Serikali: Idadi ya Wagonjwa wa COVID19 kwenye baadhi ya vituo yapungua

Serikali: Idadi ya Wagonjwa wa COVID19 kwenye baadhi ya vituo yapungua

Mwenyezi Mungu aendelee kuwalinda na kuwaepusha na hili janga, wewe, ndugu, jamaa na marafiki zako unaowajua.

Wengine tumeguswa na hata tusiowajua moja kwa moja, na ilitusikitisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
sasa usiowajua una uhakika gani kama wanachokuambia ni kweli ?
 
Mpaka mwezi Wa saba ugonjwa kwisha au tutaishi nao kama waya/ngwengwe/grid
 


Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Prof. Mabula Mchembe amesema idadi ya watu waliopata maambukizi ya Virusi vya Corona kwenye baadhi ya vituo vya matibabu imepungua na wengi wao wanaendelea vizuri.

"Pale Amana kuna wagonjwa 12 na wengi wana hali nzuri, Mloganzila kuna wagonjwa 6 na kule Lulanzi-Kibaha tuna wagojwa 24 walio wengi wana hali nzuri na katika hospitali za private tunashukuru tumekuwa na ushirikiano na kuna wagonjwa wa aina mbalimbali ambao wana magonjwa tofauti pamoja na kwamba wana ugonjwa wa Corona"
 
Hii yote ni kwa juhudi ya serikali ya awamu ya tano au chadema mnasemaje..?😅
 
Kipindi corona inaanza tuliambiwa wasemaji ni 3 tu yani raisi, waziri mkuu na waziri wa afya sasa huyu katibu vipi tens

Hizi takiwimu itakuwa za kupikwa na ndio maana bi Ummy amekataa kuzitangaza inawezekana bi Ummy amefunga hivyo hawezi kudanganya

Mimi hizi siziamini nasubiri zitakazo tangazwa na Ummy hata kama miezi 3 ijayo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunadanganyana hapo.Ugonjwa unapunguaje wakati hakuna upimaji.
 
Hii inaitwa "Goal corner" kama lile la Paul Nonga Lipuli V Yanga

Yaani mpira unaingia golini halafu mwamuzi anasema lile siyo goal na si offside wala mpira wa adhabu cha ajabu badala uwe goal kick anaamuru iwe corner.

Madereva wa malori pekee kwenye border ya Namanga tu waliopimwa upande wa Kenya ni wengi kuliko tulionao kwenye vituo rasmi.
 
sasa usiowajua una uhakika gani kama wanachokuambia ni kweli ?
Kwa hiyo mtu atatoka huko aje kuripoti uongo? Na inapotokea mpaka maiti yanamkuta bado watakuwa ananiambia uongo? Ukiwa unafanyakazi sekta ya afya, haina maana unamjua kila mgonjwa na pia sio kwamba hautaguswa na ukweli wa yanayowasibu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakifa wanazikana wao kwa wao ina maana hata mortuary wanaogopa kupeleka maiti zao zitapata Corona?

Kwa theory hii maana yake mortuary zingefurika na misiba huko mitaani ingekuwa kila kona.
Unaujua uhalisia wa aliyefia hospitali kwa korona au unaishi wapi? Hujui kuwa ndugu hamtamzika ndugu yenu? Kuna wanaoiba maiti za ndugu yao mara tu anapofariki kuepuka hilo, sasa nani atapeleka kuhifadhi mwili hospitali ilhali anajua atapokonywa na kuna uwezekano asiruhusiwe kumzika?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wapo watakaouliza kuwa hiyo idadi inayopungua ni pamoja na wale madereva wanaokutwa na corona mipakani hasa mpaka wa Kenya. Alafu wame prove vipi kuwa idadi inapungua wakati tume ipo kwenye uchunguzi wa maabala, au pengine yamedhibitiwa magonjwa hatarishi ya corona ndio maana watu wanapata nafuu na kuruhusiwa kutoka hospital.
 
Back
Top Bottom