Serikali ichunguzeni kampuni ya Mysol, inatesa wananchi

Wewe ndio jambazi. Kwani mlikubaliana ukipata umeme utaacha kuwalipa? Watanzania tuwe na tabia ya kuIipa madeni.
ni suala ambalo lipo wazi kabisa, mtoa post mlalamikaji embu kuwa serious na maisha .
watu wanafanya biashara unawaletea mchezo. Wakati wamepoteza soko kubwa huko.
Kwa hiyo unataka kutuambia ambao washalipia deni lote na kwa sasa wameweka tanesco nao wakitaka warudishe hizo soler warudishiwe hela inawezekana?
Cha msingi kama huitaki tena huyo soler kaa nao chini mkubaliane nusu hasara au urudishiwe kiasi fulani manake kwa ulivyoelezea hiyo ussue you are on the loosing side
 
Pole sana ila wewe hapa ndio mwenye makosa lipa deni lao liishe then umiliki solar na tv yao ila kama haujakamilisha wana haki ya kukunyan'ganya mtambo wao hata kama umelipa 2.65m.

Haya makampuni ya kukopesha ni wezi sana ,wanawadanganya wateja kwa miflat screen mikubwa tu ila at the end wanapiga fedha kubwa sana.

Mimi huku minjingu nimefunga solar ya dukani ,sijataka kubanwa na mambo ya kulipia kila siku.
 
una IDs ngapi ?

acha ujanja wa kijinga, lipa Pesa wengine wakope mtambo
 
Sijauona huo mkataba, kwa scenario hii, una wajibu wa kumaliza hilo deni, labda utuambie kama kulikua na makubaliano kuwa grid ya taifa ikifungwa na kuanza kazi ama ukiwa/ukipata chanzo kingine cha nishati itakubalika kusitisha wajibu wako kulipa na kumaliza deni.

Na uache ujuaji.
 

Wapo sahihi, huo ni mkataba kati yako na wao. Uwe umefungiwa umeme wa Tanesco au la, lazima umalize deni lao! Ni sawa na mkopo wa benki, kama umeshindwa kuulipa wote lazima ufilisiwe na hela huwa hairudi! Kwa hiyo pambana na hali yako hakuna kitu cha bure duniani!
 
Unafeli Mkuu!! Ununue tu mtambo uwe wako. Peleka bushi huko ufunge onyesha mpira. Utakulipa sana
 
Acha kelele lipa deni letu. Na ole usipomalizia tutachukua solar yetu na kukushtaki
 
Ungeeleza kwanza inakusumbuaje
 
Mbona hiyo kampuni hapo haina shida,hapo hujamaliza mkataba,bado wanakudai.

Kuunganishiwa umeme wa tanesco hapo haiwahusu,maliza deni lao.
 
Mimi ni mteja miaka miwili sasa,nilinunua baada ya kuona rafk yangu akitumia mwaka wa 5 sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…