Mtoto anavunja ungo akiwa na miaka 12, unataka avumilie kufanya mapenzi hadi afikishe miaka 26 hadi 30? Ni ngumu sana bila nguvu za Mungu kuingilia kati.
Kule boarding school walikuwa wanatuwekea mafuta ya taa kwenye chakula hasa maharage maana walijua vidume tumebalehe tayari.
sisapoti uzinzi wala watoto kufanya mapenzi. lakini kuna ukweli ufuatao ambao hauepukiki kuufikiria kichwani kama una akili timamu.
1. Majority ya watoto wanafanya mapenzi hata kabla hawajafika 18. na bado ni watoto akili zao za kitoto, wakipata mimba wachukulie kuwa bdo ni watoto sio watu wazima hata uwahukumu kama watu wazima.
2. kama wanafanya ngono, hata kama utawachunga namna gani, wanawez akupata mimba.
3. akipata mimba ukamchinjia baharini aidha kwa kumhukumu zaidi, kumfukuza home, kumsimamisha masomo, unakuwa umemkomoa kwa kumpa adhabu kubwa kupita kiasi, adhabu ya kukatisha ndoto zake za elimu, hivyo haujamsaidia bali umemharibia zaidi.
4. wewe unayestopisha mtoto asiendelee na elimu kwasababu amepata mimba hauna tofauti yeyote kimatendo na yule aliyempa mimba. wote mnafanya makosa.
5. pamoja na kwamba amepata mimba, lakini bado anahitaji kusaidiwa ili ndoto zake zisiishie hapo.
6. watoto/wanafunzi wanapata mimba kwasababu tu ni wanawake, ingekuwa wanaume pia wanapata mimba, basi watoto wa kiume wangepata mimba nyingi kuliko hata wanawake kwasababu kwa uzoefu wangu mimi mwenyewe kama mwanaume, watoto wanaofanay mapenzi mapema zaidi kuliko wenzao ni wanaume. mwanamke anaweza kuishi bikra hadi miaka 20 na kuendelea, lakini watoto wa kiume wanatoa bikra zao/wanaanza mapenzi mapema sana. watoto wa kike wanakua wakiogopa kufanya mapenzi na wanachelewa kuyaanza kuliko watoto wa kiume.
7. watoto wa kike wanaopata mimba wanatakiwa kusaidiwa zaidi kuliko kukomolewa.
8. ni akili za kiporipori tu ndizo zinaamini mtoto wa kike aliyepata mimba hatakiwi kuendelea kusoma. jifunzeni duniani kwenye nchi za wenzetu walioendelea, wanafanyaje, nasema hivi kwasababu watanzania wengi wanaamini mtoto anatakiwa kuishi hivyohivyo hadi aolewe wapate ng'ombe au pesa za mahali though anapoolewa anakuwa sio bikra na hawajui kama as long as hakuwa bikra angepata mimba na wanamhukumu kuhusu mimba tu ila sio kufanya mapenzi.
9. kupata elimu, kutunzwa na kusaidiwa kufika ndoto zake ni haki ya mtoto, akipata mimba as long as bado ni mtoto usifikiri wajibu huo kama mzazi umefutika bado unawajibika.
10. ni nani ana binti hapa amemsomesha akipata mimba atafurahia aishie hapohapo kwenye suala la elimu? hakuna mzazi wa aina hiyo.
11. hatutakiwi kuwahukumu kuhusu mimba, kama hukumu basi tuhukumu watoto/wanafunzi wote ambao sio bikra, nendeni mashuleni pekueni watoto wote wale ambao bikra ndio wabaki shuleni. wale wote wasio na bikra manake wamekuwa wakifanya mapenzi na kulikuwa na possibility yao kupata mimba na hivyo hawana tofauti yeyote na wale waliopata mimba. kama ndio hukumu mnataka kutoa. manake mnapo wahukumu waliopata mimba peke yake na kuacha hao wanaofanya ngono bila kupata mimba, mnachomaanisha ni kwamba ninyi mliopata mimba tunawahukumu kwa uzembe wa kupata mimba lakini hamhukumu kitendo cha ngono. kama mnataka basi hukumuni kitendo na sio matokeo. acheni kuishi kiporipori, tupo kwenye ulimwengu wa civilization.