DOKEZO Serikali Ifanye Uchunguzi Wa Kifo Cha Dkt Faustine Ndugulile Na Kuongeza Ulinzi Mzito Kwa Dkt Tulia Ackson

DOKEZO Serikali Ifanye Uchunguzi Wa Kifo Cha Dkt Faustine Ndugulile Na Kuongeza Ulinzi Mzito Kwa Dkt Tulia Ackson

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Ccm Huwa mnafirahi kuua wapinzani

Sasa mnaanza kuuana wenyewe kwa wenewe

Nchi ya ajabu hii eti ccm mnaua think tanks wenu mnabakiza manungayembe kama Kipara, goli la mkono na kifua kipana, hakika maendeleo tutayasikia china
Acha maneno ya uongo na uzushi
 
Huyo TULIA WAKO wampe ulinzi mkali kama nani MUNGU AKIMTAKA HATA MUMUWEKEEE ULINZIBWA SHOT YA UMEME ATAKWENDA TU
NA WAHUNI WAKIMTAKA APATITIWA TU SO JIRINDE WW KAAAA AKIJUA ILINZI WA KWELI NI UNATOKA KWA MUNGU
 
Tulia hana madhara kwa ccm
Ametusaidia Kuuza bandari
Alitusaidia kudhibiti hunge
Ametusaidia kumfukuza dungai
Anasaidia kutoiwajibisha serekali

Si Dhani kama Kuna anayefikiria kumdhuru
 
Kuwa tu kwenye eneo fulani kuwazidi wenzako tayari unakuwa upo kwenye vita na baadhi ya watu ambao unakuta walikuwa wanatamani wao ndio wangekuwa hapo.ndio maana hata ungekuwa mwema vipi lakini bado huwezi kupendwa na kila mtu.
Vipi nyumbani kwenu kuko salama?
 
Unataka niweje na kufanya nini ndio uamini kuwa mimi ni mkulima.
Yaani mwanaume mzima stable anaejiamini na anatumia kipato chake halali kuendesha familia yake, hata kama kipato chake ní kidogo hawezi kufanya upuuzi kama unaoufanya. Naamini hata madam president amesha tambua dhima yako ndo maana hakupi uteuzi.
 
Yaani mwanaume mzima stable anaejiamini na anatumia kipato chake halali kuendesha familia yake, hata kama kipato chake ní kidogo hawezi kufanya upuuzi kama unaoufanya. Naamini hata madam president amesha tambua dhima yako ndo maana hakupi uteuzi.
Kwani wapi nimesema natafuta uteuzi hapa jukwaani.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Ifike mahali kama Taifa tusikubali kila kifo kipite hivi hivi au kuacha mambo yaende hivihivi kana kwamba hakuna kilichotokea vile au kusema ni Mapenzi ya Mungu au kuona ni kawaida.Mungu ametupatia akili kwa ajili ya kufikiri na kufanya tafakari kwa msaada wake Mungu Mwenyewe.

Ikumbukwe hii ni Dunia yenye vita vya kila aina ikiwepo kuhujumiana,kudhoofishana na kumalizana kwa kila mbinu .ambavyo vinakuwa vinafanywa kwa akili na maarifa ya hali ya juu sana na kufanywa na watu wenye akili za hali ya juu sana na ambao wapo kwa ajili ya kazi hiyo tu na wamefundishwa na kuivishwa kisawasawa.

Ifahamike kuwa wakati Mwingine kama Taifa linaweza kumalizwa na kutafunwa kama ugonjwa wa kansa kwa kumalizwa viongozi wake hasa wale wenye maono,akili kubwa,upeo,maarifa na ufahamu mkubwa wa masuala mbalimbali.watu wanaweza wakawa wanamaliza viongozi na watu wako muhimu pasipo wewe kujua .unapokuja kushituka ni wakati huna uwezo wa kusimama tena kukabiliana na hujuma hizo kwa sababu unakuwa tayari umepoteza watu wote wale wa muhimu.

Hivyo ni muhimu sana tuanze utaratibu wa kufanya uchunguzi wa vifo vya watu wa muhimu au viongozi pale inapotokea vifo vya ghafla na vyenye kutatanisha ili kuweza kujua ni vifo vya Mungu au vyenye mikono ya Binadamu. Kumbukeni hapa Majuzi tu tumepoteza kiongozi mashuhuri na muhimu sana hapa Nchi ambaye ni Mafuru.na sasa tumempoteza mwingine mtu wa muhimu sana kwa Taifa letu Dkt Faustine Ndugulile.

Lakini tujiulize huko India tumepeleka viongozi wetu wangapi katika kumbukumbu zetu na wangapi wamepoteza Maisha. Ni wakati wa kufumbua macho sasa kama Taifa kwa idara zetu za Ujasusi ndani na nje ya Nchi katika ulinzi wa viongozi wetu muhimu na watu muhimu.maana kuhujumiwa unaweza kuhujumiwa kwa njia mbalimbali ikiwepo hata wafanyabiashara wako wakubwa na wenye mitaji mikubwa na wenye mchango mkubwa kwa Taifa kupotezwa.

Lakini ni wakati pia wa kumuangalia Dkt Tulia kwa jicho la kijasusi zaidi kwa kujua kuwa anawakilisha Taifa letu huko Nje ya Nchi.hivyo ni Muhimu kumuongezea ulinzi zaidi awapo ndani na nje ya Nchi.Maana ikumbukwe ya kuwa hata katika kugombea hakugombea peke yake na hivyo siyo kila mmoja anapenda kuona Taifa fulani likiwa linang'ara katika nafasi za kimataifa kama ambavyo ilikuwa tumepata kwa Dkt Faustine Ndugulile kuongoza WHO kanda ya Afrika pamoja na kuwa na Dkt Tulia upande wa IPU.

Kwa hiyo kwa nafasi ambazo watanzania wanapata kuongoza taasisi za kimataifa tuhakikishe tunaongeza ulinzi ikiwepo kwa yule ambaye yupo kwenye masuala ya Fedha. Tukilala unaweza shangaa unafanyiwa hujuma na kupigwa mapigo makubwa makubwa mahali panapouma na kuacha majeraha,mapengo na alama zisizofutika wala kuzibika.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
KIFO NI KIFO TU.
 
the suprime hospital yetu ni muhimbili, nategemea ndipo matibabu ya juu kabisa yapo pale. sasa siku za karibuni naona ile kasumba ya kutibiwa india inarudi kwa kasi.

lakini najiuliza huyu boss siku ya gorofa kariakoo alifika wa kwanza na cha ajabu hata ambilance ya ofosini kwake hakujanayo. nawasiwasi na ufanisi wa huyu bwana mkubwa ipo haja atupishe ofisi ya umma
Ni kilaza na porojo nyingi
 
Back
Top Bottom