Serikali: Idadi ya Wagonjwa wa COVID19 kwenye baadhi ya vituo yapungua

Serikali: Idadi ya Wagonjwa wa COVID19 kwenye baadhi ya vituo yapungua

Kwa kauli iliyotolewa na katibu wa afya.... Wakati akipokea msaada toka serikali ya China.
Kupungua huko ni matokeo ya kupona? Au kutodhuria/kuripoti vituo vya afya?
Kwa taarifa za madereva toka Tanzania wanaopatikana na maambukizi huko nje, ni ishara maambukizi nchini ni makubwa na hakuna jambo lolote linaloonyesha limechukuliwa kudhibiti zaidi ya kunawa mikono na kushona barakoa.
Je, bado serikali haioni ni muhimu kuchunguza ni kwa nini wagonjwa wanapungua hospital badala ya kuongezeka? Na kama ni matokeo ya uhamasishaji wa matumizi ya limau, tangawizi n.k. ndio inapelekea watu kuungulia majumbani, mie napenda kupata taarifa sahihi za maendeleo ya janga hili nchini.
 
hii ndio kazi aliyopewa! mmesahau yeye ndio alipima mapapai! kwa lugha nyingine yeye ndio kafunga maabara kwa maelekezo maalumu! kwa kauli hii ina maana baada ya wiki tuu tutakua tumeifuta corona hapa Tz kwenye vyombo vya habari tutabakia nayo majumbani mwetu
 
Wakifa wanazikana wao kwa wao ina maana hata mortuary wanaogopa kupeleka maiti zao zitapata Corona?

Kwa theory hii maana yake mortuary zingefurika na misiba huko mitaani ingekuwa kila kona.

Haina maana hivyo, japo linawezekana.
Nilichokimaanisha ni kuwa hata wamiliki wa mortuary wanaogopa kupokea hizo maiti za waliokufa kwa korona, achilia mbali kuwa "wahusika wenyewe" hawataki ijulikane kuwa hizo maiti zimetokana na Corona
 
Back
Top Bottom