Serikali ikemee kwa nguvu zote wanaodai Hayati Magufuli kauawa, iondoe video zote YouTube na kuwasaka wahusika

Duniani Hakuna mwanadamu yeyeto aliyewahi pambana na watu na akawashinda.Pambana na maendeleo usipambane na watu.Ukitaka kufika salama tembea na watu
 
Kwa mtazamo wangu naona ni Bora serikali iendelee hivihivi kupuuza UJINGA wa watu wachache kwasabb kama itaanza operations za kuwasaka hawa wapuuzi itazidi kuleta taharuki kubwa.
ukweli huwa na tabia ya kujisimamia wenyewe ndiyo maana serikali imeona haina haja ya kusumbuka na wajinga wachache.

kama bado kuna watu wanabishana na MUNGU juu ya Kifo cha POMBE kuna haja gani ya kusumbuka? MUNGU amemchukua magufuli kwasabb zake
 
Alikuwa na ulinzi kama tupo Iraq hao maadui wangepenyea wapi.Huu ni uzushi tu wa watapaji.
 
This country will stay.People will come and go.Maisha yaendelee
 
Binafsi sipendi huu uzushi wa kila siku tunaambiwa JPM aliuawa na watu fulani kwa namna fulani lakini wakiambiwa wawasilishe ushahidi wao katika maeneo yanayohusika hawafanyi hivyo.
Hili watu wote hawafanani uelewa kwa hiyo Hawa wazushi wanapotoa hizi taarifa zao Kuna watu wanaamini na kubaki na msimamo huo kuwa JPM aliuawa.
Hata tunapenda uhuru wa vyombo vya Habari sio kwa kiasi cha kuzushia mambo ambayo hawayatolei ushahidi.
 
Huyu bwana alikufa kwa sababu ya uoga wake wa kwenda kutibiwa kwa mabeberu,sijui hofu yake ilikuwa mini,mbona Mugabe alikuwa hapatani na wazungu lakini alikuwa anaenda kutibiwa Singapore na hawakumdhuru
Point mkuu,,big point
 
Sie tumekubali kuwa alifariki na alikua kipenzi Chetu na bado tunampenda, lakini wao kutwa kila siku kugombana na marehemu!! Hiyo teyari ni laana washakua mazombie.
Nasikia amewahi kuhonga nyumba ya umma kwa kimada akiwa waziri?
 
Nasikia amewahi kuhonga nyumba ya umma kwa kimada akiwa waziri?
Alishinda uchaguzi kwa kishindo na tulimzika baada ya kufariki kwa mapenzi makubwa vilevile.
 
Mimi nadhani wana haki ya kitowa maoni yao kama wewe ulivyotoa ya kwako kwa mujibu wa sheria. Hakuna dhambi katika mtu kufikiria tofauti na mwingine. Wako sahihi kama wewe ulivyo sahihi. Na hata hivyo yote yanawezekana chini ya jua.

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
 
Kashfa za kipuuzi sana hizo na wajinga wengi wanaziamini na wengi wao wanaamini Vasco pia ni muhusika.
mara oohhh wakora walitumwa ila mtt w town akasanda afu ndo aka retaliAte@@akaliwa timing safiiii
 
Ni bora walete huo ushahidi, maana mambo ya kuzusha siyo mazuri...
 
Mkuu

Kwa hiyo wewe ni mmoja wa wahusika mbona unapiga kelele kuzuia wengine kupaza sauti zao?

Undeni tume huru ya uchunguzi kuhusu madai haya badala ya kutoa vitisho kwa wananchi wanaotoa hisia zao kutokana na kuumizwa.

Wewe ndio unajiona unahaki ya kusema chochote chenye majungu usikilizwe ila wenzio wanyamazishwe?

Kitu gani kinafichwa mpaka unadai video zoteyutube zifutwe?

Hapo hamuwezi kuwaziba midomo hao watu na wana ushahidi wa kutosha kwa mjibu wa maelezo yao hivyo kuwatisha ni kosa la jinai
 
Kuwaziba Watu Midomo ni kazi nzito sana kuwapuuza ni kazi rahisi sasa hapo unatakiwa uchague.
Naomba niongee hili toka rohoni na nitangulize kuomba radhi kwa watakaokwazika na hili andiko langu
Yeyote aliyehusika na kifo cha mwanakwenda awe pekeyake ama kikundi anastahili kupewa heshima kubwa na kutambuliwa kama shujaa wa Taifa...
 
Wewe ni mchochezi
 
Kama ushahidi wanao kwanini wasiupeleke kwa IGP au DPP au kwa Samia mwenyewe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…