Serikali ichunguzeni kampuni ya Mysol, inatesa wananchi

Wewe ndio jambazi. Kwani mlikubaliana ukipata umeme utaacha kuwalipa? Watanzania tuwe na tabia ya kuIipa madeni.
ni suala ambalo lipo wazi kabisa, mtoa post mlalamikaji embu kuwa serious na maisha .
watu wanafanya biashara unawaletea mchezo. Wakati wamepoteza soko kubwa huko.
Kwa hiyo unataka kutuambia ambao washalipia deni lote na kwa sasa wameweka tanesco nao wakitaka warudishe hizo soler warudishiwe hela inawezekana?
Cha msingi kama huitaki tena huyo soler kaa nao chini mkubaliane nusu hasara au urudishiwe kiasi fulani manake kwa ulivyoelezea hiyo ussue you are on the loosing side
 
Pole sana ila wewe hapa ndio mwenye makosa lipa deni lao liishe then umiliki solar na tv yao ila kama haujakamilisha wana haki ya kukunyan'ganya mtambo wao hata kama umelipa 2.65m.

Haya makampuni ya kukopesha ni wezi sana ,wanawadanganya wateja kwa miflat screen mikubwa tu ila at the end wanapiga fedha kubwa sana.

Mimi huku minjingu nimefunga solar ya dukani ,sijataka kubanwa na mambo ya kulipia kila siku.
 
una IDs ngapi ?

acha ujanja wa kijinga, lipa Pesa wengine wakope mtambo
 
Hii ni kampuni ya KITAPELI kama si KIJAMBAZI. Mwezi Februari mwaka huu niliingia mkataba wa sola ya watt 180 ambapo baada ya kulipa malipo ya awali ya shilingi laki mbili, niliendelea kulipa kila siku kidogokidogo na mpaka leo tarehe 24 nimeshalipa jumla ya shilingi 1,688,000 kati ya shilingi 2,700,000.
Sijauona huo mkataba, kwa scenario hii, una wajibu wa kumaliza hilo deni, labda utuambie kama kulikua na makubaliano kuwa grid ya taifa ikifungwa na kuanza kazi ama ukiwa/ukipata chanzo kingine cha nishati itakubalika kusitisha wajibu wako kulipa na kumaliza deni.

Na uache ujuaji.
 
Wana Jamii Forums nawasalimu nyote

Mimi ni mkazi wa wilaya ya Kibondo hapa mkoani Kigoma. Ninaomba msaada wa kisheria kutokana na ugomvi nilionao na kampuni ya KITAPELI ya sola inayoitwa MYSOL maana tunakoenda naweza kuja kukata kichwa cha mfanyakazi wao nikapata kesi ya mauaji.

Hii kampuni hukopesha mitambo ya sola ambapo mteja hutakiwa kulipa malipo ya awali kutegemea na ukubwa wa sola mfano Tsh.180,000 au 300,000,kisha malipo mengine hutakiwa kulipa kidogokidogo mpaka atakapomaliza mkataba wake.

Hii ni kampuni ya KITAPELI kama si KIJAMBAZI. Mwezi Februari mwaka huu niliingia mkataba wa sola ya watt 180 ambapo baada ya kulipa malipo ya awali ya shilingi laki mbili, niliendelea kulipa kila siku kidogokidogo na mpaka leo tarehe 24 nimeshalipa jumla ya shilingi 1,688,000 kati ya shilingi 2,700,000.

Kama mnavyofahamu,wiki iliyopita Raisi kazindua Gridi huku Kigoma nami ni mmoja kati ya wananchi tuliounganishwa na umeme wa TANESCO.

Jambo la kushangaza ni kwamba haya MAJAMBAZI YA KAMPUNI YA MYSOL bado yanataka eti niendelee kulipia sola yao wakati nimeshapata umeme wa TANESCO ambao kwangu ni rahisi na nafuu kuliko MISOLA YAO YA KIPUMBAVU. Tangu nimefunga hilo LISOLA lao limekuwa likinisumbua mara kwa mara na wao kuja kurekebisha ni mpaka wajisikie wao kuja. Nilishagombana nao sana lakini niliendelea kuvumilia.

Kwa kuwa tayari nina umeme wa TANESCO, Sola nimeitoa na kuiweka ndani. Nashangaa wanakuja na Polisi eti kuichukua kwa sababu siilipi tena, je pesa yangu shilingi 1,688,000 nitaipataje?wananijibu hiyo pesa HAIRUDISHWI. Kwa kweli nimewazuia hao maofisa wa hiyo kampuni pamoja na polisi wawili waliokuja nao.

Naomba kama kuna mwana JF aliyewahi kudili na haya MAJAMBAZI YA MYSOL anipe msaada wa jinsi ya kukabiliana nayo maana nasikia HARUFU YA KUMWAGA DAMU wakija tena kutaka kuchukua kwa nguvu maana wameahidi kuja kuchukua na bunduki. Na tupo wananchi 7 ambao haya MAJAMBAZI YA MYSOL yamekuja yanataka KUTUDHULUMU. Msaada tafadhali

Nawasilisha

Wapo sahihi, huo ni mkataba kati yako na wao. Uwe umefungiwa umeme wa Tanesco au la, lazima umalize deni lao! Ni sawa na mkopo wa benki, kama umeshindwa kuulipa wote lazima ufilisiwe na hela huwa hairudi! Kwa hiyo pambana na hali yako hakuna kitu cha bure duniani!
 
Unafeli Mkuu!! Ununue tu mtambo uwe wako. Peleka bushi huko ufunge onyesha mpira. Utakulipa sana
 
Acha kelele lipa deni letu. Na ole usipomalizia tutachukua solar yetu na kukushtaki
 
Wana Jamii Forums nawasalimu nyote

Mimi ni mkazi wa wilaya ya Kibondo hapa mkoani Kigoma. Ninaomba msaada wa kisheria kutokana na ugomvi nilionao na kampuni ya KITAPELI ya sola inayoitwa MYSOL maana tunakoenda naweza kuja kukata kichwa cha mfanyakazi wao nikapata kesi ya mauaji.

Hii kampuni hukopesha mitambo ya sola ambapo mteja hutakiwa kulipa malipo ya awali kutegemea na ukubwa wa sola mfano Tsh.180,000 au 300,000,kisha malipo mengine hutakiwa kulipa kidogokidogo mpaka atakapomaliza mkataba wake.

Hii ni kampuni ya KITAPELI kama si KIJAMBAZI. Mwezi Februari mwaka huu niliingia mkataba wa sola ya watt 180 ambapo baada ya kulipa malipo ya awali ya shilingi laki mbili, niliendelea kulipa kila siku kidogokidogo na mpaka leo tarehe 24 nimeshalipa jumla ya shilingi 1,688,000 kati ya shilingi 2,700,000.

Kama mnavyofahamu,wiki iliyopita Raisi kazindua Gridi huku Kigoma nami ni mmoja kati ya wananchi tuliounganishwa na umeme wa TANESCO.

Jambo la kushangaza ni kwamba haya MAJAMBAZI YA KAMPUNI YA MYSOL bado yanataka eti niendelee kulipia sola yao wakati nimeshapata umeme wa TANESCO ambao kwangu ni rahisi na nafuu kuliko MISOLA YAO YA KIPUMBAVU. Tangu nimefunga hilo LISOLA lao limekuwa likinisumbua mara kwa mara na wao kuja kurekebisha ni mpaka wajisikie wao kuja. Nilishagombana nao sana lakini niliendelea kuvumilia.

Kwa kuwa tayari nina umeme wa TANESCO, Sola nimeitoa na kuiweka ndani. Nashangaa wanakuja na Polisi eti kuichukua kwa sababu siilipi tena, je pesa yangu shilingi 1,688,000 nitaipataje?wananijibu hiyo pesa HAIRUDISHWI. Kwa kweli nimewazuia hao maofisa wa hiyo kampuni pamoja na polisi wawili waliokuja nao.

Naomba kama kuna mwana JF aliyewahi kudili na haya MAJAMBAZI YA MYSOL anipe msaada wa jinsi ya kukabiliana nayo maana nasikia HARUFU YA KUMWAGA DAMU wakija tena kutaka kuchukua kwa nguvu maana wameahidi kuja kuchukua na bunduki. Na tupo wananchi 7 ambao haya MAJAMBAZI YA MYSOL yamekuja yanataka KUTUDHULUMU. Msaada tafadhali

Nawasilisha
Ungeeleza kwanza inakusumbuaje
 
Mbona hiyo kampuni hapo haina shida,hapo hujamaliza mkataba,bado wanakudai.

Kuunganishiwa umeme wa tanesco hapo haiwahusu,maliza deni lao.
 
Mimi ni mteja miaka miwili sasa,nilinunua baada ya kuona rafk yangu akitumia mwaka wa 5 sasa
 
Back
Top Bottom