Serikali ifute somo la historia mashuleni libakie kama somo kwa wanaosomea mambo ya mortuary

Serikali ifute somo la historia mashuleni libakie kama somo kwa wanaosomea mambo ya mortuary

Naunga mkono,historia ibakie kama General studies tu. Tusome kwa starehe kutaka kujua mambo ya zamani na sio kulazimishani huku likipewa uzito sawa na hisabati.

Kuna haja ya kutazama mitaala yetu,dunia inaenda kasi sana.

Mbadala wake liwekwe somo la OSHA.
 
Kuna wakati unatamani kungekuwa na usaili was watu kujiunga kwenye majukwaa ya mijadala Kama JF!
 
Panama city , Panama
Military History Documentary
Jenerali Manuel Noriega katika historia ya watawala wa Latino Amerika. Mmoja wa viongozi ktk historia wanaokumbukwa siyo kwa mazuri bali jinsi walivyotawala nchi kwa kutumia 'mkono wa chuma'.

Jenerali Manuel Noriega alikulia kijijini kwao karibu na mpaka wa nchini yake ya Panama na nchi jirani ya Colombia. Utotoni Noriega alipata bahati mbaya na kuugua ugonjwa wa surua ulioharibu uso wake kiasi cha kupewa jina la utani la 'uso wa tunda la nanasi' - a.k.a Lapina. Pamoja na majanga hayo alifanikiwa kujiunga na elimu ya sekondari katika shule bora ya vipaji mjini Panama city na kujifunza masomo ikiwemo humanities ( arts na history).


Source: Military learning

Ndoto zake Noriega akiwa shuleni ni kuja kuwa Psychiatrist au president wa taifa la Panama. Akiwa shuleni alianzisha kikundi cha vijana wenziwe wa kisoshalisti ili kupinga siasa za kibwanyenye na ubeberu. Noriega alijufunza kwa bidii sana masomo yake lakini hakuweza kufaulu vizuri kutimiza ndoto ya kuwa daktari maana alikuwa average student.

Pamoja ya kushindwa masomo chuoni Noriega aliweza kuajiriwa kama chemist / muuza madawa ktk duka mjini Panama city. Bahati nyingine ikamuangukia Noriega baada ya kutambulishwa kwa kaka yake wa tumbo lingine aliyekuwa anafanya kazi ubalozini mjini Lima, nchini Peru. Akamfahamisha Noriega kuna skolashipu za chuo cha Kijeshi kama atapenda kujiunga na jeshi.

Lakini Noriega alikuwa tayari ana umri wa miaka zaidi ya 20 wakati Chuo kilihitaji awe chini ya miaka 20 , kwa kutumia ujanja wa mjini Noriega aliweza kupata cheti kipya cha kuzaliwa na ghafla umri wake ukawa miaka 18 yaani miaka 4 pungufu ya umri wake halisi. Hivyo Noriega akaweza kupata skolashipu hivyo na kujiunga na chuo cha Kijeshi nchini Peru kwa mafunzo.

Baada ya miaka 4 ktk chuo hicho cha Kijeshi nchini Peru, Noriega alifanikiwa kuhitimu degree ya uhandisi na kurejea kwao Panama. Akapangiwa kazi ya kuwa surveyor. Siku moja alimtembelea rafiki yake katika kambi ya Polisi National Guards pwani ya pacific.

Bahati ya mtende ikamwangukia maana Kanali mmoja kamanda wa Jeshi la Polisi la National Guards machachari, mtoto-wa-mjini na maarufu Omar Torrijos alitembelea pia kambi hiyo ya Polisi, hivyo ghafla bin vuu surveyor Noriega akakumbana uso kwa uso na colonel Omar Torrijos. Noriega akajikuta ana stand attention kijeshi bila kujijua, Kanali Torrijos akagundua kuwa huyu kijana Noriega amepitia mafunzo ya kijeshi.

Kanali mtoto wa mjini Omar Torrijos akamwalika Noriega ktk sherehe maalum na kumshawishi ajiunge na jeshi maalum la National Guards huo ukawa mwanzo wa nyota ya Noriega kupaa kwa kasi jeshini.

Luteni Manuel Noriega akateuliwa kuwa mkuu wa intelehensia jimbo moja la Kusini la Panama. Noriega kutokana na cheo hicho alipelekwa kwa mafunzo zaidi na ripoti ya kadi ya mafunzo yake ktk maktaba ya CIA ilionesha alikuwa mwanafunzi mzuri yaliyepata alama za juu ktk somo la Psychological warfare. Somo lililokuwa muhimu katika kupambana na wapinzani wa Kikomunisti.

Omar Torrijos swahiba wake Manuel Noriega, akaongoza mapinduzi ya kijeshi nchini Panama na kukoleza vita dhidi ya mabeberu waliokuwa wanamiliki mfereji maarufu wa usafiri wa meli kubwa za baharini wa Panama canal.

Mabeberu hawakupenda sera za mapinduzi za Omar Torrijos hivyo wakapanga mapinduzi kumgoa Omar. Wakasubiri Omar Torrijos akiwa safarini Mexico na kuandaa mapinduzi ya mengine. Omar Torrijos kusikia mapinduzi hayo akamuagiza swahiba wake Kapteni Noriega kuzima jaribio hilo.

Kapteni Manuel Noriega alifaulu kuzima jaribio hilo na kufanikisha kurejea Panama Jenerali Omar Torrijos. Omar alirejea kishujaa na wakapanda gari moja la wazi pamoja na Noriega wakipita mitaani huku wakipunga mikono kwa wananchi wengi waliojitokeza kuonesha mshikamano dhini ya mabeberu.

Baada ya tukio hili la Manuel Noriega kufanikiwa kuzima jaribio la mapinduzi dhidi ya Omar Torrijos mara kwa mara kiongozi huyo mwana-mapinduzi wa Panama alisikika akimwita kapteni Noriega kishikaji kama 'kichaa wangu' a.k.a gangster wangu. Na kwenda mbali zaidi Dikteta Omar Torrijos akasema Noriega anajua nini cha kufanya hata bila ya kumwambia, anachohitaji Noriega ni wao kutazamana machoni tu na tayari kila mmoja anajua nini kifanyike.

Noriega nyota yake ikazidi kupaa na akapewa cheo cha u Luteni Kanali na kuwa mkuu wa military intelligence akitambulishwa kama G -2. Kupitia wadhifa huo mpya wenye nguvu, Lt Kanali Manuel Noriega akawa masikio na macho ya Diktekta Omar Torrijos kwa Noriega kufungua mafaili ya siri kuhusu taarifa za viongozi wote ktk serikali na wale wapinzania wa diktekta huyo. Hivyo Noriega aliogopwa na wengi hata wale waliokuwa na nyadhifa kubwa kuliko Noriega.

CIA hawakuwa mbali ktk kufuatilia nyendo za Noriega na kufungua faili la siri kutunza ripoti za habari lukuki kuhusu kamanda huyu 'mzalendo' nambari moja na kutabiri siku za usoni anaweza kuwa Kamanda Mkuu wa Majeshi yote na hata kiongozi diktekta wa Panama.

Utabiri wa CIA kuhusu 'nyota' ya Manuel Noriega ulitimia baada ya ndege iliyombeba Diktekta Jenerali Omar Torrijos ilipoanguka ktk milima ya Panama mwezi Julai 1981. Uvumi kuhusu ajali hiyo ulizagaa kuwa kulikuwepo bomu ndani ya ndege na kuwa Manuel Noriega alihusika kulipenyeza humo.

Uchunguzi wa ajali hiyo ya ndege iliyopora maisha ya Jenerali Omar Torrijos ulibaini ni ajali tu ya kawaida ya ndege na siyo kama uvumi ulivyokuwa umetapakaa kuwa Noriega anahusika. Miaka miwili ya msuguano wa nani amrithi Omar Torrijos ilipita na hatimaye Manuel Noriega akaibuka kama kiongozi wa Panama. Hii ilichukua muda kutokana na viongozi waandamizi wa kijeshi na kisiasa kumuona Noriega si mwenzetu, ni 'wakuja' asiye na ushawishi wala makundi ya kumbeba kuweza kuongoza nchi kama Rais.

Baada ya utawala wake wa miaka 6 kama Kiongozi wa Panama, Jeneralia Manuel Noriega aliondolewa madarakani na jeshi la Marekani mwaka 1989 kisha kupekekwa nchini Marekani na kupatikana na hatia ya kuhusika na kushiriki katika kusaidia madawa ya kulevya kuingia Marekani. Alihukumiwa miaka 40 jela na baada ya miaka 20 aliachiwa na kufunguliwa mashtaka mengine nchini Ufaransa lakini akaachiwa na kurejea nchini Panama kufunguliwa mashitaka ya kuwapoteza wapinzani wake.

Mr. Noriega in 2011, after he was flown home to serve 20 years for the disappearances of political opponents in the 1980s.

Mr. Noriega in 2011, after he was flown home to serve 20 years for the disappearances of political opponents in the 1980s.Credit...Esteban Felix/Associated Press
 
Kujifunza mambo yaliyopita kunakufanya uweze kutambua yaliyopo,ili uweze kuchanganua yajayo.fikiri kwanza kabla ya kuandika.
 
kwa hiyo na hizi dini za uislam na ukristo nazo zifutwe, maana zinazungumzia manabii waliokufa
 
Yani CCM ndo manataka tujenge taifa la ma mbumbu plus..sasa tukitoa historia tutajuaje tulipotokea,tulipo na tunaelekea wapi..
 
Mara binaadam wa kwanza alikua Nyani lakini alitokea Africa, sijui wazungu wao walitokea wapi?
Dini inasema binaadam wa kwanza alikua Adam na Hawa.
Tatizo mnaiangalia historia katika udogo sana

Hakuna taifa duniani ambalo wananchi wake wanajielewa au tu kuwa na uzalendo na nchi yao pasipo kuijua historia yao vizuri...

Leo hii Korea ni nchi kubwa lakini haijapuuza historia yao ya B.C na bado wanaitumia kutengeneza series ili kusambaza culture na phylosophy yao dunia nzima... hii ni history

Leo U.S.A inaitwa the land of the free, the land of the brave.. Phylosophy ambayo wanayoisambaza dunia nzima. Hii ni history inayowapa supremacy

Leo hii kuna kama ldc tunapigana na umaskini ila kuna Asian tiger economies na CHINA zilizotoka tulipo. Ni reference tu tungefanya plus Africanization of the solutions

Unakutana na mtu haelewi hata UN ama international organisations nyingine ni nini ??.. Hajui hata cold war wala neo colonialism. Kwa sababu anajua kusoma na kuandika mnampa ubunge. what a crisis

Leo hii Tz kuna mambo yanayoendelea kuanzia kisiasa, kidini na kiuchumi.. unadhani kuna jipya hapo HAKUNA... watanzania wangeijua historia wangekuwa na jicho la tatu kuelewa kila kitu ila ndo hivyo. Tusome tujibu mitihani PATHETIC
 
Eyce,
Lol,
Naelewa bro History na umuhimu wake, i was just entertained nina uhakika hata mtoa mada hayupo serious kama wengi mlivyochukulia.
 
ngusillo,

Sasa hapo CCM imeingiaje? Mlela mada Ndio akili yake imeshindwa kupanuka akaelewa why ni muhimu watu kujua history ya mazingira yao (yani kila kinachowahusu)... Sasa unapomuelewesha kwa kuweka ishu za CCM unapoteza lengo. japo siasa ni sehemu ya historia lakini ulivyoiweka imepoteza ladha
 
Ndio maana elimu ya Wakenya ipo juu zaidi ya everybody in East Africa! Ndio maana Wakenya wanaajirika zaidi ya kenge wote!

Kukwepa elimu huku! Taifa lina watu wajinga from East to West,North to South! Sijui nini tutaweza kwenye hii dunia
 
Kuna majukwaa yana nyuzi za kijinga sana. Ndio nini sasa hii?
 
Kafutwa kabisa nakubaliana na wewe ila sababu za kufutwa natofautiana kabisa na wewe.
 
Umenifurahisha sana eti somo la marehemu hujui ata wewe ni marehemu to be
 
Back
Top Bottom