Mtoa hoja uko sahihi, mimi pia, kiukweli, huwa sipendi hii tabia. Mara nyingi mimi naogopa hata kuzifungua clips za watu wa dini kwa kuogopa nitakayoyakuta huko. Lakini ungekuwa sshihi zaidi kama ungeenda 'deep' zaidi kwa kuangalia chanzo halisi haswa cha hali hii na kulisemea kuanzia huko.
Chunguza vizuri nyakati na aina ya makemeo yanayotoka kwa viongozi wetu wa dini kwenda kwa serikali. Kuna nyakati kiongozi mkuu wa serikali hana nafasi wala pumzi ya kupumua katika mipango yake ya kimaendeleo kama kiongozi. Kila mpango wake wowote wa kimaendeleo (kiuchumi) huingiliwa kwa lundo (rundo?) la waraka na matamko......yaani ni kama hakuna kuaminika na wao wanajivika u'filters' wa kila mpango wake. Nyumba za ibada na siku za ibada huwa maalum kwa matamko kila baasa ya sala. Haya hufanyika kijanja sana chini ya 'usomi' na 'uchambuzi' ulioshiba tu......kipengele kwa kipengele.
Wakati huo huo kuna nyakati mtawala mkuu hupata relief......ataingiliwa kwa mengine tu tena very partially lakini mipango yake ya nini akusanye na kivipi hata haijadiliwi sana. Shwari hutamalaki na mtawala hupata haki ya kutawala. Hayo, mtoa mada, kwa kujua au kutokujua, ndiyo yanayotuletea hali kama hizi unazozikemea sasa.
Nachukia haya mambo kwakweli.