History au historia huenda mbali zaidi hata suala la kusoma na kuchambua matendo ya kiongozi, kikundi cha watu wenye ushawishi au chama cha siasa ni sehemu ya somo la historia.
Historia kama somo lipo ktk nyanja mbalimbali kama military history, utabibu, jiografia, uhandisi, siasa, sosholojia, usafiri wa majini (marine), elimu ya nyota n.k
Tutazame historia za kisiasa zinazohusu utawala wa dola na watu ambacho ni kipengele kidogo ktk somo la historia, hususan utawala wa awamu ya 5 wa CCM kulinganisha na tawala (awamu) za CCM zilizopita katika siasa za nchini Tanzania.
Kumeibuka hoja ya kufuta somo la historia ktk mitaala ya shule Tanzania moja ya sababu ni somo la marehemu , somo la kututia unyonge watu weusi dhidi ya watu wa rangi nyingine n.k Hoja zote hizi ni mufilisi.
Sababu kubwa ya kutaka kufuta somo la historia ni woga wa watawala waliopo madarakani na kukiogopa kivuli cha historia inayosuta matendo yao.
Ndiyo maana hufanyika juhudi kubwa watawala conqurers kuharibu kufuta historia ya jambo lolote kubwa ktk jamii wanayoitawala ili watawaliwa wasipate sehemu ya kufanya rejea ya matendo ya watawala waliopo madarakani.
Mfano katika nyanja ya historia ya siasa hapa Tanzania, utawala wa awamu ya 5 umejitahidi kujitabanisha na utawala wa awamu ya Nyerere lakini wameshindwa na imekuwa mwiba mchungu kwao.
Ila cha kushangaza upande wa upinzani unaweza kumtumia Mwalimu Nyerere wa CCM ya zamani kama role model wao wa kushawishi, kutoa angalizo na kuiga maono yake kuhusu mustakabali wa ujenzi wa taifa moja lenye upendo litakalo zuia uvunjifu wa amani na kuleta maendeleo huku watu wakiwakubali wapinzani kuwa maadui wa kweli wa Taifa ni ujinga, njaa, maradhi na rushwa.
Kila wakipata nafasi ktk media utawaka wa awamu ya 5 wa CCM wakijenga hoja kuwa wayafanyao yanafanana na ya Mwalimu Nyerere hakuna anayekubali hivyo ktk jamii ya kitanzania wawe wazee au sisi vijana tunaosoma maandiko ya CCM ya Nyerere na kusikiliza clips za Nyerere tunaona hakuna ambacho awamu ya 5 ya CCM inaweza kujibainisha na CCM / TANU / TAA / AA ya babu zetu na baba zetu.
Mwanahistoria guli wa JamiiForums mwanaJF Mohamed Said katika makala zake nyingi hapa JamiiForums katika jukwaa la historia ya vuguvugu la siasa za ukombozi wa Tanganyika ametusimulia mengi sisi vijana kuhusu ukweli wa mababa wa siasa za ukombozi wa Tanganyika ni kina nani.
Na sasa kipindi chetu kunajitokeza hoja za kutaka kufuta historia ya kilichojiri tangu CCM ilipoasisiwa mwaka 1977, Azimio la Zanzibar, uanzishwaji wa vyama vingi vya siasa 1992, Nguvu na ushawishi wa vyama vingi ktk chaguzi mbalimbali n.k yote siyo kwa faida ya nchi bali kikundi cha kusifu na kutukuza cha awamu ya 5 ya CCM.