Serikali iangalie uwezekano wa kutoa mikopo kupitia halmashauri kwa mtu hata mmoja mmoja badala ya kulazimishwa kuwa katika kikundi

Huu ndio utakuwa mwanzo wa kufa kwa hiyo project.

Risk ya pesa kupotea kwa mtu mmoja ni kubwa kuliko kikundi.

Mtu mmoja anaweza kopa na kutokomea nazo ila kikundi ambacho members wote wapo verified atapatikana tu mmoja au baadhi yao kubeba mzigo in case of default.

Hili jambo lisifanyike.
Nenda kakope benki siasa nyingi zinakupotezea muda na malengo yako. Unaomba mkopo leo zamu yako inakuwa miaka miwili au mitatu mbele
 
Kakope benki, hata ya mikopo ya Halmashauri inatakiwa ifutwe kabisa.
Ndugu zangu watanzania,

Mfumo uliopo kwa Sasa juu ya pesa za halmashauri zinazotolewa Kama mkopo kwa vijana kutokana na makusanyo na mapato ya ndani unataka vijana au akina mama au watu wenye ulemavu kuweza kujiunga au kuunda kikundi cha kijasiriamali ili kuweza kupatiwa mkopo, ambapo hapa kuna taratibu za kufuata ili kukidhi vigezo Kama vile kutengeneza katiba, kuwa na akaunti ya kikundi, viongozi wa kikundi, mradi au wazo la mradi au biashara na mengineyo.

Ndugu zangu katika utolewaji wa pesa hizi hazitoi fursa kwa mtu mmoja mmoja kupatiwa mkopo, ukiwa kijana pekee huwezi ukapata mikopo hii hata Kama Ni muaminifu,una wazo zuri la biashara au mradi au una mradi au biashara ambayo ungependa uongeze na kukuza mtaji wako.

Hali hii inawanyima fursa vijana wengine ambao wanaona katika vikundi Kuna kuwa na baadhi ya changamoto Kama vile uaminifu mdogo kwa baadhi ya wanakikundi,kutofautiana kwa malengo, matumizi mabaya ya Fedha, uzembe wa baadhi ya wanakikundi, wengine kuchukua hela na kuishia kugawana pasipo kutumia katika malengo husika.

Kutokuwa na Elimu ya kutosha juu ya mradi au biashara tarajiwa na hivyo kuishia kupoteza mtaji wote kabla hata ya kurejesha, Haraka ya baadhi ya Wana kikundi au vijana kutaka utajiri wa haraka haraka na hivyo kuwekeza katika maeneo hatari wasio na uzoefu nayo au ujuzi nao zaidi ya habari za kusikia tu juu ya faida kubwa watakayoipata.

Hivyo nilikuwa naona Ni wakati wa serikali ya Rais wetu mpendwa mama Samia kuangalia uwezekano wa kutoa fursa ya mkopo kwa mtu hata mmoja mwenye kuhitaji mkopo huu huku wenye kuungana na kuwa kikundi nao waendelee kupewa Kama kawaida,hii itarahisisha na kusaidia vijana wengi Sana kuweza kupata mikopo na kuwasaidia vijana wengine hata kimawazo na kiushauri.

Vigezo vinavyoweza kutumika ni Kama vile uwepo wa Taarifa za kutosha juu ya mwenendo wa kiuadilifu, kiweledi, kimaadili, kiutendaji, kiuaminifu na kitabia kutoka katika uongozi wa serikali za mitaa.

Uwepo wa mdhamini anayeaminika na mwenye makazi ya kudumu katika eneo analotokea na kuishi kijana anayehitaji mkopo, mdhamini akubali kuwajibika endapo mhusika au kijana ataamua kukimbia au kutoroka kabla ya kurejesha pesa halmashauri.

Mdhamini asaiini fomu maalumu mbele ya mwanasheria wa serikali na kula kiapo cha kuwajibika juu ya Deni la anaye mdhamini na kopi ya fomu hiyo ibaki halmashauri ,nyingine kwa mwanasheria,nyingine kwa serikali ya mtaa ,nyingine kwa anayechukua mkopo na nyingine abaki nayo mdhamini.

Mdhamini awe na Mali zisizo hamishika na zenye hati inayotambulika kisheria,mdhamini awe Ni mzazi wa mhusika au mtu mwingine yeyote mwenye Mali zisizo hamishika na makazi ya kudumu eneo husika,Mdhamini akitaka kumdhamini mtu zaidi ya mmoja aruhusiwe mpaka pale tu itakapothibitika kuwa Mali za mdhamini Zina thamani kubwa ukilinganisha na mikopo au fedha inayotaka kuchukuliwa.

Hili Jambo litasaidia halmashauri kupata marejesho ya mikopo yote inayotolewa kwa vijana lakini pia itawasaidia vijana wengi kupata mikopo kwa urahisi bila mlolongo wa kutafutana na hata kuwalazimisha wengine ili wajiunge kwenye vikundi kusudi kutimiza lengo la kupata mkopo ambapo mwisho wa siku Hawa walio lazimishwa au kupachikwa kwenye kikundi kuweza kusaidia kupata mkopo wanakuwa hawana ule moyo au ufanisi mzuri na uwajibikaji mzuri na wanakuwa hawana mchango wowote ule katika kukuza ,kulinda na kuendeleza mtaji.

Naiomba Sana serikali iliangalie hili kwa jicho la kipekee kabisa, maana unakuta mtu unalima lakini unakosa hela ya pembejeo hasa mbolea kwa kuwa unawaza ukitaka mkopo wa kupanua kilimo chako inahitaji uende kwenye kikundi ambacho unajikuta nacho kina malengo mengine kabisa Kama vile ufugaji wa kuku wa mayai au ng'ombe wa maziwa ambapo unaona wewe huwezi ukapata hata nafasi ya kwenda kukatia ng'ombe majani au kuwawekea maji kuku kwa kuwa wewe shughuli zako Ni shambani muda mwingi na ndio Jambo unalolipenda kuliko ufugaji wa kuku wa mayai au nyama au ng'ombe wa maziwa.

Unakuta kikundi kimeundwa na kuomba mkopo wa Jambo fulani lakini Wana kikundi kila mmoja ana malengo yake kichwani juu ya hela ikiwa mkononi mwao, hivyo kupelekea mradi uliolengwa kukosa nguvu ya pamoja ya wanakikundi.

Kazi Iendeleee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu. 0742-676627
 
Juzi nilienda kupata ABCD kama kijana nikaambiwa hayo hayo ya kikundi nilimchallenge yule dada Afisa Maendelo kuhusu kuruhusu mkopo wa mmoja mmoja akasema hilo suala limejadiliwa na sio muda Wizara itatoa tamko lakini hadi sasa kuna matumaini ya kuja kwa mikopo ya mtu mmoja mmoja,
Endelea kua karibu na Halmashauri yako utakuja kupokea habari njema.
Ndio imeisha hiyo. Mradi yeye aningiza mshahara na anapiga madili ya upigaji basi hawezi kuwazia faida ya wanajamii wengine.
 
Na ripoti ya CAG, imebaini ufisadi wa hali ya juu kwenye hizo halmshauri
 
Ndugu zangu watanzania,

Mfumo uliopo kwa Sasa juu ya pesa za halmashauri zinazotolewa Kama mkopo kwa vijana kutokana na makusanyo na mapato ya ndani unataka vijana au akina mama au watu wenye ulemavu kuweza kujiunga au kuunda kikundi cha kijasiriamali ili kuweza kupatiwa mkopo, ambapo hapa kuna taratibu za kufuata ili kukidhi vigezo Kama vile kutengeneza katiba, kuwa na akaunti ya kikundi, viongozi wa kikundi, mradi au wazo la mradi au biashara na mengineyo.

Ndugu zangu katika utolewaji wa pesa hizi hazitoi fursa kwa mtu mmoja mmoja kupatiwa mkopo, ukiwa kijana pekee huwezi ukapata mikopo hii hata Kama Ni muaminifu,una wazo zuri la biashara au mradi au una mradi au biashara ambayo ungependa uongeze na kukuza mtaji wako.

Hali hii inawanyima fursa vijana wengine ambao wanaona katika vikundi Kuna kuwa na baadhi ya changamoto Kama vile uaminifu mdogo kwa baadhi ya wanakikundi,kutofautiana kwa malengo, matumizi mabaya ya Fedha, uzembe wa baadhi ya wanakikundi, wengine kuchukua hela na kuishia kugawana pasipo kutumia katika malengo husika.

Kutokuwa na Elimu ya kutosha juu ya mradi au biashara tarajiwa na hivyo kuishia kupoteza mtaji wote kabla hata ya kurejesha, Haraka ya baadhi ya Wana kikundi au vijana kutaka utajiri wa haraka haraka na hivyo kuwekeza katika maeneo hatari wasio na uzoefu nayo au ujuzi nao zaidi ya habari za kusikia tu juu ya faida kubwa watakayoipata.

Hivyo nilikuwa naona Ni wakati wa serikali ya Rais wetu mpendwa mama Samia kuangalia uwezekano wa kutoa fursa ya mkopo kwa mtu hata mmoja mwenye kuhitaji mkopo huu huku wenye kuungana na kuwa kikundi nao waendelee kupewa Kama kawaida,hii itarahisisha na kusaidia vijana wengi Sana kuweza kupata mikopo na kuwasaidia vijana wengine hata kimawazo na kiushauri.

Vigezo vinavyoweza kutumika ni Kama vile uwepo wa Taarifa za kutosha juu ya mwenendo wa kiuadilifu, kiweledi, kimaadili, kiutendaji, kiuaminifu na kitabia kutoka katika uongozi wa serikali za mitaa.

Uwepo wa mdhamini anayeaminika na mwenye makazi ya kudumu katika eneo analotokea na kuishi kijana anayehitaji mkopo, mdhamini akubali kuwajibika endapo mhusika au kijana ataamua kukimbia au kutoroka kabla ya kurejesha pesa halmashauri.

Mdhamini asaiini fomu maalumu mbele ya mwanasheria wa serikali na kula kiapo cha kuwajibika juu ya Deni la anaye mdhamini na kopi ya fomu hiyo ibaki halmashauri ,nyingine kwa mwanasheria,nyingine kwa serikali ya mtaa ,nyingine kwa anayechukua mkopo na nyingine abaki nayo mdhamini.

Mdhamini awe na Mali zisizo hamishika na zenye hati inayotambulika kisheria,mdhamini awe Ni mzazi wa mhusika au mtu mwingine yeyote mwenye Mali zisizo hamishika na makazi ya kudumu eneo husika,Mdhamini akitaka kumdhamini mtu zaidi ya mmoja aruhusiwe mpaka pale tu itakapothibitika kuwa Mali za mdhamini Zina thamani kubwa ukilinganisha na mikopo au fedha inayotaka kuchukuliwa.

Hili Jambo litasaidia halmashauri kupata marejesho ya mikopo yote inayotolewa kwa vijana lakini pia itawasaidia vijana wengi kupata mikopo kwa urahisi bila mlolongo wa kutafutana na hata kuwalazimisha wengine ili wajiunge kwenye vikundi kusudi kutimiza lengo la kupata mkopo ambapo mwisho wa siku Hawa walio lazimishwa au kupachikwa kwenye kikundi kuweza kusaidia kupata mkopo wanakuwa hawana ule moyo au ufanisi mzuri na uwajibikaji mzuri na wanakuwa hawana mchango wowote ule katika kukuza ,kulinda na kuendeleza mtaji.

Naiomba Sana serikali iliangalie hili kwa jicho la kipekee kabisa, maana unakuta mtu unalima lakini unakosa hela ya pembejeo hasa mbolea kwa kuwa unawaza ukitaka mkopo wa kupanua kilimo chako inahitaji uende kwenye kikundi ambacho unajikuta nacho kina malengo mengine kabisa Kama vile ufugaji wa kuku wa mayai au ng'ombe wa maziwa ambapo unaona wewe huwezi ukapata hata nafasi ya kwenda kukatia ng'ombe majani au kuwawekea maji kuku kwa kuwa wewe shughuli zako Ni shambani muda mwingi na ndio Jambo unalolipenda kuliko ufugaji wa kuku wa mayai au nyama au ng'ombe wa maziwa.

Unakuta kikundi kimeundwa na kuomba mkopo wa Jambo fulani lakini Wana kikundi kila mmoja ana malengo yake kichwani juu ya hela ikiwa mkononi mwao, hivyo kupelekea mradi uliolengwa kukosa nguvu ya pamoja ya wanakikundi.

Kazi Iendeleee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu. 0742-676627
Zile pesa zipo kisiasa sio kusaidia watu, ndiomaana CAG kasema zimetafunwa na hakuna aliyeguswa
 
Huu utaratibu umetangazwa lini!?..maana juzi tu Waziri mkuu kasema hiyo mikopo isimamishwe
Mh Rais alisema juu ya suala Hilo baada ya kugundua kuwa pesa zinaliwa Sana na watumishi wasiowaaminifu katika halmashauri kwa kushirikiana na madiwani,ndipo akasema kuwa kwa Sasa pesa hizo zitakuwa zinapelekwa benki na huko ndiko zitakakochukuliwa ili iwe Rahisi hata katika urejeshaji wa mikopo kwa ajili ya kuwanufaisha wengine
 
Zile pesa zipo kisiasa sio kusaidia watu, ndiomaana CAG kasema zimetafunwa na hakuna aliyeguswa
Kwa Sasa utatumika utaratibu mpya juu ya pesa hizo ,ambapo kwa Sasa watu wata kopa kupitia benki ambako halmashauri itaingia makubaliano na benki moja wapo juu ya pesa hizo za vijana,akina mama na watu wenye ulemavu
 
Miradi ya vikundi ni upuuzi mtupu....
Kwa Sasa walengwa watanufaika nazo kwa kuwa Nafikiri hata wewe unafahamu kuwa kuchukua pesa benki hakuwezi kukawa na janja janja Kama zilizokuwepo halmashauri ambapo watu wengine walikuwa wananufaika na pesa hizi pasipo kustahili
 
Mh Rais alisema juu ya suala Hilo baada ya kugundua kuwa pesa zinaliwa Sana na watumishi wasiowaaminifu katika halmashauri kwa kushirikiana na madiwani,ndipo akasema kuwa kwa Sasa pesa hizo zitakuwa zinapelekwa benki na huko ndiko zitakakochukuliwa ili iwe Rahisi hata katika urejeshaji wa mikopo kwa ajili ya kuwanufaisha wengine
Haimaanishi kasema itolewe kwa mtu mmoja mmoja
 
We si huko jikoni kwanini usiwabane
Viongozi wako huko

Ova
 
Hujasoma report ya CAG... Pesa zilizotengwa kwa ajili ya kukopesha zimepigwa zote...
 
Back
Top Bottom