Nafikiria.
Shule zote za msingi, sekondari na vyuo wametangaziwa kusitisha masomo kwa siku 30. Ni katika harakati za kuepusha maambukizi na kusambaa kwa virusi vya Corona.
Ni wazo zuri sana ila bado napata ukakasi katika haya
1: Wanafunzi wa shule za bweni na vyuo watalazimika kusafiri, tayari maambukizi yamethibitishwa yapo Tanzania, endapo kuna mtu/watu m/wenye maambukizi inamaanisha anaweza kusambaza kwa wengi zaidi.
2: Mipaka ya nchi kuwa wazi kwa wanaoingia na kuzuia kutoka. Hili naona wamefanya kinyume, ni rahisi sana kudhibiti kusambaa kwa virusi wagonjwa wachache waliotambulika mpaka sasa hivi endapo mipaka itafungwa kwa wageni wanaokuja. Ila kwa wanalolifanya naona kama wanakaribisha mlipuko.
3: Uchache wa vituo vya kufanyia vipimo. Je endapo ikitokea maambukizi ktk mikoa ambayo haina vituo madhubuti kwa ajili ya upimaji, nini hatma ya wananchi !?
NB: Kuna vituo vilivyotajwa katika kanda eg Mawenzi, Mount Meru, Rufaa Mbeya, Bugando na Mloganzila n.k
Swali la kizushi.
Waliowekwa karantini Arusha, gharama za chakula, malazi, vinywaji nani anagharamia!?
Sent using
Jamii Forums mobile app