Serikali ifute somo la historia mashuleni libakie kama somo kwa wanaosomea mambo ya mortuary

Serikali ifute somo la historia mashuleni libakie kama somo kwa wanaosomea mambo ya mortuary

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Posts
36,900
Reaction score
52,056
Somo la historia lifutwe mashuleni linapotezea muda watoto kusoma mambo ya maana
Somo utadhani mko makaburini kutwa mtu unasomeshwa habari za marehemu.

Mwalimu wa historia anakuja ohh Leo tunajifunza habari za marehemu chifu Mangungo, siku ingine marehemu Mkwawa, kesho tunasoma habari za marehemu kinjekitile, siku ingine tunasoma habari za marehemu Hitler, siku ingine tunasoma habari za marehemu Nyerere, Karume au marehemu Mandela

Yaani mtu darasani hadi nywele zinasimama kwa woga utadhani mko makaburini

Hilo somo lifutwe mashuleni liwe linafundishwa tu kwa wafanyakazi wa mortuary na MC wa misibani wanaosoma wasifu wa marehemu
 
Sijui umewaza nini kwa bandiko lako hili. Historia haifundishwi kwa kuifungamanisha na marehemu. Kama kuna mwalimu alikufundisha hivyo alikuibia ada. Kadai urudishiwe ada yako.

Historia ni mtiririko wa matukio yaliyotendeka zamani. Kamwe historia haijawahi kuwa wasifu wa marehemu. Huyo aliyekufundisha hivyo kwa kweli alikupotezea muda na anapashwa kutupwa jela.

Labda mitaala inayoandaliwa na CCM ndiyo inayokudanganya kuwa historia ni wasifu wa watu waliokufa badala ya matukio yaliyotukia zamani, sababu zake na hadhira yake.

CCM inawahujumu sana. Mtafakari sana mnaoishi chini ya CCM muitoe madarakani ili muweze kusoma mambo yanayoendana na dunia ya kisasa.
 
Historia ni mtiririko wa matukio yaliyotendeka zamani. Kamwe historia haijawahi kuwa wasifu wa marehem
Asilimia 90 ya somo la historia Ni habari za marehemu
 
Kama huwezi kujua ulipotoka ni ngumu sana kujua unapokwenda.
Mtoto huzaliwa akiwa hajui anakotoka lakini hujua anakokwenda.Hoja Haina nguvu hii
 
Kaandika naye habari za marehemu kwenye kitabu chake. Wote anaowataja kwenye kitabu chake Ni marehemu

Si sahihi kusema ameandika kwa Marehemu, ni mafunzo tunapata kupitia Wazee wetu wa Zamani, inakuwa Kama reference kwetu kwa maamuzi yetu ya sasa, ndio maana hata Marekani na kwingineko huwa wana declasify info zao yote ni kupata rejea ya vilivyotendeka
 
Sitaki nihusishe na uccm wako ila kitaaluma zaidi ni kwamba lengo la historia ni kutukumbusha tuendako na kupredict future.Ndio maana dunia leo inapendelea haki za binadamu kutokana na makosa yaliyotokea huko nyuma yakasababisha uhalifu wa kivita,ya kwanza na ya pili ya dunia,kukatokea Great Economic depression ndo maana leo tunakataa mtu anayefanya miradi bubu kwa mabilioni ya wanyonge.Pia inatupa kujua kuwa nchi yetu haikupata uhuru kwa damu hivyo sisi leo hatuwezi kutafuta uhuru wetu kwa damu,nchi kama kenya wao wanadai uhuru kwa damu kwa sababu wanaamini bila damu uhuru wao usingepatikana.Leo tunapinga ubaguzi kwa sababu tunajua kuhusu soweto massacre,Rwanda Genocide,mauaji ya wayahudi,.n.k ndio maana tunamshangaa Magu anavyobagua watu kwa misingi ya vyama na ukabila.

Katika historia tunajua utamaduni wetu n.k
Yapo mengine mengi naweza hata kuandika kitabu kupitia hayo.
 
Back
Top Bottom