Serikali ifungie tovuti zote za pichani za ngono ili kuokoa vijana wetu

Serikali ifungie tovuti zote za pichani za ngono ili kuokoa vijana wetu

marco polo jr

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2020
Posts
362
Reaction score
1,771
Wakuu.

Nimependa leo tujadili suala hili, mitandao ya ngono inaharibu vijana wetu pamoja na utamaduni wetu kama waafrika. Ilikuwa siyo kawaida kuona picha za faragha kwani ilifahamika ni jambo la aibu kuona na pia kulikuwa na hofu fulani.

Zamani kidogo kuona picha hizi ilikuwa lazima ulipie unaenda jumba la sinema unaangalia. Kutokana mabadiliko ya sayansi na teknolojia leo picha hizi zipo bure kabisa mtandaoni, watu wakisuuza macho na kufurahia kutazama picha chafu hizo.

Kutokana vijana kushindwa kuchuja wanavoviona wao wanaamua kuiga mambo yote na matokeo yake ufirauni umekithiri katika jamii na maadili yanaporomoka kwa kasi.

Tuungane kukemeea huu ujinga, yule anayeangalia anashusha utu wake, wale wacheza filamu hizo wengi wapo katika stress kubwa huishia kutumia madawa ya kulevya hata kujiua.Nashauri serikali ifungie tovuti hizi za ngono ili kunusuru kizazi hiki.

Mwisho
 
Mtoa mada na yeye ni mfuasi mkubwa tu inaonekana....
Point ni kwamba kila mtu afuate maisha yake wewe pamabana kivyako na mm nitapambana kivyangu...kuwekeana limit ya mienendo ya kimaisha ni ubebari huo hali ambayo kwa karne hii haipoo!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom