Serikali: Idadi ya Wagonjwa wa COVID19 kwenye baadhi ya vituo yapungua

Serikali: Idadi ya Wagonjwa wa COVID19 kwenye baadhi ya vituo yapungua

Serikali yatoa Update ya Corona Nchini .

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Prof. Mabula Mchembe amesema kuwa wagonjwa wa corona nchini wamepungua katika vituo vya kutolea huduma za afya na kuwataka watoa huduma za afya kujitahidi kutoa huduma bora kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na magonjwa mengine pia

VIDEO NI KWA HISANI ya Millard Ayo wa Ayo Media.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Prof. Mabula Mchembe amesema idadi ya watu waliopata maambukizi ya Ugonjwa huo kwenye baadhi ya vituo vya matibabu imepungua na wengi wao wanaendelea vizuri.

Ametaja idadi ya wagonjwa kwa siku ya leo kwa Mkoa wa Dar na Pwani katika Hospitali ya Amana kuna wagonjwa 12, Kisoka- Mloganzila 6 pamoja na Kituo cha Kibaha chenye wagonjwa 24

View attachment 1451311

Watu ni kuwa hawaendi hospitali wameamua kfia nyumbani. Hakuna kupungua
 
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Prof. Mabula Mchembe amesema kuwa wagonjwa wa corona nchini wamepungua katika vituo vya kutolea huduma za afya na kuwataka watoa huduma za afya kujitahidi kutoa huduma bora kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na magonjwa mengine pia
😳😳😳😳😳😳
 
Piga kazi acha kushinda mitandaoni kwa kisingizio cha Korona
Dawa yng hyo

Ova
20200516_083820.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Prof. Mabula Mchembe amesema idadi ya watu waliopata maambukizi ya Ugonjwa huo kwenye baadhi ya vituo vya matibabu imepungua na wengi wao wanaendelea vizuri.

Ametaja idadi ya wagonjwa kwa siku ya leo kwa Mkoa wa Dar na Pwani katika Hospitali ya Amana kuna wagonjwa 12, Kisoka- Mloganzila 6 pamoja na Kituo cha Kibaha chenye wagonjwa 24

View attachment 1451311
Kumbe maabara inaendelea kupima? Si Walisema sasahivi hawapimi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kipindi corona inaanza tuliambiwa wasemaji ni 3 tu yani raisi, waziri mkuu na waziri wa afya sasa huyu katibu vipi tens

Hizi takiwimu itakuwa za kupikwa na ndio maana bi Ummy amekataa kuzitangaza inawezekana bi Ummy amefunga hivyo hawezi kudanganya

Mimi hizi siziamini nasubiri zitakazo tangazwa na Ummy hata kama miezi 3 ijayo

Sent using Jamii Forums mobile app
We jamaa unahitaji maombi mengine ya siku tatu mfululizo maana naona yale Mkulu alituelekeza yaliacha baadhi ya wenzetu nyuma wewe ukiwemo.
 
Kwa hiyo mtu atatoka huko aje kuripoti uongo? Na inapotokea mpaka maiti yanamkuta bado watakuwa ananiambia uongo? Ukiwa unafanyakazi sekta ya afya, haina maana unamjua kila mgonjwa na pia sio kwamba hautaguswa na ukweli wa yanayowasibu.

Sent using Jamii Forums mobile app
endelea kufuata propaganda za mzungu utakuja kuelewa baadae
 
Nimetafakari sana .Yaani kinachotokea sasa ni sawa na kupunguza mahindi shambani unaacha yale yenye afya .madhaifu yote unang'oa.

Ndiyo huu ugonjwa unvyotufanya unaua wale wadhaifu dhaifu tuu.wenye kinga za kutosha unawaingia lakini una dunda.mwisho taifa litabakia na watu wenye miili imara na hivyo in long run budget ya wizara itapata ahueni
Darwin Theory law of the jungle survival for the fittest.
Kwa hiyo wanyonge hawatakiwi kulindwa?
 
Mimi sidhani kuwa hali imekuwa nzuri.
Wagonjwa wengi wanakwepa kwenda kwenye vituo vilivyotengwa maana huduma hairidhishi.
Wengi wanaamua kujitibia majumbani mwao.
 
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Prof. Mabula Mchembe amesema idadi ya watu waliopata maambukizi ya Ugonjwa huo kwenye baadhi ya vituo vya matibabu imepungua na wengi wao wanaendelea vizuri.

Ametaja idadi ya wagonjwa kwa siku ya leo kwa Mkoa wa Dar na Pwani katika Hospitali ya Amana kuna wagonjwa 12, Kisoka- Mloganzila 6 pamoja na Kituo cha Kibaha chenye wagonjwa 24

View attachment 1451311
Kapimeni watu huko waliko ,haya ya vituoni kupungua sio kipimo cha kuonyesha hali halisi ya wagonjwa ,wengine hawaendi vituoni,kwanza ilitakiwa mtoe orodha ya vituo vya kupimia corona kwa kila wilaya.
 
Takwimu pekee zilizobakia hapa Tanzania na za kuaminika ni za madereva ya malori ya mizigo, ambao ni wale wavukao mpakani kuingia nchi za jirani, ambapo wenzetu wanatusaidia kuwafanyia vipimo ya Corona na hatimaye kutupa matokeo yake, wakati sisi kwa upande tukiendelea na zoezi la "herd immunity"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa Sawa
Taarifa Njema Iwapo Ni Kweli
Kama ni uongo muulizeni mtoto wa mbowe maana alikua kwa wagonjwa mtuonyeshe picha za wagonjwa walio jazana kama mnavyo dai maana kila kitu mijitu inabisha .

Send by APOLO 1
 
Back
Top Bottom