo binti na kijana kila mmoja atumikie adhabu yake ili iwe fundisho Kwa wengine.

Elimu pasipo na maadili haina maana yoyote.
 
Kuna NGO zipo kumonitor masuala ya jamii zikiona hilo Gap haraka mnoo misaada itasitishwa.

Zaidi ya watoto elfu 50 huacha shule kila mwaka kwa sababu mbalimbali ikiwemo ujauzito. Sasa basi unataka uwanyime hao mabinti haki ya kupata elimu kisa ana ujauzito???

Kama issue ni kuwatisha basi inatakiwa hiyo jela miaka 30 ndio iwatishe wanaume ili wasiwarubuni mabinti.

Nimewahi sema humu na narudia, jamii nzima imechafuka na maadili yameporomoka kote sasa utaadhibu vipi kundi fulani la jamii tena kwa kuwanyima haki ya kusoma ili wawe na future nzuri baadae ILIHALI kuna wababa na wamama watu wazima wanaendekeza uzinzi na rudhwa ya ngono makazini lakini sijawahi sikia mkisema na wao wafutiwe digrii zao!!

Wapewe adhabu ya fine au kazi ngumu ila sio kukosa elimu. Sijui kwanini mnawaza ujinga kiasi hiki. Kwa hili nasimama na serikali!!

Elimu pasipo maadili haina maana yoyote ile ndani ya jamii.

Sheria hiyo ilipaswa izingatie mazingira ya nchi ZETU.
Huwezi leta sheria za nchi zilizoendelea kwenye nchi masikini, labda zile sheria kuu za ulimwengu.

Magufuli licha ya kuwa nilikuwa natofautiana naye kwenye masuala ya demokrasia na utawala Bora lakini katika hili nilimuunga Mkono.

Hiyo ni adhabu na haipaswi kuwa kwa mtindo WA huruma.

Kama binti au kijana anataka kusoma achague moja kusoma au Kulea.
Kuchekeana chekeana na huruma zisizo na maana yoyote hazipaswi kupewa Nafasi.

Yaani uharibu taifa kisa misaada ya muda mfupi?
 
Chief, ukumbuke huyu binti bila shaka atakuwa na umri chini ya miaka 18

Sheria na wote tunaamini binti au kijana chini ya 18yrs wanakuwa hawana akili timamu kimaamuzi ndio maana tunasema chini ya 18yrs atakuwa amebakwa..

Sasa kama wote tunakubaliana binti chini ya miaka 18 kisheria kufanya mapenzi ni makosa na anakuwa amebakwa tunaanzaje kumhukumu huyu binti na kumnyima haki yake?...
 
Back
Top Bottom